Papa anaweza kukaa muda mrefu bila oksijeni na amefanya mikutano na wakuu wa Curia
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko anaendelea na matibabu yake akiwa katika makao yake ya nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican na vipimo kwa ujumla vya kimatibabu viko thabiti na maboresho ya taratibu katika mifumo yake ya mwili na kupumua. Haya ndiyo masasisho yaliyotolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican, kuhusu hali ya Papa Francisko, tarehe 11 Aprili 2025 kuhusu afya yake, ambaye amekuwa akitibiwa na kufanya mapumziko mjini Vatican, tangu tarehe 23 Machi 2025 baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali ya Gemelli Roma. Kwa njia hiyo taatifa ilibainisha kuwa “Papa Francisko ana uwezo wa kukaa vile vile bila oksijeni kwa muda mrefu. Anatumia mtiririko wa juu na hasa zaidi kwa madhumuni ya matibabu.” Aliweza kufanya Mkutano wa takriban dakika ishirini na Mfalme wa Uingereza Charles na Mke wake Malkia Camilla mnamo tarehe 9 Aprili 2025 uliofanyika bila msaada wa oksijeni. Vipimo vya damu pia vilikuwa vyema na uboreshaji pia ulionekana na uboreshaji wa mapafu.
Mikutano na washirika wake
Papa Francisko pia anaendelea na shughuli yake ya kazi kwa kutazama hati na akikutana na washirika wake. Ofisi ya Vyombo vya Habari iliripoti kwamba katika siku za hivi karibuni alikutana na Katibu Msaidizi wa Vatican Askofu Mkuu, Edgar Peña Parra, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, na Monsinyo Luciano Russo, katibu Mwakilishi wa Kipapa. Mbali nao, pia kuna baadhi ya wakuu wa Mabaraza ya Kipapa na wakuu wa Curia Romana.
Matembezi katika Basilika ya Mtakatifu Petro
Hali ya Papa inaendelea kuwa nzuri, kama ilivyoonekana kwenye matembezi yake ya tarehe 10 Aprili katika Basilika ya Mtakatifu Petro. Katika wakati huu wa kustaajabisha, Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican ilieleza kwamba “Papa alikuwa akitembea na akachagua kupanua matembezi yake ili kwenda kusali katika Basilika.”
Ibada za Juma Takatifu
Kwa sasa hakuna utabiri au dalili yoyote kuhusu ibada za Juma Takatifu, wala uwepo wa Papa wakati wa maadhimisho ambayo pia yatategemea hali ya hewa. Ofisi ya Vyombo vya Habari ilithibitisha, hata hivyo, kwamba, kwa ujumbe wa Papa Francisko, atawakilishwa na Kardinali Leonardo Sandri, Makamu wa Baraza la Makardinali, ambaye ataadhimisha Misa ya Dominika ya Matawi tarehe 13 Aprili 2025.