Tafuta

2019.01.11 Cupola di San Pietro, piazza san Pietro , esterno basilica San Pietro

Papa anahimiza ushirikishwaji wa walemavu mjini Vatican

Katika maandishi yaliyochapishwa leo Jumamosi Septemba 13 yaliyotiwa saini na Kardinali Parolin,Papa Leo XIV anaidhinisha maazimio ya Baraza la ULSA kuhusu upokeaji wa watu wenye ulemavu katika Jumuiya ya kazi ya Kiti Kitakatifu "katika roho ya ukaribisho"na,inapobidi,"kwa kupitishwa kwa hatua zinazofaa na maalum,kutokana na kwamba hali ya ulemavu haizuii kufaa kwa kazi"katika miimili Vatican.

Vatican News.

Papa Leo XIV, katika mkutano wake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican mnamo tarehe 4 Agosti 2025, aliidhinisha kwa Maandishi juu ya maazimio ya Baraza la ULSA kuhusu kujumuishwa kwa watu wenye ulemavu katika jumuiya ya kazi ya Kiti Kitakatifu. Kwa hiyo kuanzia sasa na kuendelea,"uajiri wa watu wenye ulemavu unahamasishwa kwa moyo wa kukaribisha na, inapobidi, kwa kupitishwa kwa hatua zinazofaa na maalum, ikizingatiwa kwamba ulemavu hauzuii kufaa kwa kazi" katika vitengo vyote vya Vatican, iwe chini ya Kiti Kitakatifu au Gavana. Hii imethibitishwa na kifungu kipya cha 2 kilichoongezwa kwenye "Kanuni za Kulinda Hadhi ya  Mtu na Haki Zake za Msingi kwa Kuzingatiwa Katika Ukaguzi wa Afya Kabla ya Kuajiri Wafanyakazi Wakati wa Mahusiano ya Ajira" (kilichoandikwa mnamo tarehe 8 Novemba 2011).

Marekebisho ya kifungu cha Kanuni za Jumla za Curia Romana

Kuanzishwa kwa kanuni hii kwa hivyo kunarekebisha Kifungu cha 14 cha Kanuni za Jumla za Curia Romana, kuhusu uajiri na uteuzi wa wafanyakazi: neno "hali iliyothibitishwa ipasavyo ya afya njema" inabadilishwa na neno "kufaa kwa kisaikolojia katika majukumu ya kutekelezwa, kuthibitishwa na Kurugenzi ya Afya na Usafi wa Mji wa Vatican."  Mabadiliko haya ambayo yanaanza kutumika mara moja, yanahitaji tawala za Vatican kuendeleza uajiri wa watu wenye ulemavu.

Kuhusu ulinzi na haki za wafanyakazi,Vatican.

Sheria hizo mpya zinafuata zile zilizoidhinishwa na Papa katika Maandishi yaliyochapishwa kunako Agosti 11, ambayo ilipanua ulinzi na haki za wafanyakazi wa Vatican kwa kuanzisha, pamoja na mambo mengine, siku tatu za likizo ya malipo kwa mwezi kwa wazazi wa watoto wenye ulemavu na siku tano za likizo ya malipo kwa wafanyakazi wa Vatican baada ya kuzaliwa kwa mtoto. Katika muktadha huo pia, Papa Leo XIV alikuwa ameidhinisha maazimio ya Baraza la ULSA,ambacho ni chombo kilichoundwa na wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya Kiti Kitakatifu na Wa Gavana wa Mji wa Vatican na wafanyakazi wao husika.

Papa na ushirikishwaji wa walemavu mjini Vatican
13 Septemba 2025, 13:52