Tafuta

Gari moja kwa makusudi liligonga umati wa watu wanaosherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya huko New Orleans nchini Marekani na kuua makumi ya watu. Gari moja kwa makusudi liligonga umati wa watu wanaosherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya huko New Orleans nchini Marekani na kuua makumi ya watu. 

Uchungu wa Papa Francisko kwa shambulio la New Orleans

Katika barua iliyotiwa saini na Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican kwa kuilekeza kwa Askofu Mkuu Aymond,Papa anatoa rambirambi zake kwa waliofariki na kujeruhiwa katika shambulio la mkesha wa mwaka mpya.Raia wa Marekani mwenye itikadi kali,aliendesha gari kwenye umati wa watu na kuanza kufyatua risasi mara aliposhuka kwenye gari,kabla ya kuuawa na polisi:watu 15 walikufa na karibu 30 kujeruhiwa.

Vatican News

Alhamisi tarehe 2 Januari 2025, Baba Mtakatifu Francisko  ameelezea "huzuni kubwa" kwa shambulio lililotokea usiku wa kuamkia mwaka mpya huko New Orleans nchini Marekani, ambapo Lori moja  la kubeba mizigo lilivamia umati wa watu, na kuua watu kumi na tano na kujeruhi wengine takriban thelathini. Katika barua iliyotiwa saini na Katib wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, kwa Askofu Mkuu wa New Orleans,  Gregory Aymond, Papa anatoa rambirambi zake kwa kupoteza maisha ya watu na majeruhi. Akihakikishia “ukaribu wake wa kiroho” kwa jumuiya nzima, Papa Francisko “anazikabidhi roho za wale waliokufa kwa rehema ya upendo wa Mwenyezi Mungu na kuwaombea majeruhi wapate uponyaji na wale wanaoomboleza kwa ajili ya wapendwa wao.” Papa pia ametuma baraka zake "kama ishara ya amani na nguvu katika Bwana.”

Shambulio 31 Desemba

Shambulio hilo lililotokea tarehe 31 Desemba mwendo wa saa 9.15 katika "Vieux Carre"(mtaa wa kifaransa wenye shughuli nyingi zaidi), lilitekelezwa na raia wa Marekani, mfanyakazi wa Deloitte na mwanajeshi wa zamani nchini Afghanistan, mahali ambapo alikuwa amebadili kuwa mwislamu akiwa na  umri mdogo hadi  kufika katika aina ya itikadi za ugaidi. Shamsud-Din Jabbar, jina la mwanamume huyo, mwenye umri wa miaka 42, mzaliwa wa Texas, aliendesha gari hilo kwa mwendo wa kasi katika umati wa watu waliokuwa wakisherehekea mwisho wa mwaka. Kisha akashuka kwenye gari na kuanza kufyatua risasi, kabla ya kuuawa na polisi. Watu 15 walibaki chini wameuawa na karibu thelathini walijeruhiwa. Kulingana na polisi wa eneo hilo, mshambuliaji alidhamiria kusababisha mauaji. Maneno ya rambirambi yamefika  kutoka kila mahali.

Papa atoa rambi rambi huko New Orleans
02 January 2025, 13:57