Tafuta

2025.01.22 Papa akutana na wajumbe wa Mfuko wa Hilton unaojikita kusaidia hasa wahitaji kuanzia na elimu kwa watawa. 2025.01.22 Papa akutana na wajumbe wa Mfuko wa Hilton unaojikita kusaidia hasa wahitaji kuanzia na elimu kwa watawa.  (Vatican Media)

Papa kwa Mfuko wa Hilton:ninaota waliotengwa kuwa mawakala wa mabadiliko!

Papa Francisko akikutana na wajumbe wa mfuko wa Hilton unaojikita na kutoa msadda hususani kwa mafunzo ya watawa ambao wanasaidia masikini amewashukuru sana lakini ametoa wito kwa Wakuu wa Mashirika ya kitawa ambao wanawakataza watawa kushika nafasi mbali mbali katika majimbo,kwamba:“kuweni wakarimu,jengeni maono ya Kanisa la kiulimwengu na la utume unaovuka mipaka ya Taasisi zenu.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 22 Januari 2025 amekutana na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Conrad Hilton. Katika hotuba yake Papa alisema kuwa, katika wakati wetu, kadiri idadi ya maskini na waliotengwa katika ulimwengu wetu inavyozidi kuongezeka, ndivyo wao walichagua kujitoa kikamilifu katika kukuza utu wa kibinadamu, binafsi kwa shauku na huruma, kama Msamaria Mwema. Mfano huo wa Yesu unatuhimiza kujitambulisha na mahitaji ya wengine, kuwafikia na kuwainua wale walioanguka kando ya njia, na kwa njia hii kutunufaisha sisi sote (taz. Fratelli Tutti, 67). Papa amesisitiza kuwa wasisahu kwamba katika tukio moja tu na katika tendo moja katika historia inaruhusiwa kutazama mtu kuanzia chini kwenda hasa wakati wa kumsaidia kuamka. Vinginevyo, huwezi kumtazam mtu vile mtu na wasisahau daima hilo." Mfuko wao umeonesha jinsi ukarimu na kujitolea kama hivyo unaweza kubadilisha maisha ya wale wanaojikuta katika mazingira magumu. Huduma wanayotoa kwa uhuru katika nyanja za elimu, afya, usaidizi wa wakimbizi na mapambano dhidi ya umaskini ni ushuhuda thabiti wa upendo na huruma. Papa aidha alisema wasisahau neno hili: huruma, "kuteseka pamoja." Mungu ni wa huruma, Mungu hutukaribia na kuteseka pamoja nasi. Na huruma sio kutupa sarafu mkononi mwa mtu mwingine bila kumtazama machoni. Hapana. Huruma inakaribia na "kuteseka naye". Msisahau neno hili: huruma."

Wajumbe wa Mfuko wa Hilton
Wajumbe wa Mfuko wa Hilton   (Vatican Media)

Mwanzilishi wao, Conrad Nicholson Hilton, aliacha ndoto yake, ambayo inaendelea kuhamasisha Mipango ya Mfuko huo. Miongoni mwa haya ni moja ambayo wamekuwa wakiikuza mara kwa mara: ile ya kuwaunga mkono watawa. Conrad Hilton aliwaheshimu sana Masista; katika wosia wake, aliiomba Mfuko uwaunge mkono katika utume wao wa kuwahudumia maskini na walio wadogo zaidi kati ya kaka na dada zetu. "Wakati fulani, mtu fulani aliniambia - alikuwa mwaminifu kuwa aliishia hospitalini, na watawa walimtunza… Ndiyo maana aliongoka. Na akasema: Kanisa lingekuwaje bila watawa… hii ni nzuri!" Kwa njia hiyo Papa Francisko aliwaeleza kuwa, wao wanafanya hivyo kwa uaminifu na ubunifu hasa kwa mchango wao katika malezi ya Masista wadogo na malezi ya wazee katika mashirika yao. Kwa kuongezea Papa alisema: "Katika baadhi ya nchi ni mabibi vikongwe, lakini hawapaswi kupelekwa kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi, hapana… Nakumbuka siku moja, huko Argentina, katika shirika fulani - ambapo nilikuwa na mtawa wa asili ya Kiitaliano - mkuu wa shirika  alikuja na kusema: "Hapana! Katika umri wa miaka 70, kuwa nje!”, na watawa walikuwa wanakufa kwa huzuni…

Watawa wanapaswa kufanya kazi hadi mwisho, kama wanaweza, hadi mwisho, amesisitiza Papa. Na wasipofanya hivyo, wafanya vile. Hapa tunaye ambaye amefanya kazi na maskini kila wakati. Yeye ni mzee, lakini bado anaendesha gari na wanamruhusu aendeshe, kwa hivyo anahisi kuwa muhimu. Tafadhali, watawa wadogo daima wawe pamoja na watu! Papa  alieleza pia anavyofahamu kwamba wameshirikiana na Mabaraza  kadhaa ya Vatican ili kuwapa Masista fursa ya kukua katika taaluma na uenezaji wa kimisionari. Amewashukuru sana kwa hilo! Ni kweli, kwa sababu inadhaniwa kuwa watawa, na hata wanawake, ni "wa shule za msingi". Wanafikiri hivi… Wasisahau kwamba tangu siku ya Bustani ya Edeni wamekuwa wakisimamia… Wanawake wamekuwa wakisimamia! Hapo awali, kidogo sana kiliwekezwa katika eneo hilo, kidogo sana kuliko malezi ya mapadre. Bado kuna haja ya Masista kuendelea na elimu na mafunzo ni ya dharura. Kazi yao mipakani, pembezoni na miongoni mwa maskini, inahitaji mafunzo na umahiri.

Wajumbe wa Mfuko wa Hilton
Wajumbe wa Mfuko wa Hilton   (Vatican Media)

Papa Francisko aidha alipenda wakumbuke pia kwamba misheni ya Masista ni kumtumikia aliye mdogo kabisa miongoni mwetu. Haifai kuwa watumishi wa mtu yeyote. Hili lazima likome, na wao kama Msingi wanasaidia kulitoa Kanisa katika mtazamo huo. Kwa upande mwingine, pia Papa alisema jinsi alivyowasikia Maaskofu wakilalamika na kusema, kwamba “wangependa kuwateua watawa katika baadhi ya ofisi za majimbo, lakini Wakuu wao hawatawaachilia.” Kwa hivyo Papa ametoa wito kwa wakuu wa mashirika kwamba “kuweni wakarimu, jengeni maono ya Kanisa la kiulimwengu na ya utume unaovuka mipaka ya Taasisi zenu.” Papa alisisitiza kwamba: "Watawa lazima wafanye kazi hadi mwisho, kama wanaweza, hadi mwisho. Na msipofanya hivyo, fanya vile. Hapa tunaye ambaye amefanya kazi na maskini kila wakati. Yeye ni mzee, lakini bado anaendesha gari, na wanamruhusu aendeshe, kwa hivyo anahisi kuwa muhimu. Tafadhali, watawa wadogo daima muwe  pamoja na watu! Lakini pia lazima niongeze kitu kingine: mara nyingi tunalalamika kwamba hakuna watawa wa kutosha katika nafasi za uwajibikaji, katika majimbo Curia na Vyuo Vikuu. Ni kweli.

Kwa upande mmoja, Papa amebainisha kuwa "ni kweli, lazima tushinde mawazo ya ukarani na mfumo dume. Tunamshukuru Mungu kwa sasa tunaye Msimamizi katika Curia, wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maisha ya kitawa. Tunaye Naibu Gavana wa Mji wa  Vatican ambaye atakuwa Gavana mnamo Machi. Tuna watawa watatu katika timu ya wale wanaochagua Maaskofu, na ambao walipiga kura zao. Tunaye Naibu Katibu wa Monsinyo Piccinotti katika APSA: mtawa ambaye ana digrii mbili za uchumi. Namshukuru Mungu watawa wako mbele na wanaweza kufanya vizuri kuliko wanaume. Ndivyo ilivyo… kwa sababu wana uwezo huo wa kufanya mambo, wanawake, na watawa wadogo.

Papa akutan na wajumbe wa Mfuko wa Hilton
Papa akutan na wajumbe wa Mfuko wa Hilton   (Vatican Media)

Papa aliwashukuru kwa kazi na huduma yao isiyochoka. Kwa pamoja tunaweza kujenga ulimwengu ambao kila mtu, bila kujali asili yake au hali yake, anaweza kuishi maisha ya heshima. Kwa pamoja tunaweza kusaidia kuwasha tumaini katika mioyo ya wale wanaohisi kuwa peke yao na wameachwa. Papa ameongeza kuelezea ndoto “Ninaota ulimwengu ambapo waliotupwa, waliotengwa, wanaweza kuwa mawakala wa mabadiliko yanayohitajika sana katika jamii, ili sisi sote tuishi kama kaka na dada. Mungu awabariki na Mama yetu awalinde. Papa amewawabarikii kutoka moyoni mwake na kuwaombea; na pia wamwombee!

Papa na wajumbe wa Mfuko wa Hilton
22 Januari 2025, 12:34