Tafuta

Papa Leo XIV:Popote tulipo tusipoteze fursa ya kupenda!

Matendo ya huruma ndiyo benki iliyo salama na yenye faida kubwa sana ambayo ndani yake tunaweza kukabidhi hazina ya uwepo wetu, kwa sababu pale, kama Injili inavyotufundisha, kwa “senti mbili” hata mjane maskini anakuwa mtu tajiri zaidi duniani.Ni katika tafakari ya Papa Leo XIV wakati wa sala ya Malaika wa Bwana,Dominika tarehe 10 Agosti 2025 akiwageukia waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Katika Injili ya leo, Yesu anatualika kutafakari juu ya namna ya kuwekeza hazina ya maisha yetu(Lk12,32-48). Anasema: “ Viuzeni vyote mlivyo navyo na kuwapa maskini (Lk12,33). Ndivyo Baba Mtakatifru Leo XIV alivyoanza tafakari yake, Dominika tarehe 10 Agosti 2025 akiwalekea waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, ikiwa ni Dominika ya 19 ya Mwaka C wa kawaida. Baba Mtakatifu Leo alisema: “anatushauri tusitunza kwa ajili yetu zawadi ambayo Bwana alitufanyia, bali kuziwekeza kwa ukarimu kwa wema wa wengine, hasa kwa ajili ya yule ambaye anahitaji zaidi msaada wetu.

Umati wa waamini na mahujaji katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Umati wa waamini na mahujaji katika Uwanja wa Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

“Si tu kuhusu kushirikisha vitu vya kimwili tulivyo navyo, bali kuhusu kuweka uwezo wetu, wakati wetu, upendo wetu, uwepo wetu, huruma yetu katika kuthubutu. Kwa ufupi, kila kitu ambacho kinamfanya kila mmoja wetu, kuwa katika mipango ya Mungu, kuwa na mali ya kipekee, isiyokadirika, mtaji wa maisha, mkupuo ambao ili kukua, unadai kukuzwa na kuwekezwa; vinginevyo, hunyauka na kupoteza thamani. Au unaishia kupotea, kwa huruma ya wale ambao, kama wezi, wanajinufaisha ili kuigeuza kuwa kitu cha matumizi.

Waamini katika sala ya Malaika wa Bwana
Waamini katika sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Zawadi ya Mungu ambayo sisi ni, haikufanyika kuisha namna hiyo. Inahitaji nafasi, uhuru, uhusiano ili kujikamilisha na kujieleza: inahitaji upendo, ambapo unabadilisha tu na kutukuza kila aina ya kitu cha maisha yetu kwa kufanya daima kufanana zaidi na Mungu. Baba Mtakatifu kwa njia hiyo alisema: “ si kwa bahati mbaya, Yesu anatamka maneno haya wakati alipokuwa akitembea kuelekea Yerusalemu, mahali ambapo juu ya Msalaba atataseka mwenyewe kwa ajili ya maisha yetu.” Matendo ya huruma ndiyo benki iliyo salama na yenye faida kubwa sana ambayo ndani yake tunaweza kukabidhi hazina ya uwepo wetu, kwa sababu pale, kama Injili inavyotufundisha, kwa “senti mbili” hata mjane maskini anakuwa mtu tajiri zaidi duniani (Mk 12,41-44).

Mtakatifu Agostino katika muktadha huo alisema: "Mtu angeridhika ikiwa kutoka kwa kilo ya shaba mtu angetengenezwa kwa fedha, au kutoka kwa paundi ya fedha moja ya dhahabu; lakini kutoka kwa kile ambacho mtu anatoa, mtu hupokea kitu tofauti kabisa, sio dhahabu au fedha, lakini uzima wa milele" (Sermo 390, 2). Na anaeleza kwa nini: “Kinachotolewa kitabadilishwa kwa sababu atoaye atabadilishwa.” Na ili kuelewa maana yake, tunaweza kufikiria mama anayeshikilia watoto wake karibu: je, yeye si mtu mzuri zaidi na tajiri zaidi duniani? Au wa wachumba wawili waliochumbiana, wanapokuwa pamoja: je, hawajisikii kama mfalme na malkia? Na tunaweza kutoa mifano mingine mingi.

Papa Leo XIV katika Sala ya Malaika wa Bwana
Papa Leo XIV katika Sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Kwa njia hiyo katika familia, katika Parokia, katika shule na sehemu za kazi, kila mahali popote tulipo, tusipoteze fursa yeyote ya kupenda. Huo ndiyo umakini ambao Yesu anatuomba: kuzoea kuwa makini, tayari, na wa huruma kuelekea wengine kama Yeye alivyo kwetu sisi katika kila dakika. Baba Mtakatifu Leo XIV kwa kuhitimisha alisema: “tumkabidhi Maria shauku hii, na jitihada hii: atusaidie Yeye, Nyota ya asubuhi, ya kuwa walinzi wa asubuhi katika ulimwengu uliogubikwa na migawanyiko mingi, wa huruma na wa amani, kama alivyotufundisha, Mtakatifu Yohane Paulo II (Mkesha kwa Siku ya XV ya Vijana Duniani WYD, 2000) na kama walivyotufundisha kwa njia nzuri vijana waliofika Roma kwa ajili ya Jibilei.

Tafakari ya Papa Leo XIV kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana
10 Agosti 2025, 13:05