Papa wa Papa:Warom bado wanakabiliwa na ubaguzi na hali chungu!
Vatican News
Historia ambayo mara nyingi huoneshwa na kutokuelewana, kukataliwa na kutengwa ni ile ya watu Warom nchini Hispania, ambao kwa miaka 600 ya uwepo wao itaadhimishwa mwaka 2025. Haya ni maadhimisho muhimu ambayo Papa Francisko alitaka kuadhimisha kwa ujumbe wake ambao anasisitiza “ukaribu wa Mungu kwa watu hawa hata katika nyakati ngumu zaidi." Mungu ambaye "ni msafiri katika historia na ubinadamu na akawa katika kuhamahama na watu warom,” ndivyo anaandika Papa katika maandishi yaliyotiwa saini tarehe 9 Desemba 2024 huko Mtakatifu Yohane Laterano, lakini yaliyotangazwa kwa umma Dominika tarehe 12 Januari 2025.
Njia mpya kuelekea ujumuishaji
Katika maandishi yake, kwa Kihispania, Papa anaakisi juhudi iliyofanywa katika miongo ya hivi karibuni na watu warom kwa Kanisa na jamii ya Hispania kwa ujumla, katika kuchukua njia mpya kuelekea ujumuishaji wa heshima na utambulisho wao. Ni njia ambayo imezaa matunda mengi, lakini ambayo lazima tuendelee kuifanya kazi, kwa sababu bado kuna ubaguzi wa kushinda na hali zenye uchungu kukabiliana nazo, anahimiza Papa. Miongoni mwao Papa anabainisha kuna: "Familia ambazo ziko katika shida na hazijui jinsi ya kusaidia watoto wao katika shida, watu masikini ambao wana shida ya kusoma na kuandika, vijana ambao hawawezi kupata kazi nzuri, wanawake wanaobaguliwa katika familia zao na katika jamii."
Kanisa linalofungua milango yake
Kwa Warom hao, Papa Francisko anasisitiza katika ujumbe usiosahaulika wa Mtakatifu Paulo VI, uliotamkwa huko Pomezia mnamo mwaka 1965 mbele ya maelfu ya Warom kutoka ulimwenguni kote kuwa: "Ninyi ni moyo wa Kanisa. Hao ni binti wapendwa na wana wa Mungu…”. Katika Kanisa hilo, Papa alisisitiza, kuwa: “watu wengi wamejitolea kwa uwajibikaji na upendo kwa maendeleo kamili ya watu Warom. Ni Kanisa ambalo linataka kuendelea kuifungua milango yake kwa upana, ili sisi sote tujisikie tuko nyumbani humo.” Papa anaandika tena, huku akihakikisha kwamba: “Mungu haaachi kuzidisha ukarimu na kwa hiyo atafanya mapenzi yake na wakati wa kuzaa matunda na kwamba watu hawa wamejitolea kwa uchungaji na Wajasiri.
Thamani za kutoa
Kuhusiana na hii, Papa Francisko alikumbuka Sinodi ya hivi karibuni ambayo ilizindua tena umuhimu wa kutembea pamoja. Kwa njia hiyo kutembea pamoja ndiyo mwaliko anaoutoa kwa Warom wa Hispania kwamba “watembee pamoja na maaskofu, wakuu wa wajumbe wa kichungaji na sekretarieti, parokia, washirika, vyama na taasisi za kijimbo. "Twende pamoja, kwa sababu katika Kanisa nguvu ya Injili itasafisha na kupanua maadili na utamaduni wake," alihimiza Papa, huku akikumbusha kwamba watu wa kuhamahama wana mengi ya kutoa kwa Kanisa na jamii. "Shukrani kwa wazee na hali ya familia, utunzaji wa kazi ya uumbaji, hali ya mahujaji kuelekea nchi ya mbinguni, uwezo wa kudumisha furaha na kusherehekea hata kama kuna mawingu meusi angani, mtazamo wa upeo, maana ya kazi ambayo mara nyingi haieleweki na kama njia ya kuishi na sio kukusanya.” Maadili ambayo siyo ya kiinjili tu, bali pia ya kinabii, kinyume na ya kiutamaduni ya wakati huu,” Papa aliandika.
Kueneza furaha ya kuishi
Hivyo mwaliko wa kueneza furaha ya kuishi imani, matumaini na upendo wa Kikristo, hasa kwa vijana ambao wana shida ya kumpata Mungu ndani na nje ya Kanisa Katoliki. Kwa maneno yao, kujitolea na udugu, kuwa mahujaji wa matumaini kwa watu wengi ambao wamepoteza furaha ya kuishi," pia akihimiza kuweka milango ya Jumuiya wazi kwa wale ambao hawasherehekei tena imani katika Kanisa Katoliki, daima kuwapa urafiki na mazungumzo ya kawaida ya wale kama sisi ambao wameitwa kuishi katika udugu zaidi ya tofauti zetu."
Mfano wa wenyeheri Emilia Fernández Rodríguez na Ceferino Giménez Malla
Mwishoni mwa ujumbe ilikuwa ni marejeo ya Wenyeheri Emilia Fernández Rodríguez na Ceferino Giménez Malla, Warom, walimu wa imani na maisha kwa Warom, wanyenyekevu na wajasiri watu ambao walifungua kwa ujasiri udogo wao katika ukuu wa Mungu na wanatukumbusha umuhimu wa sala, kukutana na Mungu, chanzo cha furaha, udugu, matumaini na mapendo. Kwa njia hiyo Papa alihitimisha kwa kutoa baadhi ya maneno kutoka katika wimbo wa watu hao uitwa: Opre Roma isi vaxt yaani Njooni, Warom! Sasa ni wakati. Kwa hiyo aliandika Papa Francisko: "Ni wakati wa kuendelea na safari, kujitolea kwa yaliyo bora zaidi yenu, kwa kusambaza huruma ya Mungu, na kwamba ‘Devlesa roma’ yaani Mungu awe pamoja na Warom."