Vatican:Papa akutana na Rais wa Jamhuri wa Lithuania
Vatican News
Jumatatu tarehe 6 Oktoba 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican, Rais wa Jamhuri wa Lithuania, Bwana Gitanas Nausėda, na baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirikia ya Kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi za vyombo vya habari Vatican, imebainisha kuwa “wakati wa mazungumzo mazuri, kati ya Sekretarieti ya Vatican walielezea, kupendezwa mahusiano mazuri yenye matunda ambayo yapo kati ya Vatican na Jamhuri ya Lithuania.
Katika “mazungumzo hayo aidha walisisitiza juu ya baadhi ya matatizo zenye tabia ya Kimataifa, kwa namna ya pekee yanayohusu vita nchini Ukraine, wameelezea ulazima wa kina wa kutafuta suluhisho ya kidiplomasia, kwenda mbali zaidi ya hatari zinazopanuka za migogoro zisizo tegemewa na matokeo yasiyoelezeka.”
Asante sana kusoma makala hii, ikiwa unakata kubaki na masasisho zaidi, tunakualika kujiandikisha hapa: Just click here
