Tafuta

Sehemu ya wafanyakazi wa Kituo cha Matibabu cha Kikatoliki cha Mtakatifu Monica. Sehemu ya wafanyakazi wa Kituo cha Matibabu cha Kikatoliki cha Mtakatifu Monica.  

Cameroon:Kuchagua kukaa katikati ya migogoro na umaskini

Mkoa wa Kaskazini Magharibi mwa Cameroon katika kijiji cha Baba 1, Masista wa Muungano Mtakatifu wanaendelea kuhudumia jamii iliyojaa umaskini,ukosefu wa usalama na migogoro, wakitoa huduma za afya,msaada na matumaini kwa wale wanaohitaji zaidi.

Sr. Kum Shallotte Bi, SUSC.

Katika kijiji cha mbali cha Baba 1, jamii ya vijijini katika Mkoa wa Kaskazini Magharibi mwa Cameroon, Shirika la Masista wa Muungano Mtakatifu wameishi na kufanya kazi miongoni mwa watu tangu miaka ya 1960. Kijiji hiki cha Baba1, kwa muda mrefu kimekuwa katika hali mbaya ya umaskini uliokithiri, upatikanaji duni wa barabara, umeme mdogo, vyanzo vya maji visivyo salama, viwango vya juu vya kutojua kusoma na kuandika, na utapiamlo hasa miongoni mwa watoto.

Kukaa na watu

Katika miaka ya hivi karibuni, mgogoro unaoendelea wa silaha umezidisha majeraha haya. Ukosefu wa usalama, utekaji nyara uliokithiri, na vifo vya mapema vimekuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Masista wa Muungano Mtakatifu wamechagua kubaki na wenyeji wa eneo hili hata changamoto zikiongezeka na hali ikizidi kuwa ngumu. Licha ya barabara ya kitaifa iliyochongoka na uboreshaji mdogo wa lishe ya watoto, mapambano ya msingi yanaendelea. Muungano Mtakatifu unabaki kuwa jamii pekee ya kidini katika eneo hili. Wanaweza kurudia maneno ya Mtunga Zaburi. "Hata lini, Ee Bwana, utanisahau milele?" (Zaburi 13:1). Hata hivyo, kila asubuhi masista hawa huamka kuitikia witi wao kwa wale wanao wategemea.

Mama na watoto wao wakisubiri kutibiwa katika kituo cha Mtakatifu Monica
Mama na watoto wao wakisubiri kutibiwa katika kituo cha Mtakatifu Monica

Ukarimu wa kila siku

Ni nini kinachowaweka hapo wakati wengine wengi wanapokimbia? Jibu liko katika nyuso zinazowakaribisha kila siku, kama vile bibi anayehitaji huduma ya matibabu, mwanamke mjamzito anayeumwa akisubiri kujifungua salama, mtoto anayepata kifafa anayehitaji huduma ya haraka, mwanamume anayetokwa na damu kutokana na ajali, familia zenye majonzi kwa kumpoteza mpendwa wao na kutokuwa na uhakika wakitafuta uhakikisho, wafanyakazi wanaowategemea kwa riziki ya kila siku, na vijana wanaotafuta mwongozo kwa mfano. Ukweli huu wa kila siku unaonyesha sharti la injili. "Chochote mlichomfanyia mmoja wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinifanyia mimi." (Mathayo 25:45). Watawa hawa waliojitolea kawa wakaazi wa kijiji cha Baba 1 hawawezi kuwageuka na kuwaaacha watu hawa ambao ni uso wa Kristo kati yao. Imani iliyowekwa kwao na wanakijiji inakuwa msalaba na baraka, upatikanaji halisi ulioahidiwa katika taaluma yao ya kidini.

Huduma ya afya na upendo

Huduma ya afya inabaki kuwa kitovu cha dhamira yao katika kijiji cha Baba 1 kama jibu la kila siku kwa mateso ya wanadamu. Huduma katika Kituo Katoliki cha Matibabu cha Mtakatifu Monica kinakabiliwa na changamoto maalum. Watu mahalia hawawezi kumudu kulipia huduma za matibabu wanazohitaji sana, lakini bado wanatibiwa. Kwa kuongezea, ni vigumu sana kupata wafanyakazi wa matibabu waliohitimu mara kwa mara. Ni wachache sana walio tayari kufanya kazi katika mazingira yasiyo salama na yasiyohudumiwa vya kutosha, na wale wanaokuja wanahitaji mishahara zaidi ya kile ambacho kituo hiki cha matibabu kinaweza kumudu.

Kitendawili kinaonekana wazi: mtu anawezaje kusimamia huduma zisizolipwa kwa maskini huku akidumisha rasilimali za kifedha za kuwalipa wafanyakazi wataalamu? Jibu limetokana na moja ya fadhila za Muungano Mtakatifu: Upendo. Dhamira yao ni kitendo cha upendo wa huruma. Sio upendo kama hisia tu bali upendo kama kujitolea kwa dhati kutumikia bila kuhesabu gharama.

Shahidi wa matumaini

Watu mahalia hawakuchagua kuzaliwa katika hali hizi, wala hawakuchagua mgogoro unaounda maisha yao sasa. Uwepo wa watawa ni jaribio rahisi la kuruhusu nuru ya Kristo iangaze mahali ambapo giza linatishia kutawala. Wakati mwingine hofu huingia, na kuhisi kana kwamba haiwezekani kuvumilia. Hata hivyo, maneno ya Mtakatifu Paulo yanabaki kuwa chanzo cha nguvu: "Neema yangu inatosha kwako, maana nguvu zangu hukamilishwa katika udhaifu." (2Wakorintho 12:9) Wakati mwingine, wao hupata nguvu kutokana na ustahimilivu wa watu wanaowahudumia. Ujasiri wao na uwezo wao wa kutumaini katikati ya shida pia huwahubiria injili. Hii inatumika kama ukumbusho kwamba utume si zawadi ya njia moja bali safari ya pamoja.

Maisha ya kitawa na ya kujitolea kwa watawa hawa kama wanavyoishi katika kijiji cha Baba 1 si njia ya kutoroka uhalisia bali ni kujizamisha ndani yake kwa kina. Nadhiri ambazo watawahawa huchukua huwasaidia kusimama katikati ya changamoto za kihistoria na kutetea maisha ambapo yanatishiwa zaidi. Katika kijiji cha Baba 1, hii ina maana ya kuchagua uwepo badala ya faraja na uaminifu badala ya usalama. Changamoto amabazo masista wanakabiliana nazo kila siku zinawasukuma kukumbatia njia ya uongofu kuelekea moyo wa Kristo. Kupitia matendo ya busara ya wema, wanatafuta kupunguza mizigo ya wale wanaowahudumia: mtoto kuzaliwa salama, mtoto mwenye homa anapopona, kidonda kilicho fungwa vizuri, familia iliyohakikishiwa, wafanyakazi kulipwa kwa haki, wazee kutunzwa, na wanawake vijana kufundishwa.

Vijana katika Warsha huko Cameroon
Vijana katika Warsha huko Cameroon

Nguvu halisi ya utume inakuja kupitia huduma ya masikini”

Watawa hawa pia hupata msukumo kutoka kwa Mtakatifu Teresa wa Calcutta, ambaye alielewa vizuri kwamba nguvu halisi huja kupitia huduma kwa maskini. Ingawa wengi katika ulimwengu unatangaza kwamba furaha inahitaji urahisi na maisha mazuri huepuka mateso, Masista wa Muungano Mtakatifu huko Baba1 wanashuhudia ukweli kwamba furaha inaweza kuishi pamoja na shida na maisha yenye kuridhisha yanaweza kuhusisha kukumbatia msalaba. Wito wao kama watawa hupata usemi wake wa kina katika utume huu dhaifu, wenye changamoto, na uliojaa neema.

Watawa  wanapochukua nadhiri zao za usafi wa moyo, umaskini, na utii, wanajitolea kwa uwepo mkubwa wa Mungu. Ni kujitolea kwa Mungu kunaowaongoza mahali ambapo hawakuwa wamafikiria. Masista wanatumaini kwamba siku moja, watu wa Baba 1 na jamii zote zilizoathiriwa na migogoro wataishi tena kwa amani na usalama. Mtakatifu Paulo katika barua yake kwa Warumi anathibitisha kwamba tumaini hili halikatishi tamaa. (Warumi 5:5) Mungu anayewaweka watu wake katika Kristo aendelee kufanya kazi ndani yao na kupitia wao kwa utukufu wake mkuu zaidi.

CAMEROON MASISITA WA MUUNGANO MTAKATIFU

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

11 Agosti 2026, 15:33