Madhabahu ulimwenguni kusali rosari mwezi Mei ili janga liishe
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Madhabahu thelathini, yanayowakilisha ulimwengu wote, yataongoza kusali Rozari kila siku kwa mwezi Mei katika mbio ya maombi yanayoongozwa na kaulimbiu: “Kutoka Kanisa lote Maombi yalipaa kwenda kwa Mungu”, ambalo ni wazo la Papa Francisko na kuhamasishwa na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha uinjilishaji Mpya na tukio hilo ambalo litawahusisha kwa namna ya pekee madhabahu yote ulimwenguni, ili wawe wahamasishaji wa waamini, familia na jumuiya zote kusali Rosari Takatifu
Siku ya kwanza ya mwezi Mei, Papa atafungua kwa sala na kufunga mwishoni
Sala ya Rosari itafunguliwa na Papa Francisko siku ya kwanza ya mwezi Mei, na pia kuhitimisha na yeye mwenyewe manmo tarehe 31 Mei 2021. Sala ya Rosari Takatifu hiyo itatangazwa moja kwa moja na majukwaa rasimi ya Vatican, kuanzia saa 12.00 jioni kila siku. Ikumbukwa kuwa tangu Jumatatu tarehe 17 Aprili, hadi Jumamosi saa 6.00 za kila siku, sala ya Rosari Takatifu imeanza kwa mara nyigine tena katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatica, ikiongozwa na Kardinali Angelo Comastri, Makamu mstaafu wa Papa katika Mji wa Vatican na Paroko mstaafu wa Kanisa hilo Kuu.
Rosari takatifu wakati wa wimbi la janga mnamo Machi 2020
Kipindi hicho cha sala kilikuwa kimeanzishwa mnamo Machi 2020 ili uongeza matumaini waamini na aenye mapenzi mema wakati wa mwanzo wa wimbi la janga ambalo hata leo hii bado linaendelea na ambapo sasa inawezekana kufuatilia moja kwa moja kupitia Tovuti ya Vatican News na Masafa ya Radio Vatican, Italia.