Tafuta

Duchess of Kent funeral Duchess of Kent funeral  (PA Wire/PA Images)

Papa atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Malkia Katharine wa Kent,Uingereza

Baba Mtakatifu Leo XIV amekumbuka urithi wa wema wa Kikristo'wa marehemu Malkia wa Kent katika "salamu za rambirambi kufuatia kifo huku akikumbuka urithi wake wa wema wa Kikristo na kukabidhi roho yake tukufu kwa huruma ya Baba yetu wa Mbinguni.Katharine Worsley,alijiunga na Familia ya Kifalme alipoolewa na Mfalme Edward wa Kent,binamu wa marehemu Malkia Elizabeth.Wafalme hawa lakini waligeukia Ukatoliki kunako 1994.Misa imefanyikia katika Kanisa Kuu la Westminster.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika salamu za rambirambi za Baba Mtakatifu Leo XIV kwa Mfalme Charles, ameelezea ukaribu wake na Familia ya Kifalme kwa kupoteza Malkia wa kifalme wa Kent huko Uingereza. Katika telegramu iliyotumwa tarehe 16 Septemba 2025 katika Jumba la Kifalme huko Buckingham, Baba Mtakatifu alisema alivyo huzunishwa na kifo cha Mtukufu Mfalme wa Kent.  "Ninatuma salamu za rambirambi kutoka moyoni, pamoja na uhakikisho wa ukaribu wangu wa sala, wewe Mfalme, washiriki wa Familia ya Kifalme, na hasa kwa mumewe, Malkia wa Kent, na watoto wake na wajukuu wakati huu wa huzuni," Papa Leo XIV  aliandika.

Misa ya Mazishi ya Malkia wa Kent
Misa ya Mazishi ya Malkia wa Kent   (PA Wire/PA Images)

Malkia Mkatoliki: Misa katika Kanisa Kuu Katolikimla Westminster

Katika rambi rambi hiyo Papa Leo XIV  alikabidhi roho ya marehemu huyo kwa Mungu na mbaye Mkatoliki, na Misa yake ya mazishi ilifanyika siku ya Jumanne katika Kanisa Kuu la Westminster, Uingereza na kuadhimishwa na Kardinali Vincent Nichols, Askofu Mkuu wa Westminster. Papa aliandika: "Kwa kuikabidhi roho yake tukufu kwa rehema za Baba yetu wa Mbinguni ninawahakikishia urahisi na wale wote wanaotoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa urithi wa wema wa Kikristo wa malkia huyo, unaoonekana katika miaka yake mingi ya kujitolea kwa majukumu rasmi, ufadhili wa misaada, na huduma ya kujitolea kwa watu walio katika mazingira magumu katika jamii." Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV  aliandika kuwa "kwa "wote wanaoomboleza kwa  kifo chake kwa tumaini la hakika la Ufufuko, ninatoa kwa hiari baraka zangu za kitume kama ahadi ya faraja na amani katika Bwana Mfufuka."

Misa ya Mazishi ya Malkia wa Kent
Misa ya Mazishi ya Malkia wa Kent   (ANSA)

Katharine, Mke wa Mfalme Edward

Katharine Worsley, alijiunga na Familia ya Kifalme alipoolewa na Mfalme Edward, Mfalme wa Kent, binamu wa marehemu Malkia Elizabeth. Wafalme hawa lakini waligeukia Ukatoliki kunako  1994, na kuwa washiriki wa kwanza wakuu kutoka Familia ya Kifalme ya Uingereza kufanya hivyo waziwazi tangu karne ya 18. Misa ya Mazishi  yake katika Kanisa Kuu la Westminster iliashiria mazishi ya kwanza ya kifalme kufanyika katika Kanisa Kuu la Kikatoliki huko Uingereza na Wales.

16 Septemba 2025, 18:30