China,Askofu mpya aliyewekwa wakfu wa Jimbo Jipya lililoundwa na Papa leo XIV
Vatican News
Kwa kuwekwa wakfu Septemba 10, 2025 kwa Askofu Joseph Wang Zhengui mwenye umri wa miaka 62 anakuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo la Zhangjiakou, kwa mchakato ulioanza miezi miwili iliyopita na Papa Leo XIV na kukamilika. Tarehe 8 Julai 2025, kwa nia ya kukuza uchungaji wa kundi la Bwana na kuhudhuria kwa ufanisi zaidi manufaa yake ya kiroho,” kama Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican inavyoripoti, Papa Leo XIV alivunja majimbo ya Xiwanzi na Xuanhua, na kuyaunganisha katika eneo moja la jimbo jipya, ambalo ni sehemu ya Mkoa wa Hebei na mpaka wa Beijing.
Na wakati huo huo, tarehe 8 Julai 2025, Papa Leo XIV alimteua Monsinyo Wang Zhengui kuwa Askofu wake kwanza wa Zhangjiakou, "baada ya kuidhinisha kugombea kwake," kwa mujibu wa taarifa rasmi, "ndani ya Makubaliano ya Muda kati ya Vatican na Jamhuri ya Watu wa China."
Askofu Mpya
Askofu mpya aliyesimikwa tarehe 10 Septemba 2025, alizaliwa mwaka 1962, na kuudhuria Seminari ya Mkoa wa Hebei kuanzia mwaka 1984 hadi 1988. Kwa miaka miwili iliyofuata, alimaliza mafunzo ya uchungaji katika Parokia ya Qujiazhuang. Mnamo tarehe 24 Mei 1990, akawa Padre wa Jimbo la Xianxian na akapewa parokia hiyo hiyo, ambapo aliteuliwa kuwa mchungaji mnamo 1991.Baadaye alihudumu katika Jimbo la Xuanhua.
Jimbo jipya
Kwa kuvunjwa kwa majimbo mawili ya Xuanhua na Xiwanzi, yaliyoanzishwa kunako tarehe 11 Aprili 1946 na Papa Pio XII, Jimbo jipya la Zhangjiakou lina jumla ya eneo la kilomita za mraba 36,357 na idadi ya watu 4,032,600, ambao takriban 85,000 ni Wakatoliki na mapadre ni 89. Mipaka ya kikanisa ya jimbo jipya, kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya Vatican inaarifu, itajumuisha maeneo yafuatayo: vitongoji vya Xuanhua, Qiaodong, Xiahuayuan, Chongli, Qiaoxi, na Wanquan; na wilaya za Chicheng, Huailai, Zhuolu, Weixian, Yangyuan, Huai'an, Shangyi, Zhangbei, Guyuan, na Kangbao. Kitongoji cha Yanqing kimeingizwa katika Jimbo kuu la Beijing; wakati mji wa Xilinguolemeng umeingizwa katika Jimbo la Jining.
