Tafuta

Sala ya Masifu ya adhuhuri pamoja Papa Leo XIV na Mfalme Charles wa Uingereza

Masifu ya adhuhuri ya Kiekumene kutoka katika Kikanisa cha Sistine mjini Vatican iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Leo XIV pamoja na Mchungaji Stephen Cottrell mbele ya Wakuu wa Kifalme,Mfalme Charles III na Malkia Camilla kutoka Uingereza.

Vatican News

Baba Mtakatifu leo XIV alikutana na Mfalme Charles wa Uingereza kwa njia hiyo Wafalme wa Uingereza walifika mjini Vatican saa 4:50 asubuhi, Alhamisi tarehe 23 Oktoba 2025 baada ya kupita na  kukaribishwa katika Uwanja wa Mtakatifu  Damaso, kulingana na itifaki ya ziara za serikali. Baada ya bendi iliyopiga wimbo wa taifa wa Kiingereza "God Save the King," pamoja na Walinzi wa Uswiss, Mfalme Charles III na Malkia Camilla, wakiwa wamevalia ngo rasmi waliingia kwenye Jumba la Kitume.

Wakati wa kungia katika Kikanisa
Wakati wa kungia katika Kikanisa   (@Vatican Media)

Kufuatia Mkutano wa Papa na wafalme, kama ilivyoripotiwa katika taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican, mikutano kadhaa sambamba ilifanyika: Malkia Camilla alitembelea Kikanisa cha  Pauline, wakati Mfalme Charles alikutana katika Sekretarieti ya Vatican na Kardinali Pietro Parolin Katibu Mkuu wa Vatican na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Mkutano huo ulilenga "mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi" na masuala kadhaa ya maslahi ya pamoja, kama vile ulinzi wa mazingira na mapambano dhidi ya umaskini. Uangalifu hasa ulipewa kwa "dhamira ya pamoja ya kukuza amani na usalama katika kukabiliana na changamoto za kimataifa." Hatimaye, tukikumbuka historia ya Kanisa la Uingereza, hitaji la pamoja la kuendelea kukuza mazungumzo ya kiekumene lilioneshwa.

Sala ya Masifu ya Adhuhuri
Sala ya Masifu ya Adhuhuri   (@Vatican Media)

Ahadi ya pamoja kwa uumbaji

Katika tarehe hii ya 23 Oktoba 2025, ibada ya maombi ya kiekumene, kwa Kilatini na Kiingereza, ilianza saa 6:20 jioni. Ni ushuhuda wa uhusiano mzuri kati ya pande hizo mbili, lakini pia utimilifu wa tamaa ya mfalme wa Kiingereza, Gavana Mkuu wa Kanisa la Uingereza, ambaye alinuia kuipatia nchi mwelekeo mkubwa wa kiroho, hasa wakati wa Jubilei ya Matumaini.  Ziara hiyo, iliyopangwa kufanyika mwezi wa Aprili, lakini baadaye ikaghairiwa kutokana na kifo cha Papa Francisko, ilikusudiwa pia kuakisi dhamira ya pamoja ya Uumbaji kati ya Mfalme Charles na Papa wa Argentina, miaka kumi baada ya kuchapishwa kwa Waraka wa Laudato Si'. Mada ambayo Papa Leo XIV alitaka kuendelea na kuzindua kwa upya.

Mtakatifu Ambrose na Mtakatifu Newman

Hali ya kiekumene ya huduma ilionekana mara moja katika wimbo unaotambulisha maombi. Andiko hilo ni la Mtakatifu Ambrose wa Milano, Mwalimu wa Kanisa, lililoimbwa katika tafsiri ya Kiingereza na Mtakatifu John Henry Newman, Mwanglikana kwa nusu ya maisha yake na Mkatoliki katika nusu nyingine. Mtaalimungu wa Kiingereza, aliyeishi katika karne ya 19, atatangazwa kuwa Mwalimu wa  Kanisa rasimi mnamo tarehe 1 Novemba 2025  na Papa Leo XIV. Mfalme Charles mwenyewe alihudhuria kutangazwa  kwake kuwa Mtakatifu , mnamo tarehe 13 Oktoba  2019, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Sala ya pamoja
Sala ya pamoja   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV alisimama pamoja na Askofu Mkuu  wa Kanisa la Uingereza, Askofu Mkuu Stephen Cottrell wa York. Walioandamana na wafalme hao walikuwa ni msimamizi wa Mkutano Mkuu wa mwaka huu, Mchungaji Rosie Frew; Askofu Mkuu wa Westminster na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Uingereza na Wales, Kardinali Vincent Nichols; na Leo Cushley, Askofu Mkuu wa Mtakatifu  Andrews na Edinburgh, anayewakilisha Uaskofu wa Scotland.

Kwaya na Liturujia

Ishara nyingine ya umoja  ilikuwa uwepo wa kwaya ya watoto wa Kikanisa cha Kifalme(Royal Chapel katika Jumba la Mtakatifu  James huko London, kwaya ya Kikanisa cha Mtakatifu  George katika Nyumba ya Kifalme ya Windsor inayoundwa na watu wazima, walioalikwa na Mfalme Charles na Camilla, na kwaya ya Kikanisa cha Sistine cha Vatican. Sherehe hiyo ilifuatwa na Zaburi ya 8 na kisha Zaburi ya 64, na hatimaye kusomwa kwa Barua ya Warumi, kwa Kiingereza ambayo mada yake ya msingi ni tumaini. Dhamira ya msingi ya nyimbo na liturujia iliyochaguliwa ni sifa ya ukuu wa Mungu Muumba. Kabla ya maombi kumalizika, wimbo wa  "If You Love Me" wa Thomas Tallis, uliochapishwa mwaka wa 1565, uliimbwa. Umechukuliwa kutoka katika Injili ya (Yh 14, 15), na kusoma: “Mkinipenda, mtazishika amri zangu; nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele.”

Sala ya pamoja
Sala ya pamoja   (@Vatican Media)

Aliyepiga kinanda ni mwanamuziki wa kifalme na mtunzi kwa zaidi ya miaka arobaini, na alitunga muziki kwa ajili ya liturujia ya Kirumi na Kitabu cha Kiingereza cha Maombi ya Kawaida. Papa na Askofu Mkuu Cottrell walisali sala pamoja kwa Mungu Muumba: "Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu, ukae nasi milele." Mwishowe, Papa Leo XIV na Mfalme Charles walitoka kwenye Kikanisa cha Sistine pamoja, wakitembea huku mtu akiendelea kutembea njia ya mazungumzo ya kidini licha ya tofauti zao.

23 Oktoba 2025, 12:38