Tafuta

Kardinali Estanislao Esteban Karlic,Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Paraná ameaga dunia. Kardinali Estanislao Esteban Karlic,Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Paraná ameaga dunia. 

Papa Leo XIV:Karlic,mchungaji mwaminifu katika upendo na Kanisa

Papa Leo XIV,katika telegramu yake ya rambirambi kwa sababu ya kifo cha Kardinali wa Argentina, Askofu Mkuu Mstaafu wa Paraná,alikumbuka maisha yake ya huduma kwa Mwenyezi Mungu na Kanisa,“kuleta mwanga wa Injili katika nyanja mbalimbali za maisha na utamaduni na ushirikiano wake katika kuandaa Katekesi ya Kanisa Katoliki.”

Vatican News

Papa Leo XIV alituma salamu za rambirambi kwa kuondokewa na Kardinali Estanislao Esteban Karlic, siku ya Ijumaa, tarehe 8 Agosti 2025, katika telegram aliyoituma kwa Askofu Mkuu Raúl Martín wa Paraná, Jumamosi tarehe 9 Agosti 2025. Kardinali Karlic alihudumu katika Jimbo hilo na katika lile la Córdoba kama Padre na askofu. Papa Leo alitaka kupanua ukaribu wake wa kiroho "kwa wale wote ambao ni sehemu ya jumuiya hiyo pendwa ya kikanisa,"  na alikumbuka kwa heshima "mchungaji huyu mkarimu na mwadilifu."

Nuru ya Injili Inayoletwa kwenye Uhai na Utamaduni

Papa Leo XIV aliandika: "Kwa miaka mingi na kwa uaminifu mkubwa, alijitolea maisha yake kwa huduma ya Mungu na Kanisa, kuleta mwanga wa Injili katika maeneo mbalimbali ya maisha na utamaduni." Kardinali huyo aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99, aliongoza Baraza la Maaskofu wa Argentina kwa vipindi viwili mfululizo, huku akimkaribisha Mtakatifu Yohane Paulo II katika Hija yake ya kitume katika nchi ya Amerika Kusini.                                                                                                                                                    

Sadaka ya Ukarimu katika Huduma kwa Kanisa la Ulimwengu

Papa Leo XIV  alifafanua zaidi juu ya wasifu wake: "Miongoni mwa kazi zake nyingi za kichungaji na mipango yake katika ngazi mahalia, kitaifa na bara, alijitolea kwa ukarimu kwa huduma ya Kanisa la Ulimwengu wote, akishirikiana katika kuandaa Katekisimu ya Kanisa Katoliki." Shukrani kwa Mungu "kwa ajili ya maisha yake ya imani na upendo wake mkuu kwa Kanisa" vinaambatana na sala kwa ajili ya pumziko la milele la roho yake, "ili Bwana Yesu ampe taji la utukufu lisilofifia." Na kwa kumkabidhi roho ya Kardinali aliyekwenda mbinguni, pamoja na baraka ya kitume, ni kwa maombezi ya Mama yetu wa Rozari, "kama ishara ya tumaini la Kikristo kwa Bwana Mfufuka."

Papa Leo atuma rambirambi kwa kifo cha Kardinali Karlic
10 Agosti 2025, 10:17