Papa alipata mshituko kwenye mkono wa kulia kwa sababu ya kuanguka
Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imeripoti kuwa Papa Francisko alianguka kwenye makazi yake ya Mtakatifu Marta mjini Vatican asubuhi tarehe 16 Januari 2025,bila kuvunjika bali mshutuko na kufungwa kwa tahadhari.
Vatican News
“Leo asubuhi, kwa sababu ya kuanguka katika nyumba ya Mtakatifu Marta, Papa Francisko alipata mshtuko kwenye mkono wake wa kulia, bila kuvunjika."
Hayo yalitangazwa katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, ambapo ilielezwa kwamba: "mkono huo ulifungwa tu kama hatua ya tahadhari." Hata hivyo Papa Francisko alidumisha hata hivyo ajenda zake zilizokuwazimepangwa asubuhi tarehe 16 Januari 2025, ikiwa ni pamoja na ile ya kukutana na Nosipho Nausca-Jean Jezile, rais wa Kamati ya Usalama wa Chakula Duniani(CFS).
16 January 2025, 15:20