Papa Leo XIV atazindua kituo cha Mafunzo ya Juu cha Laudato si’ huko Castel Gandolfo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mawasiliano ya Kituo cha Mafunzo ya Juu ya Laudato si’, inabainish kuwa tarehe 5 Septemba 2025, saa 10:00 jioni masaa ya Ulaya, itanyika hafla itakayoongozwa na Baba Mtakatifu Leo XIV ambapo atazindua rasmi Borgo Laudato si': mahali,ambapo kwa karne nyingi yamekuwa ni makazi ya Mapapa, ambayo sasa yamefunguliwa kwa umma na ambapo kanuni zilizomo katika Waraka wa Kitume wa Laudato si', mwaka huu zinaadhimisha miaka kumi tangu kuanza kwake. Eneo hilo ndani yake likiwa ni makazi ya Papa huko Castel Gandolfo, Borgo Laudato si' ni mpango uliozaliwa kutokana na Waraka wa Baba Mtakatifu Francisko, ambaye mwaka 2023 alikikabidhi Kituo cha Mafunzo ya Juu cha Laudato si' utume wa kujenga mahali ambapo utunzaji wa uumbaji na heshima kwa utu wa binadamu, hasa wale walio katika mazingira magumu zaidi, unaweza kulindwa na kuimarishwa kupitia dhamira ya pamoja yenye mizizi ya imani.
Mali hiyo ya hekta 55 ni pamoja na bustani za kihistoria, majumba, makaburi, na mabaki ya kiakiolojia, maeneo ya kilimo, na maeneo mapya yaliyotolewa kwa elimu na kilimo hai na cha kuzaliwa upya. Ni matokeo ya safari inayofungamana na hali ya kiroho, elimu na uendelevu, inayolenga kutoa nafasi wazi, inayoweza kufikiwa na jumuishi kwa ajili ya kujifunza, kutafakari, na kupata uhusiano makini na wenye heshima zaidi na uumbaji. Kwa njia hiyo alasiri hiyo, kabla ya kuongoza Liturujia ya Neno kwa Ibada ya Kubariki, Baba Mtakatifu Leo XIV, atafanya ziara ya kwenye Borgo, ili kutembelea maeneo yake muhimu na kukutana na wafanyakazi, washirika, familia zao, na watu wote ambao, katika nyadhifa mbalimbali, wanaleta maisha hai humo Borgo Laudato si', kama vile watawa, waelimishaji, wanafunzi, wananchi, washirika, na wafadhili. Wawakilishi wa Curia Romana, na taasisi pia watakuwepo kwenye sherehe, pamoja na wengi ambao wamechangia kuzaliwa kwa mpango huo. Kabla ya Baba Mtakatifu kubariki eneo hilo, Mwalimu Andrea Bocelli na mwanawe Matteo wataungana katika sala na kuimba wimbo pamoja.
