Tafuta

Huko Napoli kuyeyuka damu ya Mtakatifu Gennaro tukio la kila mwaka. Huko Napoli kuyeyuka damu ya Mtakatifu Gennaro tukio la kila mwaka.  (ANSA)

Papa Leo XIV kwa Juma la 75 la Kiliturujia Kitaifa:waamini wagundue imani katika makanisa

Papa Leo XIV alitoa matashi mema kwa washiriki wa Juma la 75 la Liturujia Kitaifa,huko Napoli,Italia kuanzia tarehe 25-28 Agosti 2025,”inaweza kuwatia moyo kutafakari na kufanyia kazi kanuni za kichungaji zinazofanya kazi ili waamini wagundue makanisa kama mahali pa ibada,mahali pakuadhimisha imani,wanakutana na Bwana aliyepo na anayetenda katika Sakramenti,anaishi na umoja kidugu.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV  tarehe 26 Agosti 2025 alituma ujumbe kwa washiriki wa Mkutano wa 75 wa Liturujia kitaifa nchini Italia ulioanza tangu tarehe 25 hadi 28 Agosti 2025, kwa kuuelekeza kwa Askofu Mkuu Claudio Maniago, wa jimbo Kuu Katoliki la Catanzaro-Squillace, na Rais wa Kituo cha Matendo ya Kiliturujia wa Baraza la Maaskofu, Italia, kwa ushirikino na Jimbo Kuu Katoliki la Napoli.

Kuibua upyaisho wa utambuzi wa tabia za kuinjilisha

Katika Ujumbe huo Papa Leo  anabaisha kuwa “tukio hilo linampatia fursa ya kuelezea shauku na kupongeza wale ambao katika Kanisa la Italia wanajikita kwa ajili ya kuhuisha Liturujia ya Watu wa Mungu, walioitwa katika shughuli tofauti na huduma za kutoa sifa kwa Bwana.”  Papa amewapa salamu “watoa mada na washiriki wote katika siku hizo za mafunzo,” huku akiwatakia heri ili  ziweze kusaidia ushiriki hai daima wa waamini katika matendo ya kiliturujia ya Kanisa, kwa kuibua upyaisho wa utambuzi wa tabia za kuinjilisha za maadhimisho matakatifu.”

Kanuni za kuchungaji

Baba Mtakatifu aidha anasema warsha hiyo “inaweza kuwatia moyo kutafakari na kufanyia kazi za kanuni za kichungaji zinazofanya kazi ili waamini wagundue makanisa kama mahali pa ibada, mahali pakuadhimisha imani, wanakutana na Bwana aliyepo na anayetenda kazi katika Sakramenti, anaishi na umoja kidugu.” Kwa kusindikizwa na matashi hayo na bidii Papa Leo anawakumbuka katika sala , na kuwatakia kila mema ya mafanikio ya kazi, na kwa utashi anawatumia Baraka ya Kitume.”

Papa kwa washiriki wa Juma la 75 la kiliturujia kitaifa
26 Agosti 2025, 16:32