Papa atoa wito wa kuongoka wale wanaotengeneza viwanda vya silaha
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya Katekesi yake, Jumatano tarehe 15 Januari 2025, Baba Mtakatifu Francisko alianza kutoa salamu mbali mbali kwa mahujaji kutoka pande za dunia. Na wakati wa kuzungumza na wale wa kiitaliano, Papa alisema kuwa "Juzi, akiinaminisha tarehe 13 Januari. maporomoko ya ardhi yalisomba nyumba kadhaa katika eneo la uchimbaji madini katika jimbo la Kachin nchini Myanmar na kusababisha hasara, kukosa watu na uharibifu mkubwa. Niko karibu na watu walioathiriwa na janga hili na ninawaombea waliopoteza maisha na familia zao. Uungwaji mkono na mshikamano wa jumuiya ya kimataifa usikose kwa kaka na dada zetu walio katika shida.”
Salamu kwa mahujaji
Papa Francisko aliendelea kuwakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano. Kwa namna ya pekee, aliwasalimu waamini wa jimbo la Acqui Terme, Jumuiya ya Magnificat Dominum na parokia ya Lungavilla. Vile vile aliwakaribisha moyo mkunjufu wanafunzi na walimu wa shule ya kibinafsi ya Kikatoliki "Highlands Institute" ya Roma. Na kwamba wasikike kwa kelele zao.
Tusisahau Ukraine inayoteswa na nchi nyingine
“Na tusisahau Ukraine inayoteswa, Myanmar, Palestina, Israel, na nchi nyingi zinazopigana. Tuombe amani. Vita daima ni kushindwa. Na pia, tafadhali, tuombe uongofu wa mioyo ya watengenezaji wa silaha kwa sababu ya bidhaa zao husaidia kuua,” Alisema Papa Francisko
Kazi ya sarakasi ni kazi ya kibinadamu
Baba Mtakatifu akiendelea alisema kuwa “Mawazo yangu- lakini kwanza ningependa kuwashukuru kikundi cha sarakasi ambao sasa watarudi kupigwa picha ya mwisho. Kazi ya sarakasi ni kazi ya kibinadamu, ni kazi ya kisanii, kazi inayohitaji juhudi nyingi. Wakirudi tutawapigia makofi makubwa-, hatimaye mawazo yangu yawaendee vijana, wagonjwa, wazee na wenye ndoa wapya," alisema Papa. Kwa njia hiyo aliwahimiza “kila mtu kushuhudia kwa ukarimu imani katika Kristo, ambaye huangazia njia ya uzima.” Na alitoa Baraka yake kwa kwa wote!