Papa,Dominika ya Neno la Mungu:Tukaribishe unabii wa kale wa moyo wa Kristo!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ameongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 26 januari 2025. Ni katika muktadha wa Maadhimisho ya Dominika ya VI ya Neno la Mungu iliyoanzishwa na Papa mwenyewe kunako 2019. Katika fursa hiyo imetolewa pia Huduma ya Usomaji wa Neno la Mungu kwa waamini 40 kutoka mataifa mbali mbali duniani. Vile vile misa hiyo ilikuwa ni kufunga Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano, iliyoanza tangu tarehe 24 Januari kwa ufunguzi wa misa.
Baba Mtatifu akianza alisema, Injili tuliyoisikia inatangaza utimilifu wa unabii unaofurika katika Roho Mtakatifu. Na yule anayeitimiza ni Yeye ajaye “kwa nguvu za Roho”( Lk 4:14 ): ni Yesu, Mwokozi. Neno la Mungu liko hai: linatembea nasi kwa karne nyingi, na kupitia nguvu za Roho Mtakatifu linafanya kazi katika historia. Bwana, kiukweli, sikuzote ni mwaminifu kwa ahadi yake, ambayo huiweka kwa sababu ya upendo kwa wanadamu. Hivi ndivyo alisema Yesu katika sinagogi la Nazareti: "Leo Maandiko haya yametimia masikioni mwenu"(Lk 4:21). Baba Mtakatifu alisema kuwa ni bahati iliyoje yenye furaha! Katika Dominika ya Neno la Mungu, bado tukiwa mwanzoni mwa Jubilei, ukurasa huu wa Injili ya Luka unatangazwa, ambamo Yesu anajidhihirisha kuwa Masiha “aliyewekwa wakfu kwa kupakwa mafuta” na kutumwa “ kutangaza mwaka “kwa neema ya Bwana.”
Yesu ndiye Neno lililo Hai, ambaye ndani yake Maandiko yote yanatimizwa kikamilifu. Na sisi, katika Liturujia Takatifu Papa aliongeza kuwa ni watu wa wakati wake: sisi pia, tukiwa na mshangao, tunafungua mioyo na akili zetu ili kumsikiliza, kwa sababu "ndiye anayesema wakati Maandiko Matakatifu yanasomwa katika Kanisa" (Katiba Sacrosanctum Concilium, 7). Baba Mtakatifu alikumbusha alivyotaja neno moja "mshangao." Tunaposikia Injili, maneno ya Mungu, si suala la kuyasikiliza tu, kuyaelewa, hapana. Lazima zifikie moyo, na kuzalisha kile nilichosema: "ajabu."Neno la Mungu daima hutushangaza, hutufanya upya kila mara, huingia mioyoni mwetu na kutupyaisha daima.” Na katika mtazamo huo wa imani ya furaha tunaalikwa kuukaribisha unabii wa kale unaotoka katika Moyo wa Kristo, ukijikita katika matendo matano yanayodhihirisha utume wa Masiha: utume wa pekee na wa ulimwengu wote; wa kipekee, kwa sababu Yeye, anaweza kulitimiza; kwa sababu anataka kuhusisha kila mtu.
Kwanza kabisa, “Anatumwa kuwahubiria maskini habari njema”. Hapa kuna “injili”, habari njema ambayo Yesu anatangaza: Ufalme wa Mungu umekaribia! Na Mungu anapotawala, mwanadamu huokolewa. Bwana anakuja kuwatembelea watu wake, akiwatunza wanyenyekevu na wenye huzuni. Injili hii ni neno la huruma, ambalo linatuita kwa hisani, kusamehe madeni ya jirani zetu na kujitolea kwa ukarimu wa kijamii. Papa aliongeza kusisitiza kuwa “Tusisahau kwamba Bwana yu karibu, mwenye huruma na mwenye upole. Ukaribu, huruma na upole ndiyo mtindo wa Mungu kama huo.
Tendo la pili la Kristo ni “kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao.” Mwovu siku zake zinahesabika, kwa sababu wakati ujao ni wa Mungu, kwa nguvu za Roho, Yesu anatukomboa kutoka katika kila hatia na kuufungua moyo wetu, kuufungua kutoka katika kila mnyororo wa ndani, akileta msamaha wa Baba duniani. Injili hii ni neno la huruma, linalotuita sisi kuwa mashuhuda wa dhati wa amani, mshikamano na upatanisho.
Tendo la tatu, ambalo Yesu anatimiza unabii huo, ni kufanya “vipofu waone.” Masiha hufungua macho ya mioyo yetu, mara nyingi hushangazwa na mvuto wa nguvu na ubatili: magonjwa ya roho, ambayo yanatuzuia kuutambua uwepo wa Mungu na ambayo huwafanya wanyonge na wanaoteseka wasionekane. Injili hii ni neno la nuru, linalotuita kwenye ukweli, kwa ushuhuda wa imani na kushikamana kwa maisha.
Hatua ya nne ni “kuwaweka huru walioonewa.” Hakuna utumwa unaoweza kupinga kazi ya Masiha, ambaye hutufanya tuwe ndugu katika jina lake. Magereza ya mateso na kifo yanafunguliwa kwa nguvu ya upendo ya Mungu; kwa sababu Injili hii ni neno la uhuru, linalotuita kwenye uwongofu wa moyo, kwenye uaminifu wa mawazo na ustahimilivu katika majaribu.
Hatimaye, hatua ya tano: Yesu anatumwa "kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa" (Lk 4, 19). Huu ni wakati mpya, ambao hautumii maisha, lakini huifanya upya. Ni Jubilei, kama ile tuliyoianza, tukijitayarisha kwa matumaini kwa kukutana kwa uhakika na Mkombozi. Injili ni neno la furaha, ambalo linatuita kukaribisha, kwa ushirika na kusafiri, kama mahujaji, kuelekea Ufalme wa Mungu. Papa Francisko alibainisha kuwa kupitia matendo hayo matano, Yesu tayari ametimiza unabii wa Isaya. Kwa kuleta ukombozi wetu, anatutangazia kwamba Mungu anakaribia umaskini wetu, anatukomboa kutoka katika uovu, hututia nuru macho yetu, anavunja nira ya ukandamizaji na anatuingiza katika furaha ya wakati na historia ambayo anajifanya mwenyewe, kutembea nasi na kutuongoza kwenye uzima wa milele. Wokovu anaotupatia bado haujatimizwa kikamilifu, tunajua; na bado kuna vita, ukosefu wa haki, maumivu, lakini kifo hakitakuwa na neno la mwisho. Kiukweli Injili ni neno lililo hai na la hakika, ambalo halikatishi tamaa, yaani Injili haikatishi tamaa.
Papa alisema kuwa katika Dominika hii iliyowekwa maalum kwa ajili ya Neno la Mungu, tumshukuru Baba kwa kuwa ametuelekezea Neno lake, lililomfanya mtu kwa wokovu wa ulimwengu. Hili ndilo tukio ambalo Maandiko yote yanazungumza juu yake, ambayo yana watunzi wao wa kweli yaani watu na Roho Mtakatifu (taz.Dei Verbum, 11). Biblia nzima inamkumbuka Kristo na kazi yake na Roho hufanya uwepo katika maisha yetu na katika historia. Tunaposoma Maandiko, tunapoomba na kuyasoma, hatupokei habari kuhusu Mungu tu, bali tunamkaribisha Roho ambaye hutukumbusha yote ambayo Yesu alisema na kutenda (Taz Yh 14:26).
Hivyo mioyo yetu, ikiwa imewashwa na imani, inangojea kwa matumaini ujio wa Mungu. Papa alisema kuwa lazima tuwe na mazoea zaidi ya kusoma Maandiko. Katika hilo alipendekeza tena kwamba kila mtu awe na Injili ndogo, mfukoni ya Agano Jipya, na kubeba katika mfuko na wakati wa mchana kuisoma. Na kwa hiyo hata wakati wa mchana kuna mawasiliano na Bwana. Injili inatosha. Papa amesihi kuitikia kwa ari kwa tangazo la furaha la Kristo! Bwana, kiukweli, hakusema nasi kama wasikilizaji kimya, bali kama mashuhuda, akituita kuinjilisha nyakati zote na kila mahali.
Waliopokea huduma ya Usomaji
Papa akiwageukia ndugu 40 kutoka sehemu nyingi za ulimwengu wamekuja roma kupokea huduma ya usomaji. Amewashukuru akisema “Asante! Tunawashukuru na kuwaombea. Sote tunawaombea.” Sote na tujitolee kuwahubiria maskini habari njema, kuwatangazia wafungwa uhuru wao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru walioonewa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Kwa hiyo Papa aliomba kwamba wote kuwa tunaweza kubadilisha ulimwengu kulingana na mapenzi ya Mungu, ambayo aliiumba na kuikomboa kwa upendo.