Tafuta

2022.12.29 Maria Mtakatifu sana Mama wa Mungu. 2022.12.29 Maria Mtakatifu sana Mama wa Mungu. 

Gazeti la “San Pietro,”Papa Leo XIV amjibu msomaji

Katika Makala ya“Piazza San Pietro,Baba Mtakatifu Leo XIV amemjibu mwanamke mmoja na mama kuhusu namna ya kushinda vishawishi.“Ikiwa msimamo wako ni Maria,utaweza kukabiliana na kila ukosefu wa uhakika(…).Kushirikishana mipango ya upendo wa kikirsto ni mguzo kwa ajili ya kuendelea kiroho na kushirikishana neema na mapenzi ya Mungu.”

Vatican News

Mwezi Agosti ni kipindi cha polepole na kujigunduwa kile kinachotuunganisha. Ni katika tafakari hii ambayo inafungua upya makala ya kwanza ya Gazeti la “Piazza San Pietro,” linalohaririwa na Padre Enzo Fortunato.  Lakini pia ni kipindi cha kusikiliza, kama inavyoonesha barua ambayo Laura mama na mwanamke alivyoandika kupitia makala ya kila mwezi ya kipapa akikabidhi furaha na ugumu wa imani yake.

Yeye anajiuliza jinsi gani ya kukabiliana na matatizo na Papa Leo XI anamshauri kuyaita majina na kushirikisha uzoefu wake binafsi. “Nina mme ambaye ananipenda sana… na ni mama wa watoto 3 wazuri wa kike ambao ninatafuta namna ya kuwamwilisha kwa sala na nNno la Injili kila siku. (…) Niko napitia wakati mgumu ambao imani yangu ina nguvu kuliko hapo awali… labda, ni kwa sababu hiyo ninahisi kwa nguvu vishawishi vya kupata ushindi wa juu. Je ina maana kwamba imani yangi siyo thabiti?

Jibu la Papa Leo XIV linasisitiza jinsi ambavyo “shuku ya imani na ukweli ya upendo wako ni baraka kwako na kwa familia yako (…) Ikiwa msimamo wako ni Maria, utaweza kukabiliana na kila ukosefu wa uhakika(…). Kushirikishana mipango ya upendo wa kikristo ni msingi kwa ajili ya kuendelea kiroho na kushirikishana neema na mapenzi ya Mungu.”

Makala ya kila mwezi zaidi , ya kuwa Mkutano muhimu wa Udugu, ambao jijini Roma, utafanyika kuanzia tarehe 12 na 13 Septemba, katika fursa ya mkutano huo, ukaribu na kushirikishana kwa njia ya mazungumzo ya pamoja; na kutafakari kwa kina juu ya amani katika Historia ya Mapapa 12 kuanzia na Papa Leo XIII hadi Papa leo XIV, na juu ya uhusiano wa kina na udugu.

Katika makala yenye kichawa: “Kupumzika udugu na amani,” Padre Fortunato, anasimulia maana ya kina ya mwezi wa kiangazi: mji mtupu. Mdundo wa maisha ambayo yanakuwa polepole, na hata Baba Mtakatifu anakwenda kwenye makao ya Castel Gandolf kwa kipindi cha ukimya na kutafakari.

Jambo la mwisho la makala ya “Piazza san Pietro”(yaani Uwanja wa Mtakatifu Petro), linamulika jumuiya ya kwanza iliyokuwa imemzunguka Yesu ambayo inageuka ‘kwa namna hiyo  sura ya Kanisa ambalo linaalikwa kujenga madaraja na siyo kuta, kama anavyotukumbusha Baba Mtakatifu kuwa: “ Kabla ya kuwa waamini sisi tunaalikwa kuwa binadamu.”

Uwanja wa Mtakatifu Petro,Papa anajibu swali
19 Agosti 2025, 15:00