Papa akutana na Mwana Mfalme na Wazir Mkuu wa Ufalme wa Bahrein
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatatu tarehe 29 Septemba 2025 alikutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican na Mwana Mfalme na Waziri Mkuu wa Ufalme wa Bahrein, Salman bin Hamad Al Khalifa, ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, akisindikizana na Monsinyo Mirosław Stanisław Wachowski.
“Wakati wa majadiliano ya kina,kuridhika kulioneshwa kwa uhusiano mzuri baina ya nchi mbili, na makubaliano yalifikiwa juu ya hamu ya kuimarisha zaidi. Kisha majadiliano yalilenga sera ya Ufalme wa Bahrain ya kukuza mazungumzo ya kidini na kuishi pamoja kwa amani kati ya dini tofauti katika Ufalme, kwa kujitolea kwa amani kati ya mataifa." Hayo yalithibitishwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican.
