Siku kuu kubwa katika mji wa kishasa,milioni 1 wanacheza na kumwimbia Papa
Na Angella Rwezaula;– Vatican.
Ndugu msomaji na msikilizaji wa Vatican News, wawakilishi wetu wanatuelezea kile ambacho kinaendelea Jumatano tarehe Mosi Februari, wakati wa misa Takatifu katika Uwanja wa Ndege wa Ndolo, jiji la Kishasa DRC katika Hija ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko aliyofika huko tarehe 31 Januari 2023. Hawa ni wanaume, wanawake, watoto, wazee, makuhani, watawa, katika uwanja huo mkubwa ambapo mapema asubuhi au kutoka siku kabla ya kuchwa waliweza kufika. Kila mtu anamshukuru Papa Francisko kwa uwepo wake, kwa matumaini kwamba ainawezekana kubadilisha kitu. Hasa mashariki mwa nchi ambapo kaka na dada zetu wanauana hivyo.
Kwa maana hiyo katika maelezo ya mwandishi wamebainisha kwamba wengine walilala kwa usiku mbili mfululizo katika uwanja huo mkubwa wa kijani kibichi ambao ni wa ndege huko Ndolo, kwenye kingo za mto Funa, ili kupata nafasi za kwanza nyuma ya vizuizi na labda kuweza kusalimiana na hata na père François kwa karibu kama wanavyomuita. Walitoka Kinshasa yote , lakini pia kutoka Brazzaville na miji au nchi nyingine za jirani. “Vive le Pape, vive le Pape!, wanapaza sauti wakipeperusha bendera zenye sura ya Papa, bila kukatiza miondoko ya mabega na kwa mdundo wa nyimbo wakitumia vyombo vya muziki kama magitaa ya umeme na pianola ya sintetiki, kwaya kiukweli ni kubwa ambayo ilianza kufanya mazoezi tangu saa moja asubuhi. Zaidi ya waamini milioni moja wamehudhuria Misahiyo kwa ajili ya amani na haki ambayo ni matarajio ya Papa Francisko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na ambayo imeadhimishwa kutumia Misale ya Kirumi kwa ajili ya majimbo ya Zaire.
Ili kuruhusu ushiriki katika tukio hilo, mamlaka za serikali zimetangaza siku hii tarehe Mosi kuwa sikukuu ya kitaifa. Shule na biashara zimefungwa. Tangazo hilo lilitolewa tarehe 31 Januari mchana kwenye vyombo vya habari vya serikali na Waziri wa Mawasiliano na Vyombo vya Habari, Bwana Patrick Muyaya, ambaye akizungumza kwa njia ya vipaza sauti vya Radio Vatican - Vatican News amesema : “Ni ziara ya kihistoria na ya kiishara kwetu. Tunayo furaha kumkaribisha Papa, mliona jana mamilioni ya Wakongo waliokuwa mtaani kumkaribisha... Tumefurahishwa sana na hotuba aliyoitoa jana kwa sababu ilikuwa ya wazi kabisa na alizungumza kwa ukali na tunatumaini waliosikiliza walikubali ujumbe wake na atafanya kazi kwa ajili ya kurejesha amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Huko N'Dolo, uwanja wa pili katika manispaa ya Barumbu, kaskazini mwa Kinshasa, wimbi la wanadamu limemiminika, linaloundwa na wanawake waliovaa nguo za kiutamaduni zilizoshonwa kwa alama za kikabila, picha za Papa na misemo kutoka Injili, wanaume wakiwa wamevaa nguo za kiutamaduni zilizoshonwa sare au mashati, wazee wenye miavuli ya kujikinga na jua, watoto wenye vidole gumba mdomoni wakipungia kamera inayowachukua picha. Kisha kuna watawa na mapadre. Takriban 3,000 kati ya hao wa mwisho, miongoni mwao baadhi ni kama “kondoo weupe”, kama mmishonari mmoja Padre Massimiliano Nazio alivyosema kwa upendo. Yote yamepangwa kila upande wa altare kubwa nyekundu na nyeupe, iliyozingirwa na njiwa wawili weupe na maandishi “Tous réconciliés en Jésus-Christ. Wote wapatanishwe katika Yesu Kristo”, ambayo ni kauli mbiu ya Ziara ya 40 ya kitume ya Papa Francisko.
Kunwa waichana wadogo wapatao hamsini waliovalia mavazi meupe ya Komunyo ya Kwanza wakitamadunisha misa nzima bila kucho kwa muda wote ambao Papa Pia Papa aliwazungukia waamini kwenye gari la popemobile. Papa Francisko aidha aligeuka huku na kule, huku akijaribu kuwabariki licha ya jua kali, na kupokea mapokezi ya macho ya furaha na ukarimu ambao ni rasilimali kubwa zaidi ambayo nchi bado haijaibiwa. “Amani iwe kwenu”, alisema, na kuongeza kwa lugha ya Kiswahili: “Bandeko, boboto… Esengo. Amani, udugu, furaha. Zawadi ambazo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inahitaji leo hii.