Tafuta

Mkutano huko Taasisi ya Kipapa ya Regina Apostolorum, Roma kuanzia 10-12 Septemba 2025. Mkutano huko Taasisi ya Kipapa ya Regina Apostolorum, Roma kuanzia 10-12 Septemba 2025. 

Papa Leo XIV:Katika Dhiki,unaweza kusikia ujumbe wa Tumaini la Uumbaji!

Katika ujumbe uliotiwa saini na Kardinali Parolin,Katibu Mkuu wa Vatican,Papa Leo XIV alibariki shughuli za Mkutano wa XII wa Sayansi na Dini wa Amerika ya Kusini, unaoendelea katika Taasisi ya Kipapa ya Regina Apostolorum hadi 12 Septemba kuwa:Lugha za Uumbaji:Sayansi,Falsafa na Utambuzi wa Kitaalimunu wa Kitabu cha Asili kama Njia ya Matumaini.Papa akimnukuu Mtakatifu Agostino,kuwa anatuhimiza kutafuta njia zinazomruhusu mwanadamu kuvuka yale yote yanayoweza kupimika."

Vatican News

Mtakatifu Agostino ndiye msukumo nyuma ya mwongozo ambao Baba Mtakatifu Leo XIV, katika ujumbe uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin,  Katibu Mkuu wa Vatican, alitoa kwa washiriki katika fursa ya  Mkutano wa XII wa Sayansi na Dini wa Amerika Kusini. Mada ya toleo hili ni: "Lugha za Uumbaji." Mafundisho ya kisayansi, kifalsafa na kitaalimungu ya "Kitabu cha Asili" kama njia ya matumaini. Huu ni mpango unaendelea katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Regina Apostolorum,  Roma kuanzia Septemba 10, hadi tarehe 12, 2025.

Katika Ujumbe uliolekezwa kwa Padre José Enrique Oyarzún, L. C., Mkuu wa Chuo hicho cha Kipapa, Baba Mtakatifu Leo anawalekeza wote na  na waandaaji na washiriki wote huku  akiwaalika washiriki “kutafuta njia zinazoruhusu ubinadamu kwenda zaidi ya yote yanayoweza kupimwa, kutafakari Kipimo kisicho na kipimo, kwenda zaidi ya yote yanayoweza kuhesabiwa; kutafakari Namba isiyo na idadi, kwenda zaidi ya yote ambayo inaweza kuwa dhambi, kutafakari Uzito usio na uzito." (Mtakatifu Agostino De Genesis, IV, 3, 8).

Kwa njia hiyo, Papa anathibitisha kuwa “hata bila kusema neno moja, kazi ya Mungu itatangaza utukufu wa Muumba wake, na wanadamu wataweza kusikia ujumbe wake wa tumaini, si tu katika fahari ya siku angavu za kuwepo kwake, bali pia katika usiku wa dhiki na dhiki ambazo ni tabia ya hali ya mwanadamu” (rej. Zab 19:1-4). Kwa matashi hayo, Baba Mtakatifu, huku akiwaalika wote “kwa  Jina la utamu wa Maria, Nyota ya Asubuhi, anamwomba Bwana aidumishe kazi yao  kwa neema yake na kwa upendo amewapa  Baraka ya Kitume mlinayoomba.”

11 Septemba 2025, 16:00