Tafuta

Kimbunga kikali Melissa huko Jamaica. Kimbunga kikali Melissa huko Jamaica.  (AFP or licensors)

Maombi ya Leo XIV kwa Waathiriwa wa Kimbunga Melissa huko Jamaica na Cuba

Mwishoni mwa Katekesi,Papa alionesha ukaribu wake kwa walioathiriwa na dhoruba "mbaya" na kuwatia moyo viongozi wa kiraia"kufanya kila linalowezekana"kuwasaidia watu.Aliwashukuru Jumuiya za Kikristo na wanaojitolea kwa msaada wao.

Vatican News

Nguzo za umeme zilizoanguka, marundo ya uchafu, na magari yaliyozama kwenye maji yenye matope: hizi ni baadhi ya picha zinazowasili kutoka Jamaica, eneo la uharibifu uliosababishwa na Kimbunga kikali kiitwacho Melissa. Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatano tarehe 29 Oktoba 2025 mara baada ya Katekesi yake akiwa anatoa salamu kwa watu lugha tofauti mawazo yake  yaligeukia Caribbean, iliyokumbwa na dhoruba "mbaya", ambayo ilisababisha "mafuriko makali."

Kimbunga Melissa
Kimbunga Melissa

Kimbunga hicho kilitua Cuba, karibu na Chivirico, katika jimbo la Santiago ya Cuba, na tayari kimesababisha maelfu ya watu kuhama makazi yao na nyumba zilizoharibiwa, miundombinu, na hospitali kadhaa. Papa Leo aliwahakikishia kila mtu "ukaribu" wake na maombi kwa ajili ya waathiriwa, waliohama makazi yao, na wale wanaosubiri maendeleo ya dhoruba kwa "wasiwasi." Pia aliwasilisha mawazo yake kwa mamlaka za kiraia, kwamba wajitolee kufanya kila linalowezekana kupunguza uharibifu, na alitoa shukrani zake kwa jumuiya za Kikristo kwa msaada wao, pamoja na mashirika ya kujitolea.

kimbunga Melissa
kimbunga Melissa   (AFP or licensors)

Waziri Mkuu wa Jamaica Andrew Holness alitangaza kisiwa hicho kuwa "eneo la maafa" kufuatia kimbunga hicho, ambacho kilivuma kwa kasi ya hadi kilomita 300 kwa saa. "Ripoti ambazo tumepokelewa ni pamoja na uharibifu wa hospitali, uharibifu mkubwa wa mali za makazi, nyumba, na hata mali za kibiashara na kwa hiyo alieleza "athari mbaya za kimbunga hicho." Kimbunga hicho, kulingana na Desmond McKenzie, makamu  rais wa Baraza la Usimamizi wa Hatari za Maafa la Jamaica, kiliharibu hospitali nne na kuacha moja bila umeme, na kulazimisha mamlaka kuwahamisha wagonjwa 75. Zaidi ya watu nusu milioni walibaki bila umeme kufikia 28 Oktoba jioni. Kimbunga hicho tayari kimelaumiwa kwa vifo vya watu saba huko Kisiwani Caribbean, wakiwemo watatu huko Jamaica, watatu huko Haiti, na mmoja katika Jamhuri ya Dominika, ambapo mtu mwingine bado hajapatikana.

 

29 Oktoba 2025, 18:26