Tafuta

Marekani ya Mlilia Charlie Kirk katika mkesha wa kumuombea. Marekani ya Mlilia Charlie Kirk katika mkesha wa kumuombea. 

Papa Leo XIV amwombea Charlie Kirk na familia yake

Msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican,Matteo Bruni,alithibitisha kwamba wakati wa mazungumzo ya Jumamosi iliyopita Septemba 13 na Balozi mpya wa Marekani anayewakilisha nchi yake katika Kiti Kitakatifu,kuwa Papa Leo XIV alitoa hakikisho la maombi yake kwa mwanaharakati wa Marekani aliyeuawa Septemba 10 nchini Marekani na kwa ajili ya familia yake.

Vatican News.

"Papa alithibitisha kwamba anamuombea Charlie Kirk," mwanaharakati wa kisiasa aliyeuawa tarehe 10 Septemba 2025, na "mkewe na watoto wake," wakati wa Mkutano wa Jumamosi tarehe 13 Septemba 2025 na Balozi mpya wa Marekani anayewakilisha nchi yake katika Kiti Kitakatifu, Bwana Brian Burch, wakati wa kuwasilisha Barua zake za Utambulisho.

Msemaji mkuu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya  Vatican, Dk, Matteo Bruni, alitoa kauli hiyo akiwajibu waandishi wa habari kadhaa. Kwa upande wa Dk. Bruni alisema “Papa, alionesha wasiwasi wake kuhusu ghasia za kisiasa na alizungumzia haja ya kujiepusha na maneno na unyonyaji unaosababisha ubaguzi na si mazungumzo."

16 Septemba 2025, 18:16