Tafuta

Ubatizo wa Yesu. Ubatizo wa Yesu. 

Jordan,maandalizi yanaanza kwa ajili ya sherehe za Ubatizo wa Kristo mwaka 2030

Mkutano wa kwanza wa Kamati itakayoandaa na kusimamia tukio hilo kubwa la kihistoria na kidini ilifanyika tarehe 10 Agosti.Ukiongozwa na Waziri Mkuu Hassan,unaundwa na mawaziri,viongozi wa kidini na wawakilishi wa taasisi.Sambamba na maagizo ya Mfalme Abdullah II,rasilimali zote zimekusanywa kutekeleza miradi mbalimbali,kama vile jumba la makumbusho na kijiji cha mahujaji.

Vatican News

Jordan imeanza maandalizi ya sherehe za milenia ya pili ya Ubatizo wa Yesu Kristo, zitakazofanyika mwaka 2030. Siku ya Jumatatu, tarehe 10 Agosti 2026, Waziri Mkuu wa Jordan Bwana Jafar Hassan aliongoza mkutano wa kwanza wa Kamati ya Kitaifa inayohusika na kusimamia tukio hili muhimu la kidini na kihistoria. Kamati, kulingana na taarifa ya serikali, inaundwa na mawaziri, viongozi wa kidini na jamii, na wawakilishi wa taasisi husika. Inatumika kama kitovu cha kitaifa cha maandalizi na usimamizi wa sherehe hizo na inawajibika kwa kutengeneza sera na miongozo ya jumla, kuratibu shughuli za kimataifa za uhamasishaji na taratibu za kitaifa, na kupanga matukio ya maadhimisho ya miaka.

Sambamba na maagizo ya Mfalme Abdullah II

Wakati wa mkutano huo, Waziri Mkuu Hassan alisisitiza hitaji la kuanza mara moja maandalizi sambamba na maagizo ya Mfalme Abdullah II, ili kuunga mkono mpango uliotolewa na Baraza la Viongozi wa Makanisa huko Jordan, kwa kuzingatia mpango kamili na ratiba iliyofafanuliwa wazi.

Alisema zaidi kwamba "ukumbusho wa milenia ya pili ya Ubatizo wa Kristo unaonesha heshima ya kihistoria na kidini ya Jordan na jukumu lake kama mahali pa kimataifa pa hija ya Kikristo," huku pia akisisitiza "ujumbe wa Ufalme wa kuishi pamoja, heshima kwa wengine, amani, upendo, na undugu wa kibinadamu."

Hassan pia alisema kwamba "serikali inakusanya rasilimali zote zinazopatikana ili kuunga mkono tukio hilo, akielezea kama fursa ya kuimarisha nafasi ya Jordan kama nchi ya urithi wa kidini na mahali pa kimataifa kwa mahujaji Wakristo."

La riunione del Comitato

Mkutano wa Kamati ya maandalizi

Mipango mbalimbali

Wakati wa mkutano huo, mipango ya Mfuko wa Maendeleo wa Ardhi, iliyo karibu na mahali pa  Ubatizo kwa mipango  kadhaa ilipitiwa, ikiwa ni pamoja na kijiji cha mahujaji na wageni Wakristo, jumba la makumbusho lililowekwa wakfu kwa ajili ya Ubatizo, ukanda wa kijani kibichi, na uboreshaji wa miundombinu ya eneo hilo. Washiriki pia walisisitiza umuhimu wa kuanzisha kamati ndogo maalum ili kusimamia utekelezaji wa mipango na kuhakikisha kufikiwa kwa malengo yaliyowekwa, kwa usaidizi wa wataalamu.

Muundo wa Kamati

Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Sherehe ya Milenia ya Pili ya Ubatizo wa Yesu Kristo mwaka 2030 inaongozwa na Waziri Mkuu. Wajumbe wake ni pamoja na Mawaziri wa Mawasiliano, Mambo ya Ndani, Uchumi wa Kidijitali na Ujasiriamali, pamoja na Utalii na Urithi wa Utamaduni. Mjumbe huyo pia anajumuisha: Askofu Christophoros Atallah, Askofu Mkuu wa Kiorthodox wa Ugiriki wa Jordan; Askofu Mkuu Iyad Twal, wa Upatriaki wa Kilatini huko Jordan; Askofu Mkuu Hossam Naoum, Askofu Mkuu wa Kianglikani; Askofu Munib Younan, Askofu wa zamani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri; Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko  wa Maendeleo ya Eneo la Ubatizo; Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Eneo la Ubatizo; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Utalii ya Jordan; Nadim Al-Mauasher; Osama Imseeh; na Basem Farraj.

Il primo ministro della Giordania, Jafar Hassan

Waziri Mkuu wa Jordan Bwana, Jafar Hassan

JORDAN UBATIZO 2030

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

11 Agosti 2026, 10:29