Papa awashangaza waamini ndani ya Kanisa la Mtakatifu Petro akisali katika kaburi la Papa Pius X
Na Salvatore Cernuzio – Vatican.
Ilikuwa karibu saa 7:00 za mchana katika Basilika ya Mtakatifu Petro wakati baadhi ya wanawake walisikika wakipaza sauti kwenye vinjia: "Papa yuko hapa! Papa yuko hapa!" Baada ya mshangao wa Dominika iliyopita, (Aprili 6), pale ambapo waamini elfu 20 walikuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, kwa ajili ya Jubilei ya Wagonjwa na ya Ulimwengu wa Kiafya kwa ghafla walipomwona Papa akiwasili kwenye kiti cha magurudumu, tukio hilo limerudiwa tena mchana wa Alhamisi tarehe 10 Aprili 2025, wakati Papa Francisko alipendelea kutoka kidogo katika makazi yake ya Mtakatifu Marta, ambapo anaendelea na matibabu yake na kuvuka Mlango wa Maombi ili kwenda kwenye Basilika. Ilikuwa ni chini ya dakika kumi za sala ya kimya mbele ya kaburi la Papa Pius X, Papa ambaye amekuwa akisema alikuwa karibu sana na Papa huyo na ambaye pia alikwenda kusali Dominika iliyopita.
Mamia wamsalimia Papa
Hata hivyo, dakika chache zilitosha kuwashtua mamia ya watu waliokuwa wamekuja kuhiji katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro walikusanyika kumsalimu Papa. Miongoni mwao walikuwa pia baadhi ya wasanii warejeshaji ambao walikuwa na shughuli nyingi wakati huo nyuma ya pazia kwa kazi za ndani zilizofanywa katika miezi ya hivi karibuni na Kiwanda cha Mtakatifu Petro (Fabbrica di San Pietro,) ambao walipeana mikono na Jorge Mario Bergoglio, watoto kadhaa aliowabariki na makundi yote ya mahujaji walikuwa jijini Roma kwa ajili ya Jubilei. "Hisia nyingi sana, maono yangu yalififia kutokana na machozi na sikuweza hata kupiga picha," Monsinyo Valerio Di Palma,Mwanasheria wa Kanisa la Mtakatifu Petro alielezea vyombo vya habari vya Vatican.Alikuwa amerudi kwenye sakrestia, karibu 6.50 mchana kwa hiyo, dakika kumi baadaye alitoka nje akivutiwa na msukosuko huo na kuona kiti cha magurudumu na Papa, kikisukumwa na Massimiliano Strappetti, msaidizi wa afya ya kibinafsi. Na Pande zote kulikuwa na walinzi wakijaribu kudumisha utulivu ndani ya Kanisa Kuu.
Baraka na salamu
“Papa alipitia Mlango wa Sala na kisha akaenda kwenye Madhabahu ya Kiti kitakatifu na hatimaye kwenye kaburi la Mtakatifu Pius X ili kusali. Mwishoni alisalimia watu wachache, kwa kadiri alivyoweza,” kwa maelezo ya Monsinyo Di Palma.” Hakuna maneno kutoka kwa Papa Francisko, bali ishara tu. Ishara za ukaribu na upendo kwa wale aliowakuta mbele yake, wengine hata walijipanga ili kupata muda wa ukaribu na Askofu wa Roma katika wakati huu ambao, kutokana na kutoonekana hadharani kumekuwa nadra sana: "Kila mtu alikimbia akijua kuwa Papa amefika ghafla." Kadahalika "Papa Francisko alijionesha kwa watu akiwa na blanketi ndogo miguuni ili kumkinga na baridi na mirija za pua za oksijeni: "Hii ilituchochea, kumuona hivi 'akiwa na nguo za kiraia', rahisi. Kila mtu alikuwa akilia, hata usalama. Watoto wengine walikwenda karibu na Papa, mwanamke alibarikiwa kwa machozi. Kwa sababu ni ishara kwamba amepona, ndiyo, anateseka lakini yuko karibu. Kilichonigusa ni macho yake: makubwa, angavu. Mtazamo huu wa kupenya na makini. Hakusema chochote: alisalimia na kubariki. Nilimwambia, Baba Mtakatifu, tunakusubiri mapema urudi hapa tena. Alitabasamu," alihitimisha.