Papa Leo XIV alikutana na Waziri Mkuu wa Jumuiya ya Madola ya Dominica
Vatican News
Papa Leo XIV amekutana Septemba 12, katika Jumba la Kitume mjini Vatican na Waziri Mkuu wa Jumuiya ya Madola ya Dominica, Bwana Roosevelt Skerrit. Baada ya Mkutano huo, Bwana Skerrit alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican , akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican
"Wakati wa majadiliano mazuri katika Sekretarieti ya Vatican" taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican ilisema, "kuridhika kulioneshwa kwa uhusiano mzuri kati ya Vatican na Dominica. Kisha majadiliano yalilenga juu ya mchango muhimu ambao Kanisa hutoa kwa nchi, hasa katika nyanja za ustawi na elimu." "Wakati wa mazungumzo," taarifa hiyo inaendelea, "majadiliano yaligusa masuala kadhaa ya sasa ya kijamii na kisiasa katika kanda na nchi, kama vile changamoto za kijamii na matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa, na kufanya upya dhamira ya pamoja ya kukuza ushirikiano wa pamoja kwa manufaa ya watu wa Dominica."
