Tafuta

2025.01.03  Papa na Wajumbe wa Muungano wa Kifalme wa Watakatifu Yohane Mbatizaji na Mwinjili wa Jeshi la  Malta, wa Catanzaro,Italia.  2025.01.03 Papa na Wajumbe wa Muungano wa Kifalme wa Watakatifu Yohane Mbatizaji na Mwinjili wa Jeshi la Malta, wa Catanzaro,Italia.   (Vatican Media)

Papa:Katika mwaka wa Jubilei tukuze sala ya kibinafsi,Jumuiya na kujitolea sana!

Kuabudu,kutumikia na kutembea pamoja ndiyo maneno matatu aliyotafakari Baba Mtakatifu katika hotuba kwa Wajumbe wa Udugu wa Kifalme wa Watakatifu Yohane Mbatizaji na Mwinjili wa Jeshi la Malta, huko Catanzaro nchini Italia alipokutana nao mjini Vatican tarehe 3 Januari 2025.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana  mjini Vatican, tarehe 3 Januari 2025 na Wajumbe wa Muungano wa Kifalme wa Watakatifu Yohane Mbatizaji na Mwinjili wa Jeshi la  Malta, wa Catanzaro, Italia. Katika hotuba yake Papa amefurahi kukutana nao “mwanzoni mwa mwaka huu mpya, ambapo tunasherehekea Jubilei kama wakati wa upatanisho na matumaini.” Papa aliongeza kusema kuwa tumetoka kusherehekea Siku kuu ya Maria, Mama Mtakatifu wa Mungu: ambaye ndiye mlinzi wa udugu wao, anayemkumbuka kwa jina la Odigitria, "yeye anayeonesha njia, yaani, Yesu, ambaye ni Njia, Ukweli na Uzima (Yh14:6). “Ni Yeye, ndiye anayemwonesha Yesu, daima! Kamwe hajioneshi mwenyewe: Yesu! Hodegetria..." Maria amemshika Mwokozi aliyezaliwa kwa ajili yetu mikononi mwake. Hapa kuna tukio la upendo ambalo unashuhudia kwa kuabudu Ekaristi, kuwahudumia wengine na kutembea katika historia ya jiji lao.

Papa na Ujumbe kutoka Canzaro
Papa na Ujumbe kutoka Canzaro

Kwa hiyo Baba Mtakatifu alipenda kutafakari kwa ufupi nao juu ya vitenzi hivi vitatu: kuabudu, tumikia, na kutembea.  Kwanza kabisa, kuabudu. Udugu wao unakusanyika mbele ya Sakramenti Takatifu. Hasa katika Mwaka huu Mtakatifu, Papa amewaaalika  kukuza ibada ya sala, sala ya kibinafsi na ya jumuiya,na  kwa kujitolea sana. Na  hiyo waache iwe nguvu, ambayo itafanya upya ushirika wao wa zamani kila wakati. Hamasa  kiukweli, huhifadhi udugu: udugu wa Bwana Yesu, ambaye hutulisha kwa maisha yake na kututegemeza kwa Roho wake, kutoka katika karama zote, karama, matunda ya wema ambayo hufanya Kanisa kuzaa matunda na furaha .

Hatua ya pili ni kutumikia. Papa Francisko amesisitiza kwamba “wanapowahudumia maskini, kila wanapowatembelea wagonjwa, wakiwa pamoja na wanaoteseka wanamtumikia Bwana (Mt 25:40). Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya kuabudu na huduma, ambayo hatupaswi kamwe kusahau. Kristo alikuja ulimwenguni kutumikia (Mk 10:45): nao pia, kama matawi yaliyounganishwa na Mzabibu, waendeleza upendo wake wanapokaa karibu na wadogo na wahitaji kwa huruma na upole. Papa  kama kawaida yake kuhusiana na hili kwamba: “Msisahau hili: huruma na upole,  yaani ukaribu na wadogo na maskini.” Kwa sababu kuna Vitenzi vitatu vinavyoonesha jinsi Mungu alivyo pamoja nasi katika ukaribu, huruma na Upole. Mungu yuko karibu nasi; Mungu ni mwenye huruma;  na Mungu ni mpole.” Ndipo ushuhuda wao wa ujitoaji kwa Mungu na wakfu kwa ndugu zao utakuwa nyeti kwa kila mtu njiani.

Ujumbe kutoka Catanzaro
Ujumbe kutoka Catanzaro

Na kitenzi cha tatu ni kutembea na ambapo Papa amesema kuwa  kinatukumbusha kwamba Yesu, ni Njia, anatuita tumfuate kwa ustahimilivu, tukishika taa ya  imani, ikiwashwa wakati wa hija hii ya duniani. Kwa njia, hiyo Papa ametoa shukrani za kipekee kwao kama Askofu wa Roma kwamba udugu wao, kiukweli, hutoa mshumaa wa Pasaka katika Basilika ya Lateran kila mwaka, pamoja na sadaka ya kuchangia upendo wa Papa. Asante sana!” Baba Mtakatifu Francisko amewasihi waendelea kuwa na matumaini katika njia ya ukarimu, ambayo kwayo Bwana ataambatana nao daima. Amewabariki kwa moyo wote wao na familia zao. Na tafadhali wasisahau kumwombea.

Papa na Ujumbe kutoka Catanzaro
03 January 2025, 15:22