Tafuta

Matokeo ya shambulio la anga katika mji wa Kyauktaw nchini Myanmar. Matokeo ya shambulio la anga katika mji wa Kyauktaw nchini Myanmar.  (AFP or licensors)

Leo XIV: Jumuiya ya kimataifa haipaswi kusahau mateso ya Myanmar

Mara baada ya Katekesi ya Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Papa aliwaalika waamini kuombea amani duniani, hasa kwa nchi ya Asia, huko Myanmar iliyokumbwa na miaka minne ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na mgogoro mkubwa wa kibinadamu.Hatimaye, akikumbuka siku kuu ya hivi karibuni ya Watakatifu Wote, aliwahimiza kila mtu kufuata "wito wao wa utakatifu."

Vatican News

Ninawaalika kuungana nami katika kuwaombea wale walioathiriwa na migogoro ya silaha katika sehemu mbalimbali za dunia. Nafikiria hasa Myanmar. Na naisihi Jumuiya ya kimataifa isiwasahau watu wa Burmiania na kutoa msaada wa kibinadamu unaohitajika. Huu ulikuwa ni wito wa Papa Leo XIV mara baada ya Katekesi yake katika  Uwanja wa Mtakatifu Petro, Jumatano tarehe 5 Novemba 2025   akiwaalika waamini kuombea pamoja amani kote ulimwenguni. Pia alitoa wito wa dhati kwa Jumuiya ya kimataifa kuja kuwasaidia watu wa Myanmar, walioathiriwa na vurugu za vita vya wenyewe kwa wenyewe na ukiukwaji mwingi wa haki za binadamu ambao umesababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu.

Miaka Minne ya Vurugu

Mnamo Februari 2021, jeshi lilichukua madaraka, na kuipindua serikali ya chama cha National League for Democracy (NLD), ambacho kilishinda uchaguzi mnamo Novemba 2020. Kikosi cha kijeshi, kilichoitwa Baraza la Utawala la Jimbo (SAC), kilijibu maandamano dhidi ya mapinduzi kwa nguvu, kikipiga vita vya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya makundi mengi ya kikabila yenye silaha yanayopinga. Mgogoro wa kijeshi umesababisha ukiukwaji mkubwa na ulioenea wa haki za binadamu, kama vile kuajiri kwa nguvu, kuwekwa kizuizini kiholela, na kunyongwa bila ya haki.

Uchaguzi Usio na Uhakika na Maafa ya Asili

Matumaini ya wakazi wa Myanmar ya serikali mpya iliyochaguliwa kidemokrasia pia yanafifia. Mkuu wa serikali tawala, Jenerali Min Aung Hlaing, ambaye ameongoza vikosi vya kijeshi tangu mapinduzi ya 2021, hivi karibuni alitangaza kwamba utawala unaoungwa mkono na jeshi, kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe, hautaweza kufanya uchaguzi mkuu ujao kote nchini. Pamoja na hali hii ya kisiasa, hali ya kibinadamu iliyozidi kuwa mbaya zaidi, iliyozidishwa na mafuriko mwezi Juni na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.7 la Machi 28, ambalo lilisababisha vifo vya takriban 3,700 na majeruhi 4,800, na kusababisha idadi ya watu waliokimbia makazi yao, kulingana na data ya UNHCR, kufikia zaidi ya milioni 3.5.

Mwezi Novemba, tunaomba kwa ajili ya mapumziko ya milele ya waamini waliofariki

Kwa wanaouzungumza Kiingereza katiia salamu  Papa alisema: “Ninawakaribisha kwa uchangamfu asubuhi ya leo mahujaji na wageni wote wanaozungumza Kiingereza wanaoshiriki katika Hadhira ya leo, hasa wale wanaotoka Uingereza, Ireland, Angola, Kenya, Nigeria, Tanzania, Australia, China, Hong Kong, Indonesia, Japani, Malaysia, Filipino, Kanada na Marekani.

Papa alielendelea kusema kuwa “ Wakati wa mwezi wa Novemba, tunaomba hasa kwa ajili ya mapumziko ya milele ya waamini waliofariki. Bwana aliyefufuka awaoneshe rehema zake, na tumaini linaloletwa na imani yetu katika Ufufuko liendelee kutufanya tuangalie na mioyo yetu kuelekea furaha ya Mbinguni. Mungu awabariki nyote!

Katika salamu zake kwa wanauzungumza Kiitaliano Papa alisema: “Ninawakaribisha kwa dhati waamini wanaozungumza Kiitaliano, hasa Kundi la GEN 3 la Harakati ya Wafocolare, Masista wa Mama Yetu wa Upendo wa Mchungaji Mwema, waamini wa Asti, Castel del Piano, na Lauria. Pia nawasalimu Wasalesian wa Caserta, Taasisi ya Hoteli ya "Filippo De Cecco" ya Pescara, na Chama cha Walimu Wakatoliki cha Italia.”

Papa wa Roma hakuishia hapo bali aliwasalimia “ kwa upendo washiriki katika Siku ya Jubilei ya Mazingira ya Kilimo kwamba: wapendwa, ninawashukuru kwa kazi yenu ya thamani, ambayo huzaa matunda ya dunia, na ninawahimiza kujitolea kila tahadhari kwa utunzaji wa Uumbaji. “

Mwaliko wa Utakatifu

Hatimaye, aliwasalimu vijana, wagonjwa, na wenye ndoa wapya. Kwa  msukumo wa Siku kuu ya Watakatifu Wote ya hivi karibuni, iliyoadhimishwa na Kanisa mnamo Novemba 1, kwa maneno haya Papa aliwaalika kila mtu kufuata mfano wake, kuchukua njia ya utakatifu na urafiki mkubwa zaidi na ujumbe wa Yesu Kristo.  Papa alisema:  “Sikukuu ya hivi karibuni ya Watakatifu Wote inanifanya nitafakari wito wa pamoja wa utakatifu. Sote tumeitwa kuwa watakatifu. Kwa hivyo ninawaalika mshikamane zaidi na Kristo, kwa kufuata vigezo vya uhalisi vilivyooneshwa na Watakatifu.”

Mara baada ya Katekesi
05 Novemba 2025, 16:34