Nia za Papa Francisko kwa mwezi Januari 2025:haki ya elimu kwa wahamiaji na wakimbizi!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kaka kawaida ya kila mwezi video inayoundwa na Mtandao wa wa Kimataifa wa nia za Maombi ya Papa, kwa mwezi Januari 2025, Baba Mtakatifu anatoa sala yake ambaye anatetea haki za elimu kwa watoto na vijana ambao kwa sababu ya uhamiaji, Uhamisho unaosababishwa na vita na umaskini, hawana aina yoyote ya elimu. Kwa njia hiyo katika Ujumbe kwa njia ya video zjanga la kweli la elimu ambalo limeacha karibu watoto milioni 250 ambao hawana shule.
Elimu kwa wote, bila kujali hali zao za uhamiaji
Watoto na vijana ambao wanahama au kuhamishwa kwa sababu ya vita wanakabiliana na kukatisha mchakato wa elimu kwa sababu ya ulazima wa kukimbia katika nchi zao za kuzaliwa. Katika kesi nyingine, shule, katika sehemu za migogoro, au katika makambi ya wahamiaji wanapata fursa finyu kwa nyenzo za elimu, miundo inayofaa na walimu wenye sifa. Na zaidi, watoto na vijana wanapohamishiwa katika Nchi Nyingine au Kanda, hali yao ya uhamiaji inaweza kuwazuia wao kuendelea na elimu na matukio ya kuweza kuwa na wakati ujao mzuri. Kwa njia hiyo Papa Francisko anathibitisha katika video kuwa “watoto wote na vijana wana haki ya kwenda shule ,bila kujali hali zao za uhamiaji. ”Hili ni ombi hata hivyo la zamani, katika fursa mbali mbali, ambapo Baba Mtakatifu alikuwa ameomba kuwa wahakikishe wahamiaji na wakimbizi “ Uwezekano wa kwenda shule ya msingi na sekondari” na kama ilivyo kuishi mara kwa mara baada ya kufikia umri wa watu wengi na uwezekano wa kuendelea na masomo yao.”
Kanisa liko Mstari wa mbele
Ni watoto hasa na vijana ambao wako katika kukimbia migogoro au umaskini , walio mstari wa mbele katika picha ambazo zinasindikiza maneno ya Papa Francisko katika lugha ya kihispania: Katika Video ya Papa katika mwezi, unashuhudua jitihada ya kuwa msitari wa mbele wa kanisa katika kuhakikisha elimu kwao ambayo iko katika muktadha mgumu zaidi. Kuna vituo vya elimu vya Mfuko wa AVSI kwa ajili ya watoto wakimbizi, sehemu kubwa ya watoto kutoka Siria, Jordan na Lebanon. Kuna shule ya Kisalesiani huko Palabek, Uganda, mahali ambapo asilimia 60 ya wakimbizi wa Sudani wana chini ya miaka 13. Kuna taasisi ya Mama Maria Mpalizwa ya Tijuana, mpakani mwa Mexico na Marekani, inayoongoza na Familia ya Shirika la Wascabrini na wanaudhuria shule hiyo ni watoto kutoka sehemu mbali mbali za Nchi za Amerika Kusini.
Kuna jitihada tofauti katika ulimwengu wa Shirika la Kijesuit (JRS) Huduma ya Kijesuit kwa ajili ya wakimbizi, waliopo hata katika Mashariki ya Chad, ambapo ni karibu kizazi kizima kilichozaliwa na kukulia katika makambi ya wakimbizi. Kuna watu wa kujitolea wa Jumuiya ya Papa Yohane XXIII ambao wanasinidikiza watoto katika masomo, waliofika kutoka Ugiriki na Nchini Italia kupitia mapambano dhidi ya uhamiaji. Hazikosekani jitihada nyingine za mashirika ya kimataifa kama vile UNICEF, zilizopo na mipango ya kielimu katika nchini Nyingi zinazo karibisha, mahali ambapo katika miaka ya mwisho, watoto wengi wahamiaji, wa vita nchini Ukraine, waliweza kuendelea na kozi za lugha.
Wasiwasi wa Papa Francisko kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi
Nia za Papa Francisko kwa mwezi wa Januari kwa njia hiyo anatafakari moja ya mada msingi wa Upapa wake: wasiwasi kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi, ambao unazaliwa katika maneno ya Yesu katika Injili ya Matayo (25,35): “ Nilikuwa mgeni, na mkanikaribisha.” Kwa njia hiyo katika ujumbe wake, baba Mtakatifu anaisisitiza: “ tusisahau kamwe kuwa anayemkaribisha Mgeni, anamkaribisha Yesu Kristo.” Wakati uliopita Baba Mtakatifu, kwenye nia mbalimbali za sala kuhusu mgogogoro wa wahamiaji na wakimbizi alikuwa tayari amefafanua kuwa ni moja ya changamoto kubwa ya wakati wetu; ya mwisho ilikuwa ni mwezi Juni 2024 ambapo aliomba kusali “ ili wahamiaji na wakimbizi wa vita au njaa, waliolazimika kusafiri katikati ya hatari na vurugu, wapate kukaribishwa na kuwa na fursa mpua za maisha katika nchi zinazowakaribisha.”
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kimataifa wa Mtandao wa Maombi ya Papa, Padre Cristóbal Fones, S.J., anakumbuka kuwa “ katika fursa nyingi, Papa Francisko alibainisha kuwa ni lazima kupokea, kulinda, kuhamasisha na kufungamanisha wahamiaji na wakimbizi, tabia ambazo wote tunaweza na lazima kuzikuza katika maisha yetu ya kila siku. Tunataka kusaidia wakati wa mwezi huu, kuzigundua na kuziweka katika matendo kwenye maeneo tunayoishi.Papa anatueleza kuwa kila mgeni anayebisha hodi katika mlango wetu ni fursa ya kukutana na Yesu Kristo ambaye katika Injili anajifananisha na mgeni wa kukaribisha au kukataliwa, kwa kila wakati wa historia.”
Hata katika Tamko la kutangaza Jubilei ya Kawaida ambayo tumo tunaadhimisha, Papa Francisko anaomba wahamiaji na wakimbizi wahakikishiwe, si usalama na kupata kazi tu, lakini pia hata elimu,” alisema Padre Fones. Kwa njia hiyo: “Ni vizuri kukumbuka kuhusu Jubilei, kwamba mojawapo ya masharti ya lazima ya kupata Rehema Kamili iliyotolewa kwa Mwaka huu Mtakatifu ni hasa, kusali kwa ajili ya nia ya Baba Mtakatifu ambayo ni madhubuti na ambayo katika mwezi huu analenga kuheshimu msingi huu wa haki ya watu walio katika mazingira magumu sana.”