Tafuta

Mkuu wa Shirika la Waagostinian,Pa R. Prevost(Papa Leo XIV sasa) na Ndugu zakewengine nchini Nigeria kunako 2016. Mkuu wa Shirika la Waagostinian,Pa R. Prevost(Papa Leo XIV sasa) na Ndugu zakewengine nchini Nigeria kunako 2016. 

Waagostinian watachapisha Kitabu cha Papa Leo XIV:tafakari zake akiwa Mkuu wa Shirika

Shirika la Waagostinian na Nyumba ya Vitabu Vatican(LEV) wametangaza uchapishwaji wa kitabu kipya chenye kichwa:"Free Under Grace:Writings and Meditations 2001-2013,"ambacho kinakusanya maandishi ya Papa Leo XIV wakati alipokuwa Mkuu wa Shirika la Waagostinian.

Vatican News

Katika hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya Vitabu huko Frankfurt mnamo tarehe 15 Oktoba 2025, Shirika la Mtakatifu Agostino na Jumba la Uchapishaji la Vatican (LEV) walitangaza juu ya uchapishaji wa ujao wa kitabu ambacho hakijatolewa cha Robert Francis Prevost,(Papa Leo XIV) chenye jina la “Free under Grace: Writings and Meditations 2001–2013,” yaani: “Huru chini ya Neema: Maandishi na Tafakari 2001-2023.”Kitabu hiki kinakusanya maandishi ya Papa wa sasa kutoka wakati alipokuwa akihudumu kama Mkuu wa Shirika hapo awali la Mtakatifu Agostino.  Kwa mujibu wa Padre Joseph Lawrence Farrell, O.S.A., Mkuu wa Shirika la sasa, alifafanua kuwa mkusanyiko huo ni  “muhtasari wa mada muhimu sana.”

Kugundua hali ya kiroho ya Papa Leo XIV

Kitabu hiki kinawapa wasomaji uangalizi wa karibu wa maisha ya kiroho na mawazo ya Papa Leo XIV kupitia kurasa ambazo hazijachapishwa hapo awali ambazo ni pamoja na tafakari, mahubiri, ambayo alitoa Padre Robert Francis Prevost wakati wa miaka yake kama mkuu wa Shirika la Waagostinian. Maandiko yote yanashirikisha hali ya kipekee ya kiroho ya kiagostino ambayo ilitengeneza Papa wa baadaye. Kitabu hicho kitachapishwa katika lugha Kiitaliano na LEV katika majira ya kuchipua ya 2026. Akitoa maoni yake kuhusu mpango huo, Padre Farrell alisema: “Kitabu hiki, ambacho kinaleta pamoja mengi ya mawasiliano ya Mkuu  Mstaafu wa wakati huo Robert Francis Prevost, O.S.A., kinatoa muhtasari wa baadhi ya mambo makuu aliyositawisha wakati wa miaka yake akiwa mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino.”

Chapisho linalotarajiwa sana

“Tunafurahi sana kushiriki katika Maonesho ya Vitabu vya Frankfurt kwa kuwasilisha kwa wachapishaji ulimwenguni pote kitabu hiki ambacho hakijachapishwa na Robert Francis Prevost, O.S.A.—sasa ni Papa Leo XIV,” alisema Lorenzo Fazzini, Mkurugenzi wa Uhariri wa Jumba la Uchapishaji la Vatican."Nakala hii itawawezesha wasomaji kugundua maandishi kutoka kipindi ambacho Papa alikuwa Mwanashirika wa Kiagostino na Mkuu wa Shirika hilo.  "Ni kitabu kinachosubiriwa kwa hamu na wasomaji ulimwenguni kote."

18 Oktoba 2025, 14:29