Papa atuma rambirambi zake kwa waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Afghanistan,kuna vifo zaidi ya 800.
Vatican News.
Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu tarehe 1 Septemba 2025 ametuma telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, kufuatia na waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Afghanistan. Katika telegramu hiyo, Papa anahuzunika sana kutoka na kupotea kwa maisha ya watu kwa sababu ya tetemeko katika sehemu ya mashariki ya Afghanistani, na kwa hiyo anatoa sala zake kwa ajili ya roho za marehemu, kwa waliojeruhiwa na wale ambao hadi sasa hawajapatikana.
Baba Mtakatifu "kwa kuwakabidhi watu wote walikumbwa na mkasa huo kwa mpaji Mwenyezi, anaonesha mshikamano wa kina kwa namna ya pekee kwa wale wote wanaoomboleza kwa sababu ya kupoteza wapendwa wao, kwa watoa msaada na kwa mamlaka ya raia ambao wanaendelea na shughuli za kuwaokoa watu. Katika kipindi hiki kigumu cha taifa, Baba Mtakatifu anaombea watu wa Afghanistani baraka ya Mungu ya faraja na nguvu."
Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba idadi ya muda kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mashariki mwa Afghanistan tarehe 31 Agosti usiku inafikia zaidi ya 2,800 waliojeruhiwa na zaidi ya 800 waliokufa, lakini uharibifu ulikuwa mkubwa sana kwamba idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka zaidi. Mikoa ya mashariki ya Kunar na Nangarhar iliathiriwa,na karibu elfu tatu kujeruhiwa, lakini juhudi za misaada zinadhoofishwa na ukosefu wa rasilimali na fedha. Kundi la Taliban limetoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kuomba usaidizi.
