Tafuta

Kongamano la Kimataifa la SIGNIS Kigali Kigali, Rwanda 2026 kuanzia 3-8 Agosti Kongamano la Kimataifa la SIGNIS Kigali Kigali, Rwanda 2026 kuanzia 3-8 Agosti 

Kila kitu tayari kwa Kongamano la Kimataifa la SIGNIS 2026 Kigali Rwanda!

Kongamano la Kimataifa la SIGNIS litawaleta Wazungumzaji Wakatoliki kutoka zaidi ya nchi 100 jijini Kigali nchini Rwanda kuanzia tarehe 3 hadi 8 Agosti 2026."Mchakato wa maandalizi umekuwa mkubwa na wenye mahitaji,lakini pia umeoneshwa kwa ushirikiano mkubwa,ukarimu na kujitolea kwa pamoja katika kufanya Mkutano huu.”Alisema hayo Daniel Mugabonake,Katibu Mkuu wa Kudumu wa Kongamano la Kimataifa la SIGNIS Kigali 2026.

Na Sr. Molly Fernandes SFN.

Zaidi ya wataalamu 300 wa vyombo vya habari vya Kikatoliki, waandishi wa habari, watengenezaji filamu na wazungumzaji wa kidijitali kutoka zaidi ya nchi 100 watakusanyika Kigali kuanzia tarehe 3 hadi 8 Agosti 2026 kwa  ajili ya Kongamano la Dunia la SIGNIS 2026, ikiwa ni  kwa mara ya kwanza kufanyika mkutano kama huo wa kimataifa wa mawasiliano ya Kikatoliki kuandaliwa barani Afrika.

Uwakilishi kutoka mabara yote

Kwa kuwaandaliwa na Chama cha Kikatoliki Kimataifa cha Mawasiliano(SIGNIS), Kongamano hilo litafanyika katika Hoteli ya  Familia Takatifu (Sainte Famille) kwa kuongozwa na  kaulimbiu: "Mawasiliano ya Kidijitali kwa Ushirika, Usawa, Ustawi wa Mazingira." Mkutano huo utawapatia wawasilianaji Wakatoliki kutoka  ulimwenguni kote fursa ya kubadilishana uzoefu, kuchunguza changamoto zinazojitokeza katika vyombo vya habari na mawasiliano ya kidijitali, na kuimarisha ushirikiano katika kutumia mawasiliano kama njia ya kukuza ushirika, haki na amani. Kuna uwakilishi mkubwa kutoka Matawi ya Signis  ulimwenguni kote kuanzia  Asia, Amerika kaskazini, Kusini, Canada, Ulaya na kwingeko.

Siku nne za vikao na mijadala:Watawa ni miongoni mwao kwa Mpango wa Pentekoste

Programu hiyo ya siku nne itaakisi vikao vya jumla na mijadala ya makundi  itakayoshughulikia masuala muhimu  kwa kulinganisha mawasiliano katika ulimwengu mamboleo. Miongoni mwa mada zitakazochunguzwa ni:  Sinodi kama kielelezo cha kuishi pamoja kwa amani na maendeleo ya kijamii; mawasiliano ya kidijitali kwa ajili ya ushirika na maelewano; watawa na  utendaji wa utamaduni katika enzi ya kidijitali; Mpango wa Pentekoste na Wito wa Hekima, ambapo utachunguza jinsi wataalamu wawasilianaji na watawa wanavyoweza kushirikiana ili kuhamasisha sauti za Watawa katika nyanja ya umma. Zaidi ya watawa kumi na wawili wamepangwa kushiriki kama wazungumzaji wakuu na wanajopo, huku wakisisitiza mchango unaoongezeka wa watawa wa kike  katika huduma ya vyombo vya habari, uinjilishaji na mabadiliko ya kijamii.

Mama Yetu wa Kibeho
Mama Yetu wa Kibeho

Ufunguzi wa Kongamano na Misa ikiongozwa na Kardinali Kambanda

Kongamano litaanza na Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Mikaeli, litakaloongozwa na Kardinali Antoine Kambanda, Askofu Mkuu wa Kigali, huku mapadre kutoka sehemu mbalimbali za dunia wakishiri. Zaidi ya  Kongamano hilo,  wajumbe watapata fursa za  kufanya maombi, tafakari na kuzamishwa kiutamaduni kupitia ziara za katika Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali na mazingira ya asili ya Kigali, pamoja na hija kwenye Madhabahu ya  Mama Yetu wa Kibeho, mojawapo ya maeneo muhimu ya hija ya Kikatoliki nchini Rwanda.

Kardinali Kambanda, Askofu Mkuu wa Kigali Rwanda
Kardinali Kambanda, Askofu Mkuu wa Kigali Rwanda

Watu wa kujitolea kupokea wageni

Maandalizi ya Kongamano hilo la  kimataifa limejumuisha mipango ya malazi, usafiri na wema wa  wajumbe. Watu wa kujitolea watawekwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali na katika makutano muhimu ya jiji ili kuwasaidia washiriki wanaowasili wafike salama. Watatambuliwa na fulana rasmi za SIGNIS World Congress zilizotolewa  tarehe 1 Agosti 2026.

Mugabonake: "Rwanda ilikuwa tayari kupokea familia ya Kimataifa ya Signis

Kwa pande wa Daniel Mugabonake, Katibu Mkuu wa Kongamano la Kimataifa la SIGNIS Kigali 2026, alisema maandalizi hayo yameoneshwa kwa ushirikiano na kujitolea kwa pamoja katika kukaribisha jumuiya ya kimataifa ya SIGNIS. "Huku Kongamanao la Kimataifa la SIGNIS Kigali 2026 likikaribia, tunashukuru kwa safari ya ajabu ambayo imetufikisha wakati huu," alisema. "Mchakato wa maandalizi umekuwa mkubwa na wenye mahitaji, lakini pia umeoneshwa kwa ushirikiano mkubwa, ukarimu, na kujitolea kwa pamoja katika kufanya Mkutano huu kuwa uzoefu wa kukumbukwa kwa washiriki kutoka ulimwenguni kote.” Aliongeza kuwa Rwanda ilikuwa tayari kukaribisha familia ya kimataifa ya SIGNIS na kuonesha ukarimu, imani na roho ya ubora wa nchi hiyo.

Signis kuhamasisha mawasiliano yanayoendeleza hadhi ya binadamu,haki na amani

SIGNIS inawaleta pamoja wataalamu wa vyombo vya habari Wakatoliki wanaofanya kazi katika televisheni, radio, sinema, uandishi wa habari, mtandao na elimu ya vyombo vya habari katika nchi zaidi ya 100. Chama cha Signis kinahamasisha mawasiliano yanayoendeleza hadhi ya binadamu, haki na amani na kinalenga kuimarisha uwepo na utume wa Kanisa katika mazingira ya vyombo vya habari yanayobadilika kwa kasi. Kongamano la Kigali linatarajiwa kutoa jukwaa muhimu kwa wawasilianaji Wakatoliki kutafakari jinsi vyombo vya habari vya kidijitali vinavyoweza kusonga mbele zaidi ya kushiriki habari na kuwa chombo cha ushirika, mazungumzo, ujumuishaji wa kijamii na utunzaji wa kazi ya  uumbaji.

Imesasishwa tarehe 1 Agosti 2026 saa 3.24 asubuhi na Angella Rwezaula - Vatican.

Signis 2026 Kigali Rwanda

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

01 Agosti 2026, 09:24