Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano:Papa atoa wito wa kuachiwa huru waandishi waliofungwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ndugu Msikilizaji wa Vatican News, katika fursa ya Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano iliyoanza tangu tarehe 24 na itahitimishwa tarehe Dominika tarehe 26 Januari 2025 awali ya Yote, Baba Mtakatifu Francisko akikutana na washiriki wa Jubilei hii katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican, kutokana hotuba yake iliyondaliwa kuwa ndefuyenye kurasa tisa, Papa Francisko alependelea kuikabidhi lakini kwa kutoa maneno machache bila kusoma aliwasalimia wote na kuwashukuru kufika kwao. Papa aliongeza kusema: “Nina hotuba ya kurasa tisa mikononi mwangu. Saa hii, kuanza kuisoma wakati tumbo langu litaanza kukoroma itakuwa mateso. Nitatoa hii kwa mkuu wa Baraza( akiwa anamaanisha Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambaye alifika na kupokea hotuba hiyo na ili aiwasilishe. Makofi mengi yalisikika katika Ukumbi huo na kuwauliza: “je mmependa?
Papa aliongeza kusema kuwa “Hata hivyo “Nilitaka kusema neno moja tu juu ya mawasiliano. Kuwasiliana kunamaanisha kujiondoa kidogo ili kutoa kitu changu kwa mwingine. Na mawasiliano sio tu kutoka, lakini pia kufanya mkutano na mwingine. Kujua jinsi ya kuwasiliana ni hekima kubwa. Hii ni hekima kubwa.” Pia Papa akasisitiza kuwa: “Nina furaha kuhusu Jubilei hii ya wawasilianaji. Kazi yenu ni kazi inayojenga; inajenga jamii, inajenga Kanisa, inamfanya kila mtu aendelee, maadamu ni kweli. Hata hivyo ameongeza kusema "Baba, mimi husema ukweli kila wakati ..." "Lakini je ni kweli? Sio mambo tu unayosema, lakini wewe, ndani yako, katika maisha yako, ni mkweli?" Ni mtihani mkubwa sana. Lakini kuwasiliana kile ambacho Mungu anafanya na Mwanae, na mawasiliano ya Mungu na Mwana na Roho Mtakatifu. Kuwasiliana na kitu cha kimungu. Asante kwa kile mnachofanya. Asante sana. Nina furaha. Papa alihitimisha kwa kusema kuwa: “Na sasa, ningependa kuwasalimu lakini kwanza kabisa nitoe Baraka zangu.” Alitoa Baraka zake na kuanza kusalimia wale waliopangwa. Jubilei hii imewaleta watu wengi, katika ukumbi wa Paulo VI uliokuwa hautoshi, na wengine walikaa nje na kwenye korido mbali mbali zilizomo kwenye ukumb huo wakifuatilia katika skrini.
Ifuatayo ni hotuba kamili ya Papa Francisko aliyoikabidhi
Wapendwa dada na kaka, habari za asubuhi! Ninawashukuru nyote kufika kwa njia nyingi na kutoka nchi nyingi tofauti, kutoka mbali na karibu. Inapendeza sana kuwaona nyote hapa. Ninawashukuru wageni waliozungumza kabla yangu - Maria Ressa, Colum McCann na Mario Calabresi - na ninamshukuru Mwalimu Uto Ughi kwa zawadi ya muziki, ambayo ni njia ya mawasiliano na matumaini. Mkutano wetu huu ni tukio kuu la kwanza la Mwaka Mtakatifu unaotolewa kwa "ulimwengu muhimu," ulimwengu wa mawasiliano. Jubilei inaadhimishwa katika wakati mgumu katika historia ya binadamu, huku dunia ikiwa bado imejeruhiwa na vita na ghasia, kwa kumwaga damu nyingi zisizo na hatia. Kwa sababu hiyo Papa alitaka, kwanza kabisa kusema “asante kwa wafanyakazi wote wa mawasiliano ambao wanahatarisha maisha yao kutafuta ukweli na vitisho vya vita. Papa alipenda kuwakumbuka katika sala wale wote waliojitolea maisha yao katika mwaka huu wa mwisho, na kupata mauti kwa waandishi wa habari. Tunawaombee wote ambao wametia saini utumishi wao kwa damu zao kimya kimya.
Pia Papa alipenda kuwakumbuka pamoja nao wale wote ambao wamefungwa kwa sababu tu ya kuwa waaminifu kwa taaluma ya uandishi wa habari, wapiga picha, wachukuaji video, kwa kutaka kwenda kujionea kwa macho yao na kujaribu kueleza walichokiona. Wapo wengi sana! Lakini katika Mwaka huu Mtakatifu, katika Jubilei hii ya ulimwengu wa mawasiliano, Papa amewaomba wale ambao wana uwezo wa kufanya hivyo wawaachie huru wanahabari wote waliofungwa gerezani pasiko haki. Na "mlango" ufunguliwe kwa ajili yao pia, ambao wanaweza kurudi katika uhuru, kwa sababu uhuru wa waandishi wa habari huongeza uhuru wetu sote. Uhuru wao ni uhuru kwa kila mmoja wetu. Katika hotuba hiyo Papa aliomba kama alivyofanya mara nyingi na kama watangulizi wake walivyofanya kabla yake, kwamba “uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza ulindwe na kutetewa, pamoja na haki ya kimsingi ya kuhabarishwa. Taarifa za bure, zinazowajibika na sahihi ni urithi wa maarifa, uzoefu na wema ambao lazima ulindwe na kukuzwa. Bila hilo, tunahatarisha kutoweza tena kutofautisha ukweli na uongo; Bila hilo, tunajiweka wazi kwa chuki na migawanyiko inayokua ambayo inaharibu miunganisho ya kuishi pamoja kwa raia na kuzuia uundaji upya wa udugu.
Uandishi wa habari ni zaidi ya taaluma. Ni wito na utume. Kwa hiyo wawasilianaji wana jukumu la msingi kwa jamii leo hii, katika kusema ukweli na jinsi wanavyowaambia. Papa amebainisha “Tunajua: lugha, mtazamo, sauti, inaweza kuwa ya maamuzi na kuleta tofauti kati ya mawasiliano ambayo hufufua matumaini, kuunda madaraja, kufungua milango, na mawasiliano ambayo badala yake huongeza migawanyiko, kuchochea, na kurahisisha ukweli. Wajibu wa waandishi ni wa kipekee, Papa anasisitiza. Kazi yao ni ya thamani. Vyombo vyao vya kufanya kazi ni maneno na picha. Lakini kabla ya haya, kujifunza na kutafakari, uwezo wa kuona na kusikiliza; kujiweka upande wa wale waliotengwa, wale ambao hawaonekani wala kusikika na pia kufufua, katika mioyo ya wale wanaokusoma, kuwasikiliza, kuwatazama, hisia ya mema na mabaya na kumbukizi kwa mema wanayosema na kwamba, kwa kusema, wanashuhudia. Katika mkutano huu maalum, Papa pia kuongeza mazungumzo na wanahabari. Na amewashukuru kuweza kufanya hivyo kuanzia mawazo na maswali ambayo waandishi wawili walishirikisha muda mfupi ndani ya Ukumbi huo wa Paulo VI. Kama vile Maria, alizungumzia juu ya umuhimu wa ujasiri wa kuanzisha mabadiliko ambayo historia inaomba, ni mabadiliko muhimu ili kushinda uwongo na chuki.
Ni kweli, inahitaji ujasiri kuanzisha mabadiliko. Neno ujasiri linatokana na neno la Kilatini cor, cor habeo, ambalo linamaanisha "kuwa na moyo." Ni ule msukumo wa ndani, nguvu hiyo itokayo moyoni ndiyo hutuwezesha kukabiliana na magumu na changamoto bila kuingiwa na woga. Kwa neno ujasiri tunaweza kurejea tafakari zote za Siku za Hupashanaji habari Ulimwenguni za miaka ya hivi karibuni, hadi Ujumbe wa jana(akiimaanisha tarehe 24 Januari 2025: kusikiliza kwa moyo, kusema kwa moyo, kulinda hekima ya moyo, kushiriki tumaini la moyo. Papa anabainisha kuwa “katika miaka ya hivi karibuni, imekuwa moyo mwake ambapo ameamuru miongozo ya kutafakari kwetu juu ya mawasiliano. Kwa hiyo Papa alipenda kuongeza ombi lake la ukombozi wa waandishi wa habari yaani "wito" mwingine unaotuhusu sisi sote: ule wa "ukombozi" wa nguvu za ndani ya moyo. Kwa kila moyo! Si juu yetu kujibu wito wa mwingine.
Uhuru ni ujasiri wa kuchagua. Tuchukue fursa ya Jubilei kufanya upya na kugundua tena ujasiri huu. Ujasiri wa kuukomboa moyo kutokana na kile kinachouharibu. Hebu tuweke heshima kwa sehemu ya juu na adhimu ya ubinadamu wetu katikati ya mioyo yetu, na tuepuke kuijaza na kile kinachooza na kuifanya kuoza. Chaguzi ambazo kila mmoja wetu hufanya kuhesabu, kwa mfano, katika kuondoa "kuoza kwa ubongo" kunakosababishwa na madawa ya kulevya, kuendelea kujisogeza kwenye mitandao ya kijamii, inayofafanuliwa na Kamusi ya Oxford kama neno la mwaka. Je, tutapata wapi tiba ya ugonjwa huu ikiwa si kwa kushirikiana kutoa mafunzo, hasa kwa vijana? Tunahitaji ujuzi wa vyombo vya habari, ili kujielimisha sisi wenyewe na wengine katika kufikiri kwa makini, katika uvumilivu wa utambuzi muhimu kwa ujuzi; na kukuza ukuaji wa kibinafsi na ushiriki hai wa kila mtu katika siku zijazo za jamii. Tunahitaji wajasiriamali wenye ujasiri, wahandisi wa kompyuta wenye ujasiri, ili uzuri wa mawasiliano usiharibiwe. Mabadiliko makubwa hayawezi kuwa matokeo ya wingi wa akili zilizolala, bali huanza na ushirika wa mioyo iliyotiwa nuru.
Moyo wa Mtakatifu Paulo ulikuwa hivyo. Kanisa linaadhimisha kuongoka kwake leo hii tarehe 25 Januari. Badiliko lililotokea kwa mtu huyu lilikuwa la kupambanua sana kiasi kwamba liliashiria sio tu historia yake ya kibinafsi bali ya Kanisa zima. Na kubadilika kwa Paulo kulisababishwa na kukutana ana kwa ana na Yesu aliyefufuka na aliye hai. Nguvu ya kuanza njia ya mabadiliko daima hutolewa na mawasiliano ya moja kwa moja kati ya watu. Papa aliongeza kusema, fikiria ni kiasi gani cha nguvu za mabadiliko kinaweza kufichwa katika kazi ya waandishi ya kila wakati wanapoleta pamoja ukweli ambao, kupitia ujinga au chuki - unapingwa! Uongofu wa Paulo ulitokana na nuru iliyomfunika na kutokana na maelezo ambayo Anania alimpatia baadaye huko Damasko. Kwa hiyo kazi ya waandishi inaweza na lazima pia kutoa huduma hii: kutafuta maneno sahihi kwa miale hiyo ya mwanga ambayo inaweza kugusa moyo na kutufanya tuone mambo kwa njia tofauti.
Na hapa Papa alipenda kuunganishwa na mada ya nguvu ya mageuzi ya usimulizi, na kusikiliza historia, ambayo Colum aliakisi. Hebu turudi kwa muda kwenye uongofu wa Paulo. Tukio hilo linasimuliwa katika Matendo ya Mitume mara tatu (9.1-19; 22.1-21; 26.2-23), lakini kiini daima kinabakia kuwa Sauli anakutana na Kristo; njia ya kueleza mabadiliko, lakini uzoefu wa mwanzilishi na mabadiliko bado haujabadilika. Hata hivyo kati Hotuba ndefu ya Papa aliyokabidhi anabainisha kuwa, kusimulia historia ni mwaliko wa kuwa na uzoefu. Wanafunzi wa kwanza walipomwendea Yesu na kumuuliza, “Bwana, unakaa wapi?” (Yh 1:38 ) Hakuwajibu kwa kuwapa anwani yake ya nyumbani, bali alisema: “Njooni mwone” (Yh 1, 39). Historia zinaonesha kuwa sisi ni sehemu ya kitambaa hai; kuunganishwa kwa nyuzi ambazo tumeunganishwa kwa kila mmoja. Sio historia zote ni nzuri, lakini hata hizi zinahitaji kusimuliwa. Uovu lazima uonekane kukombolewa; lakini inatakiwa kuambiwa vizuri ili isichakae nyuzi tete za kuishi pamoja. Kwa hiyo, katika Jubilei hii, Papa Francisko anatoa wito mwingine kwa wale waliokusanyika hapo na kwa wawasilianaji ulimwenguni kote: pia kusimulia historia za matumaini, historia zinazorutubisha maisha. Simuliz zao za historia ziwe za kutumaini.
“Unaposimulia historia ya uovu, unaacha nafasi kwa uwezekano wa kurekebisha kile kilichochanika, kwa ajili ya nguvu ya mema ambayo inaweza kutengeneza kile kilichovunjika. Kupanda maswali. Kusema juu ya tumaini kunamaanisha kuona makombo ya mema yaliyofichwa hata wakati yote yanaonekana kupotea inamaanisha kuruhusu sisi kutumaini hata dhidi ya matumaini yote. Inamaanisha kutambua machipukizi yanayotokea wakati dunia ingali imefunikwa na majivu. Kusema juu ya tumaini kunamaanisha kuwa na mtazamo ambao hubadilisha mambo, kuwafanya kuwa kile wanachoweza na kile ambacho wanapaswa kuwa. Inamaanisha kufanya mambo kuelekea kwenye hatima yao. Hii ni nguvu ya historia. Na hivyo ndivyo Papa amehiza ulimwengu wa wanahabari kufanya: kusema historia ya matumaini, na shirikisha. Hii ni kama Mtakatifu Paulo angesema kwamba "vita vyenu vyema." Papa anahitimisha hotuba hiyo aliyowakabidhi huku akiwabariki na kazi zao. Na kuomba wamwombee.