Tafuta

Papa akutana na Rais wa Tume kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto. Papa akutana na Rais wa Tume kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto.  (ANSA)

Papa akutana na Rais wa Tume ya Kulinda Watoto:dhamira ya kupambana na nyanyaso iendelee

Kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani,Askofu Mkuu Thibault Verny alikutana na Papa Leo XIV na ambaye aliwasilisha kwake Ripoti ya Pili ya Mwaka kuhusu Sera na Taratibu za Ulinzi katika Kanisa.Tume ilisisitiza dhamira yake ya kuendeleza utume uliokabidhiwa kwake na Papa Francisko na "kuanzisha utamaduni wa kuzuia katika Kanisa lote."

Vatican News

Mkutano rasmi wa kwanza umefanyika asubuhi ya Ijumaa  tarehe 12 Septemba 2025 kati ya Baba Mtakatifu Leo XIV na Askofu Mkuu Thibault Verny, Askofu Mkuu wa Chambéry na Rais wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto aliyeteuliwa tarehe 15 Julai 15 kuongoza Taasisi hiyo.

Ripoti ya Pili ya Sera na Taratibu za Ulinzi Iliyowasilishwa

Katika taarifa ya Tume ya Kipapa inaeleza kuwa wahusika walimuomba  Askofu Mkuu Verny binafsi kutoa shukrani zake kwa Baba Mtakatifu kwa amana aliyopewa kupitia uteuzi wake na kuwasilisha Ripoti ya Pili ya Mwaka ya Sera na Taratibu za Ulinzi katika Kanisa. Ripoti hii, iliyoanzishwa kwa dhamira ya Baba Mtakatifu Francisko mwaka 2022, inalenga kutathmini na kukuza uwezo wa ulinzi wa Makanisa mahalia na taasisi za kitawa, ikitoa mapendekezo ya vitendo kwa kuzingatia mang’amuzi madhubuti yaliyopatikana na Kanisa katika mazingira mbalimbali. Ripoti ya kwanza iliwasilishwa  tarehe 29 Oktoba 2024.

"Hapana" kwa aina zote za unyanyasaji

Katika mkutano huo, taarifa hiyo inaeleza zaidi kwamba, Askofu mkuu Verny alisisitiza tena dhamira ya Tume ya kuendeleza utume uliokabidhiwa kwake na Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya Waraka wake wa kitume wa Praedicate Evangelium, katika kuendeleza sera za ulinzi, katika kuandaa Ripoti ya Mwaka, na kusaidia Makanisa mahalia kwa njia ya (Memorare Initiative) yaani Mpango wa kumbukumbu. "Kwa unyenyekevu na matumaini, Tume," rais alisema, "inaendelea na utume tuliokabidhiwa, ikiendeleza maono ya Baba Mtakatifu ya kuanzisha utamaduni wa kuzuia katika Kanisa lote ambao hauvumilii aina yoyote ya unyanyasaji: sio ya nguvu au mamlaka, au ya dhamiri au kiroho, au unyanyasaji wa kijinsia."

Papa akutana na Rais wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto
12 Septemba 2025, 16:07