Tafuta

Kanisa Kuu la Leopoli. Kanisa Kuu la Leopoli.  ( Mariusz Krawiec SSP)

Leo XIV:Ukraine idumu na matumaini hai kila siku

Papa ametoa mwaliko wa kuomba zawadi ya amani kwa nchi ya Ulaya iliyogubikwa na vita katika barua aliyoituma kwa Kardinali Sepe,ambaye atamwakilisha Baba Mtakatifu katika maadhimisho ya miaka 650 tangu kuundwa kwa Jimbo kuu la Halić huko Lviv tarehe 6 Septemba.

Vatican News

Hata maneno ya Kilatini yanayoonekana kuwa rasmi na yasiyoweza kueleweka mara moja yanapatana na moyo wa mshikamano wa Papa Leo XIV kwa Ukraine. Katika barua kwa Kardinali Crescenzio Sepe, aliyeteuliwa mwezi Julai iliyopita kama mjumbe wake maalum kwa ajili ya  sherehe ambazo mji wa Lviv utafanya mnamo tarehe 6  Septemba 2025 kwa  kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 650 ya kuundwa kwa Jimbo kuu la  Halić,  baada ya hapo likaitwa  Lviv kwa Kilatini na sehemu ya Kanisa Katoliki la Roma la ibada ya Kilatini, Baba Mtakatifu  Leo XIV alisisitiza katika kifungu kimoja shauku yake kwamba Askofu Mkuu Mstaafu wa Napoli awasilishe “upendo wa Papa na ukaribukwa waamini wote wa Kikristo na watu wenye mapenzi mema watakaoshiriki katika tukio hilo.”

Sadaka Makini katika Familia na katika Jamii

"Katika wakati huu mgumu sana ambao Ukraine inapitia," Papa Leo XIV anawaalika waamini wa Ukraine kulinda "amri ya upendo kwa uangalifu mkubwa zaidi, katika familia na katika hali za umma," na "kukuza tumaini dogo la Kikristo katika maisha ya kila siku," wakiomba "kwa bidii kutoka kwa Mungu zawadi ya amani." Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican ilibainisha kwamba ujumbe utakaoongozwa na Kardinali Sepe utashiriki katika sherehe hizo zitakazofanyika katika Kanisa Kuu la Mama yetu wa Kupalizwa mbinguni huko Lviv. Wajumbe hao watajumuisha Monsinyo Andrzej Legowicz, katibu binafsi wa Askofu Mkuu wa Lviv ya  kilatini, na Padre Roman Broda, profesa katika Seminari ya Jimbo Kuu na mkuu wa Ofisi ya Liturujia ya jimbo hilo hilo la Ukraine.

01 Septemba 2025, 19:53