Kard.Krajewski:Papa aliniita kuunga mkono misheni nchini Ukraine!
Vatican News
Kichekesho cha Papa ambacho kinaonesha kwa mara nyingine tena jinsi ambavyo katika kipindi cha kupona hapotezi ucheshi wake mzuri. Haya ndiyo aliyoyasema Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo ambaye yuko nchini Ukraine kwa siku kadhaa, ambako alitembelea kwa mara ya kumi tangu kuanza kwa vita, alisema katika ujumbe kwa vyombo vya habari vya Vatican. Mwenyekiti huyo alipokea simu kutoka kwa Papa Francisko mwishoni mwa asubuhi yenye shughuli nyingi huko Zaporizhzhia, ambapo alisambaza chakula cha msaada, alipeleka dawa na gari la wagonjwa kati ya zilizotolewa na Papa.
Simu ya kutia moyo
Ilikuwa ni simu ya kushtukiza kutoka kwa Baba Mtakatifu - Kardinali alisema - alitaka kujua jinsi misheni nchini Ukraine inavyoendelea. Aliniambia nisalimie kila mtu na akatoa baraka zake. Nilimwambia kwamba kulikuwa na baridi kali na yeye, ambaye alikuwa katika hali nzuri, aliongeza: ‘Unajua jinsi ya kuwapasha moto.’” Kardinali Krajewski alitabasamu alipokuwa anasimulia hitoria hiyo na kuongeza kwamba simu hiyo ilikuwa na matokeo ya mara moja, ikichangamsha mioyo ya kila mtu.
joto ya Ukraine
Kardinali kisha alizingatia ahadi zake, akikumbuka msururu wa watu maskini ambao walikuwa wakisubiri tangu saa 11 alfajiri kwa ajili ya usambazaji wa chakula ambao hata hivyo ulianza vizuri mida ya saa 4 alfajiri baadaye, kuonyesha matatizo makubwa yaliyopatikana kwa wakazi wa eneo hilo. "Ulikuwa mkutano wa maana sana - aliongeza - machoni pa watu hao niliona tumaini, upendo na licha ya baridi walitushukuru kwa uchangamfu, wanatumaini kuwa maafa haya yote yataisha hivi karibuni".
Hii ilifuatiwa na mkutano na maafisa wa afya wa eneo la Zaporizhzhia ambao walichukua ambulensi. “Tuliondoa vibao vya Vatican, wakastaajabishwa na jinsi zilivyokuwa na vifaa vya kutosha na wakaondoka kwenda mahali penye uhitaji mkubwa zaidi.” Kardinali Krajewski basi alitaka kusisitiza mchango mkubwa uliopokelewa kutoka kwa miundo mbalimbali katika ukusanyaji wa dawa zinazopelekwa Ukraine. "Dawa zilichukuliwa hasa huko Napopo ambapo pamoja na utamaduni wa kuacha pesa kwenye migahawa ya kahawa, kuna ile ya dawa iliyosimamishwa katika maduka ya dawa takriban mia moja. Mkusanyiko wenye thamani ya takriban euro laki mbili. Walituambia hapa kwamba dawa ni msaada mkubwa. Dawa pia zilitolewa bila malipo na Famasia ya Vatican na Hospitali ya Gemelli, ambayo ilitoa dawa za huduma ya kwanza.” Kutoka kwa ishara ndogo ilizaliwa wimbi kubwa la ukarimu na mshikamano kwa watu wa Kiukreni wanaoteswa ambao kwa miaka mitatu wameishi katika mateso makubwa kutokana na vita.