Papa Leo XIV, Waoblate wa Mtatifu Franciska Romana:mwanga kwa kila zama wa upendo wa Kristo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alituma ujumbe kwa Watawa wa Oblate wa Mtakatifu Franciska Romana wa Tor de' Specchi, katika fursa ya Miaka 600 ya kujitoa kwa Mtakatifu huyo. Ilikuwa ni tarehe 15 Agosti 1425 katika Sherehe ya Kupalizwa mbinguni Bikira Maria, ambapo Mtakatifu Franciska Roma, mwanzilishi baada ya kuishi maisha kama mchumba na mama wa mfano pamoja na wenzake wa kwanza tisa, alijitoa sadaka akiwekwa wakfu kwa Mungu katika huduma ya unyenyekevu na ya kujitolea kwa wale walioteswa na umaskini wa kibinadamu na wa kiroho wa wakati wake. Papa alisema: “Katika karne hizi sita, familia yao ya zamani ya kitawa, iliyouishwa na Kanuni kubwa ya Baba mkuu wa utawa wa Magharibi Mtakatifu Benedikto, imekuwa shule ya upendo hai, kisima cha hali ya kiroho, na bora ya kujitolea kwa Kristo na Kanisa.
Jubilei muhimu sana kwa jimbo la Roma
Kwa hiyo, ukumbusho huu wa pekee, ni tukio la furaha kwa baba Mtakatifu Leo XIV kuungana nao katika sala, Mabinti wapendwa, ambao kila siku, wakielekeza macho yao kwake Yeye aliyetoa maisha yake kwa ajili ya wokovu wetu (rej. Yh 10:17-18), kwa upendo wanamkabidhi maisha yao na matamanio wanayoyathamini mioyoni mwao, ili ufalme wake wa nuru na amani uweze kujengwa. Papa Leo XIV kwa njia hiyo alitoa mawazo kwa jumuiya hiyo ya watawa na wote ambao, pamoja nao wanaadhimisha tukio hili la Jubilei, muhimu sana kwa Jimbo zima la Roma. Mtakatifu Franciska wa Roma, anayependwa sana na waamini, anaendelea kuwa ni mwanga unaowaangazia waamini wa kila zama, kuwasha moto wa upendo wa Kristo ndani ya watu wa leo hii.
Alijali mahitaji ya jamii
Papa Leo XIV alisisitza kuwa :“Jamii yetu inahitaji wanawake kama yeye: wenye shauku ya Injili na kama Mtangulizi wake anayeheshimiwa alivyoandika: "wakiwa wamechochewa na bidii ya Mungu, wanaotaka kumtumikia Aliye Juu Sana kwa roho ya unyenyekevu na, kadiri udhaifu wao unavyoruhusu, kuiga maisha ya kitume ili kujishindia wenyewe kwa ajili ya Kristo na kuishi katika jumuiya na mapendo..." (Papa Eugene IV, Hati ya kuanzishwa Monasteri ya Tor de’ Specchi), roho ambazo, kama Papa mwingine mkuu, Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, alivyosema: “kwa kutiwa moyo na kuimarishwa kwa neema, huku akijali sana mahitaji na mielekeo ya jamii ya leo, alikuwa na uwezo wa kufanya uchaguzi wa misimamo mikali ya kiinjili […] yenye sifa ya nidhamu kali, kujinyima kwa furaha, na kujitolea kwa ukarimu.” (Yohane Paulo II, Barua ya Januari 15, 1984).
Ari ya kumleta Kristo Ulimwenguni
Baba Mtakatifu kwa njia hiyo alibainisha kuwa kuna mambo mengi ya utakatifu wake. Tunaweza kukumbuka njia tatu. Ya kwanza ni ile ari ambayo kwayo alijitolea kumleta Kristo ulimwenguni na kufanya uwepo wake kuwa imara na wa kweli kwa njia ya ushuhuda wake wa imani na utakatifu; Ya pili ni utiifu wake kwa uongozi wa kimalaika, ambao uwepo wao aliukuza kwa uaminifu kwa sala na kutafakari Neno la Mungu, pamoja na kujitolea kwa watakatifu wake walinzi - Mtakatifu Paulo, Mtakatifu Maria Magdalene, Mtakatifu Benedikto, na Mtakatifu Francis de Sales - chini ya uongozi wa watu wa kiroho kama vile Mtakatifu Yohane Leonardi na Mtakatifu Philipo Ner waliomsindikiza katika safari yake.
Fadhila ya tatu ni kujitolea kwake kwa umoja wa Kanisa, ambao kwa ajili yake alijitoa kwa njia ya sala na matendo. Uwepo wao kama Monasteri "iliyo wazi" - kama Mama Mwanzilishi alivyotamani - katikati ya Jiji la Milele, taa ya historia na safari ya watu, inaendeleza haya yote. Kwa karne nyingi, waja wengi wa ibada ya Mtakatifu wamefika mahali hapa pa utukufu, matajiri wa sanaa na kiroho, ili kuteka amani ya ndani na kufurahia upendo wa Mungu. Hata leo hii, katika jamii iliyochanganyikiwa na yenye furaha, kuna hitaji kubwa la kijitoa kama hiki. Kwa hiyo Papa Leo XIV aliwatia moyo waammshe tena karama yao, wakitumaini msaada wa Roho Mtakatifu, ambaye, licha ya changamoto za wakati huu, atawaimarisha na kuwasaidia kuendeleza utume wao kwa manufaa ya Kanisa. Mtakatifu Franciska alikuwa na sala nzuri kwa Mama mpendwa: Tenuisti manum dexteram meam: in voluntate tua deduxisti me: et cum gloria assumpsisti me, yaani "Umeshika mkono wangu wa kuume kwa mkono wako, umeniongoza katika mapenzi yako na kunikaribisha katika utukufu."
Mpango wa unabii
Na kwa njia hiyo Papa Leo alisema, “Na iwe pia mpango na unabii wao, katika uaminifu na hamu ya kila wakati ya nchi ya milele. Amewahimiza watawa hao wajisikie kuwa na umoja na Kanisa linalowatazama kwa upendo wa pekee, hasa wakati huu wanapokabidhiwa ulezi wa Baba wa Ndugu yao Mtukufu, Kardinali Fortunato Frezza, aliyeitwa kuwasindikiza na kuwaunga mkono katika safari hii ili kwa pamoja wamtazamie siku zijazo kwa matumaini na unyenyekevu. Kwa matashi mema hayo Papa ya heri ya maadhimisho ya Jubilei, aaliwakabidhi kwa maombezi ya Bikira Maria Aliyepalizwa Mbinguni, ya Wakili Urbis na Watakatifu Walinzi, na kuwapa Baraka yake ya Kitume, ambayo kwa hiari yake aliwapatia wote wanaoungana nao katika kushukuru, akitumaini kwamna nao watamwombea.
