Tafuta

2025.09.10 Udienza Generale 2025.09.10 Udienza Generale  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:tuwaombee watoto ulimwenguni kote walioathiriwa na vita!

Wakati wa kutoa salamu kwa waamini wanaozungumza kiplanda na Kiarabu mara baada ya Katekesi Papa leo XIV alitoa wito kwa ajili ya amani.Awali ya yote kwa ajili ya watoto wanaoteseka kwa sababu ya migogoro duniani kote,hasa katika Ukraine na Gaza.Pili kwa mahujaji kutoka Nchi Takatifu,iliyoharibiwa na vurugu.Papa ametoa mwaliko wa kugeuza kilio cha uchungu kuwa sala inayoelekezwa kwa Mwenyezi Mungu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatano tarehe 10 Septemba 2025, mara baada ya kuhitimisha Katekesi yake, wakati wa salamu mbali mbali kwa mamie legu ya wanahija wengi waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro huku wakishikilia miavuli kutokana na mvua, alitoa wito wake. Akiwasalimia wanaozungumza lugha ya kipolanda alisema kuwa: “Leo inasherehekea Siku ya Kitaifa ya Waathirika wa Vita vya Kipoland, ambayo ni kumbukumbu ya mateso yao na mchango wao katika ujenzi mpya wa Poland baada ya Vita vya Pili vya Kidunia. Kumbukeni katika sala zenu na katika mipango yenu ya kibinadamu pia watoto wa Ukraine, Gaza, na maeneo mengine ya ulimwengu yaliyoathiriwa na vita. Ninawakabidhi ninyi na watoto wanaoteseka leo kwa ulinzi wa Maria, Malkia wa Amani, na nanawabariki kutoka moyoni mwangu.”

Waamini kutoka Ulimwenguni kote katika Katekesi ya Papa
Waamini kutoka Ulimwenguni kote katika Katekesi ya Papa   (@Vatican Media)

Papa akielekeza salamu kwa waamini wanaozungumza Kiarabu, hasa wale kutoka Nchi Takatifu alisema “Ninawaalika kugeuza kilio chenu wakati wa majaribu na dhiki kuwa sala ya ujasiri, kwa sababu Mungu huwasikiliza watoto wake na kujibu kwa wakati anaoona kuwa bora kwetu. Bwana awabariki nyote na kuwalinda daima na mabaya yote!” Kwa upande wa wanaozungumza lugha ya kiitaliano, Papa alisema “hasa kwa waamini wa majimbo yafuatayo: Ivrea, pamoja na Askofu Daniele Salera; Chioggia, pamoja na Askofu Giampaolo Dianin; Teano-Calvi, Alife-Caiazzo, na Sessa Aurunca, pamoja na Askofu Giacomo Cirulli; Nicosia, pamoja na Askofu Giuseppe Schillaci; Belluno-Feltre, pamoja na Askofu Renato Marangoni; Trapani, akiwa na Askofu Pietro Maria Fragnelli.” Papa aliwashukur kwa uwepo wao na “kuwaalika kuitikia kwa ukarimu neema ya Kristo Mwokozi, anayefanya upya mioyo, familia, na jamii.”

Papa katika katekesi
Papa katika katekesi   (@Vatican Media)

Alitoa salamu kwa parokia za Mtakatifu: Alessio huko Roma, Mtakatifu Maria Mpalizwa huko Grumo Appula, Mtakatifu Antonio wa Padova huko Castellamare di Stabia; na waamini wa Palmi, Bergamo, na Bonde la Berike. Pia aliwasalimu washiriki katika Kongamano la Chama cha Sheria za Kanuni za Kiitaliano, Shirika la Ndugu wa Yesu Mwenye Huruma katika kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwao, na na washiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa kuhusu Microbiot ya Utumbo. Hatimaye, mawazo yake yaligeukia vijana, wagonjwa, na wanandoa wapya:  “Ninawahakikishia kila sala yangu: kwa ajili yenu ninyi vijana, ninamwomba Bwana zawadi ya imani yenye kukomaa zaidi; na  kwa ninyi mlio wagonjwa, imani yenye nguvu zaidi; na kwenu wanandoa wapya, imani yenye kina zaidi. Baraka yangu kwa wote!”

Wito wa Papa kwa wanaoathirika na vita
10 Septemba 2025, 11:53