Papa,kwa Waldensian:kushirikiana kwa ajili ya utu,haki na amani ya binadamu
Vatican News
Kupitia Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, Baba Mtakatifu Leo XIV alituma salamu zake kwa Sinodi ya Waaldensian iliyofunguliwa tarehe 23 Agosti huko Torre Pellice (Turino) na itahitimishwa tarehe 27 Agosti 2025. Papa alionesha matumaini yake ya "ushirika kamili" kati ya Wakristo, mada ambayo ni muhimu sana kwa Papa Leo XIV, ambayo aliithibitisha katika kauli mbiu yake, "In Illo uno unum."
Wakristo washirikiane kwa ajili ya utu, haki, na amani ya kibinadamu
Kwa njia hiyo Papa leo alitoa "salamu za kidugu" kwa wale wanaoshiriki katika Sinodi ya Waaldensia-Methodisti. Aliwahakikishia "ukumbusho wake wa bidii katika sala ili Wakristo wote wasafiri kwa unyofu wa moyo kuelekea ushirika kamili, kushuhudia Yesu Kristo na Injili yake, wakishirikiana katika huduma kwa binadamu, hasa katika kutetea utu wa binadamu, katika kuendeleza haki na amani, na kutoa majibu ya pamoja kwa mateso yanayowapata wale walio waliowadhaifu zaidi.”
Mchungaji Ciaccio: Mungu anaita si kuwaelemea wengine bali kuwatumikia na kuwapenda
Sinodi hiyo kwa kuundwa na wawakilishi wa makanisa mahalia, idadi sawa ya wachungaji, na wale wanaohusika na sekta maalum za utendajitukio hilo la Wawaldensian hukutana kila mwaka katika Mabonde ya Wawaldensiani. Hufunguliwa kwa ibada ambayo wahudumu wa baadaye, baada ya kumaliza masomo yao na mitihani ya hadhara, wanajitolea kulitumikia Kanisa na wanawekwa wakfu kwa kuwekewa mikono na washiriki wote wa sinodi hiyoo. Kazi inafanywa kulingana na kielelezo cha majadiliano ya kusanyiko hilo, katika ujuzi kwamba kitendo cha Roho huongoza maamuzi yaliyoshirikishwa.
Tarehe 23 Agosti Mchungaji Peter Ciaccio alitoa mahubiri ya ufunguzi, huku akisisitiza "kazi ngumu ya makanisa yetu hasa: kusema juu ya Mungu, kuzungumza juu ya uhusiano wetu na Mungu na matokeo yake; kuzungumza juu ya ukweli kwamba Mungu alitupata, alituita, na sio kama uhalali wa kuwakandamiza wengine, lakini kama msingi wa kuwatumikia na kuwapenda wengine, kwa kuunga mkono na kutetea wasiobahatika, wale wa mwisho,”lifafanua
