Maaskofu wa Venezuela watoa wito wa ujenzi mpya usio na uzembe na ufisadi
Na Alina Tufani Díaz.
Mwezi mmoja baada ya mitetemeko mawili ya ardhi kuikumba kaskazini na katikati mwa Venezuela, Maaskofu wa nchi hiyo wametoa ujumbe wenye kichwa: "Wasamaria Wema, MashahMashuhuda wa Matumaini." Matetemeko hayo ya ardhi yalichukua maelfu ya maisha kwani zaidi ya vifo 5,000 vimethibitishwa hadi sasa, lakini watu wengi bado hawajulikani walipo familia nyingi zimehamishwa na kuharibiwa nyumba, miundombinu na majengo ya Kanisa, na kuacha kile ambacho Maaskofu wanakielezea kama taifa "lililojaa huzuni."
Ujenzi usiongozwe na maslahi ya kisiasa
Maaskofu wanasema janga hilo limezidisha hali ngumu ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ya Venezuela, na wanasisitiza kwamba ujenzi upya haupaswi kuongozwa na maslahi ya kisiasa au ufisadi ambao unaweza tena kuweka maisha ya watu hatarini. Pia wanatoa wasiwasi kuhusu kile walichokielezea kama kushindwa kwa taasisi za umma kujibu ipasavyo dharura. “Ujenzi mpya pia unatutaka kurudia hasira ya waathiriwa wa tetemeko la ardhi ambao waliachwa bila msaada wa kutosha na taasisi za umma," waliandika. "Majanga ya asili hayatabiriki, lakini ni wajibu wa mamlaka za Serikali kuwa tayari kuyajibu," waliandika. Maaskofu wanaonya kwamba ikiwa watu wa Venezuela hawajifunza lolote baada ya teemeko hilo, wanyonge zaidi katika jamii wataathiriwa tena na kuteseka kwa sababu ya ufisadi na kutowajali.
Kujenga upya maisha
Ujumbe huo unatoa wito wa "ujenzi mpya wa haraka na wa kina" unaowapa wale waliohamishwa na tetemeko la ardhi makazi mazuri na ajira zenye hadhi, huku pia ukitoa msaada wa kiroho na kisaikolojia ili kusaidia kuponya kiwewe kilichosababishwa na janga hilo. Maaskofu wanaongeza kuwa ujenzi mpya haupaswi kuwapuuza wengine wanaoendelea kuteseka kote nchini, wakiwemo wafungwa wa kisiasa, wafanyakazi na wastaafu wanaoishi kwa kipato kidogo, wagonjwa na wahamiaji.
Mungu yuko pamoja na waathiriwa
Wakitafakari mfano wa Msamaria Mwema, maaskofu wanajibu swali ambalo mara nyingi huulizwa wakati wa msiba: "Mungu yuko wapi katikati ya mateso mengi?" Wanajibu kwamba Mungu yupo "ndani na pamoja na waathiriwa," ambao wanawaelezea kama wapendwa sana na Kristo, Msamaria Mwema wa kweli. Pia wanakataa kabisa madai kwamba matetemeko ya ardhi yalikuwa adhabu kutoka kwa Mungu, wakielezea madai kama hayo kama yenye mizizi katika ushirikina na ufuasi wa msingi.
Ushuhuda wa mshikamano
Maaskofu waliwahimiza waamini kuwa "Wasamaria Wema wenye huruma," wakishiriki mateso ya wengine na kufanya kazi kwa uhuru ili kupunguza maumivu yao. Pia walipongeza mshikamano ulioonyeshwa kote nchini, hasa na jamii maskini, na wanasifu ujasiri wa wafanyakazi wa uokoaji waliohatarisha maisha yao ili kuwaokoa watu walionaswa chini ya vifusi. Ujumbe huo unatoa shukrani kwa waliojitolea, wakiwemo wengi kutoka nje ya nchi, wakisema walionyesha kwamba watu wote ni ndugu hata nje ya mipaka na bendera za kitaifa. Maaskofu pia wanamshukuru Papa Leo XIV kwa ukaribu wake, pamoja na msaada wa Makanisa dada kote ulimwenguni na msaada wa kibinadamu unaotolewa kupitia mtandao wa Caritas za kitaifa na kimataifa. Hatimaye, waliwaalika waamini kushiriki katika Misa mnamo tarehe 24 Julai 2026 katika kila Parokia na Jumuiya, wakiwaombea wale waliopoteza maisha yao katika matetemeko ya ardhi, kwa wote walioathiriwa na janga hilo na kwa Venezuela.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.