Tafuta

2026.05.19 Roccaporena alikozaliwa Mtakatifu Rita wa Cascia:picha ni Sr Irmã Maria Atilia Collet na mwandishi wa Radio Vatican. 2026.05.19 Roccaporena alikozaliwa Mtakatifu Rita wa Cascia:picha ni Sr Irmã Maria Atilia Collet na mwandishi wa Radio Vatican.  (©Andressa Collet)

Nyayo za Mtakatifu Rita:Mtawa Mbrazil katika utume nchini Italia

Sr.Maria Atília Collet kwa mtakatifu Rita amepata mwanga katika sababu zisizowezekana na kumemuongoza maisha yake na ya maelfu ya mahujaji.Kabla ya kufika Roccaporena,mahali alipozaliwa Mtakatifu Rita mwaka 1381,utume wake ulimtoa Brazil hadi ndani ya Italia,Ureno,Hispania na Msumbiji.Alihudumia zaidi ya miaka 15 barani Afrika,ambapo aliimarisha uzoefu wa kibinadamu na kiroho ambako leo hii kunamwongoza katika kuwakaribisha mahujaji.

Na Andressa Collet – Vatican

Uhusiano unaounganisha mwanzo wa historia hii unavuka mataifa mawili, familia moja na ibada kwa Mtakatifu Rita wa Cascia. Makala haya pia, yanatokana na uhusiano huu, ulioandikwa na binti wa marehemu Rita Collet, binamu wa pili wa Sr. Maria Atília Collet. Sote tulizaliwa Brazil, lakini leo hii sisi sote wawili tunaishi Italia, ambapo historia ya familia yetu inapata utimilifu wake wa kiroho. Safari hii kupitia vizazi na maeneo inaelekea Umbria, katikati mwa Italia. Huko Roccaporena, mji mdogo takriban kilomita sita kutoka Cascia, mji unaohusiana sana na maisha ya Mtakatifu Rita. Leo hii Sr. Maria Atília anaishi Roccaporena alikozaliwa Mtakatifu Rita  Akiwa Mtawa wa Shirika la Kimataifa la Wamisionari wa Consolata, anaendelea kujitolea muda wake wa siku kuwakaribisha mahujaji waokwenda huko kwa ajili ya  sala na neema zinazotolewa kwa maombezi ya Mtakatifu  Rita ambaye anajulikana kwa maombezi yake kwa Sababu zisizowezekana.

Madhabahu ya Mtakatifu Rita huko Roccaporena
Madhabahu ya Mtakatifu Rita huko Roccaporena

Tangu kuhamia katika eneo hilo mwaka mmoja uliopita, Sr. Maria Atília alijumuisha ibada maalum ya kibinafsi katika maisha yake ya kila siku. Kila siku anamwombea mama yangu. "Hapa ndipo ninapomwombea mama yako," alisema. "Tangu siku nilipofika hapa, ninafungua mlango saa 11:30 asubuhi, na kumwombea mama yako ni kama kawaida."Mtawa huyo alikuwa akimaanisha Kanisa la Mtakatifu Montano huko Roccaporena. Ilikuwa hapa ambapo Mtakatifu Rita wa Cascia (1381-1457) alilelewa katika imani yake na kupokea Komunio yake ya Kwanza, Kipaimara na Ndoa. Uwanja wa Kanisa pia hutumika kama mahali pa maziko ya  wanafamilia wa  Mtakatifu Rita na wakazi wa zamani wa mji huo, kulinda kumbukumbu ya kihistoria ya jumuiya ya zamani ya mji huo.

Sr Maria Atilia akiwa nyumbani kwa Mtakatifu Rita
Sr Maria Atilia akiwa nyumbani kwa Mtakatifu Rita

Leo hii, Kanisa linawakaribisha mahujaji kutoka  ulimwenguni kote, wanaokuja kusali na kukabidhi nia zao zilizoonekana kuwa haziwezekani kupitia sala kwa Mtakatifu Rita. Katika mazingira haya, Sr. Maria Atília hutumikia kama daraja hai kati ya waamini wa siku hizi na maisha ya awali ya Mtakatifu Rita, ambaye malezi yake ya Kikristo yaliumbwa huko Roccaporena yenyewe. "Kila Dominika  Mtakatifu  huyo alikuja hapa kujiunga na sala ya pamoja," mtawa huyo alisema. "Hapa ndipo alipoishi maisha yake ya Kikristo kwa ukamilifu. Hapa ndipo alipojifunza kusali, kusamehe, na kumwomba Mungu neema ya msamaha na uongofu kwa mumewe. Pia aliomba amani ya eneo hilo. Wakati huo, mji huo uligawanywa na vikundi viwili vya wapinzani vikipigania madaraka, ugomvi ambao uliongezeka hadi umwagaji damu."

Safari ya kiroho na kijiografia kwenda Roccaporena

Leo, akitembea mitaa ya Roccaporena, mtawa huyu wa Brazil anatafuta kuhuisha urithi wa Mtakatifu Rita wa maisha yake, akibadilisha histiria ya mateso na msamaha kuwa uzoefu unaoonekana kwa mahujaji. Katika nyumba aliyozaliwa Rita, wageni wanaweza kuona utoto wake na mtindo wake rahisi wa maisha, kwa mfano, katika chumba kidogo alichozaliwa, na kupitia blanketi aliyokuwa akitumia wakati wa baridi, wakati halijoto ya ndani inaweza kushuka hadi nyuzi joto 20 chini ya sifuri. Ingawa kitambaa kiliharibika baada ya muda, blanketi ilipachikwa kwa umakini na uaminifu kwa kutumia vipande vya ngozi kutoka kwa ile ya asili.

Mahujaji huko Roccaporena
Mahujaji huko Roccaporena

Sr. Maria Atília pia huwaongoza wageni kupitia nyumba ambayo Rita aliishi kama mke, mama, na mjane kabla ya kuingia kwenye nyumba ya watawa, akionyesha mienendo ya familia na huzuni kubwa aliyovumilia. Kutoka hapo, mtakatifu angepanda mlima kusali kwenye Mwamba wa Maombi, kilele ambacho mahujaji bado hutembelea hadi leo, akipanda ngazi 314 hadi urefu wa mita 827. "Aliomba kwa undani kwa ajili ya uongofu wa mumewe, ambaye alikuwa mhalifu maarufu," Sr. huyo alieleza. "Rita angeondoka nyumbani kwake na kupanda mlima hadi kwenye jiwe kubwa jeupe, mahali pa sala si kwa ajili yake tu, bali pia kwa mahujaji wengi. Hata wakati huo, ilikuwa mahali pa kupumzika na kutafakari."

Kitanda cha Mtakatifu Rita wakati akiwa mdogo
Kitanda cha Mtakatifu Rita wakati akiwa mdogo

Leo hii, nyumba hiyo ya familia imekuwa "nyumba ya sala," kanisa lililo wazi kwa umma ambapo wanandoa wachanga wanaokaribia kuoa mara nyingi hukusanyika, kama mtawa huyo alivyosimulia. "Jambo la kuvutia ni kwamba hata leo, nyumba hii inawakaribisha vijana wanaokuja kutumia usiku kucha katika maombi usiku wa kuamkia harusi yao," alisema. "Kwangu mimi, hili lina nguvu sana. Mimi humfikiria Rita kila wakati, akiwa hapa na watoto wake, huku mumewe akipanga uhalifu. Na angemwomba Mungu aguse moyo wake. Au nafikiria Rita akiwalea watoto wake kwa upendo wa mama anayewatakia mema tu, akipitisha maadili ambayo mumewe hakuwa nayo. Hatujui kama alipanda mlima."

Mtakatifu Rita alipanda kilima hadi kikanisa hicho juu kusali na sadaka
Mtakatifu Rita alipanda kilima hadi kikanisa hicho juu kusali na sadaka

Wakati wa majira ya baridi kali, lakini hakika alikenda mchana, kwa sababu usiku isingewezekana. Huko juu, alihisi karibu na Mungu. Yeye ni mwanamke mkuu kweli, mtakatifu maalum sana.” Kutembelea mji mdogo wa Umbria, pamoja na nyumba zake za jadi za mawe na mandhari ya milima, pia kunajumuisha "Lazzaretto," ambayo inakumbusha upendo wa Rita kwa wagonjwa; Bustani ya maajabu, maarufu kwa muujiza wa waridi na tini ulioonekana katikati ya majira ya baridi kali; na Patakatifu pa Mtakatifu Agostino na Mtakatifu Rita,ni  kitovu cha kiroho cha Roccaporena.

Urithi wa maombi na msamaha

Pamoja na Sr. Maria Atília, mahujaji hawatembelei Roccaporena tu; wanafuatilia maisha ya Mtakatifu Rita na maadili yaliyomwongoza: sala na msamaha kama njia ya kuelewa ukuu wa Mungu. "Maisha ya Mtakatifu Rita yanagusa sana. Aliishi maisha ya sala sana, karibu na msalaba,” mtawa huyo alieleza, akifichua chanzo cha ndani kabisa cha matendo ya Mtakatifu. Ni katika mwanamke huyu wa maombi ambapo mmisionari wa Brazil alipata taswira ya maisha yake mwenyewe. Muda mrefu kabla ya kuwaongoza mahujaji huko Roccaporena, alikuwa ametembea njia zingine za umisionari, akivuka mipaka ya kijiografia na kitamaduni.

Waamini uwasha mishumaa kumuomba Mtakatifu Rita awaombee
Waamini uwasha mishumaa kumuomba Mtakatifu Rita awaombee

Sr hiyo alitoa huduma yake nchini Brazil, Italia, Ureno, Hispania, na Msumbiji. Alitumia zaidi ya miaka 15 katika taifa la Afrika kati ya Pemba, katika jimbo la Cabo Delgado, na Maputo nchini Msumbiji. Leo hii, akiwa na umri wa miaka 81, analeta uzoefu huo wa manufaa katika dhamira yake ya kuwakaribisha mahujaji na kusikiliza sala na shukrani zao. “Waliniuliza kama nipo tayari kuja hapa. Sijawahi kuchagua sehemu zangu za kwenda,” alisema. “Na leo, najisikia mwenye furaha kweli. Watu wanaonikutana huniambia kwamba ninaangaza furaha, kwa hivyo lazima nimshukuru Mungu. Ni baraka kwangu, lakini pia kwa kila mhujaji anayefika hapa, kwa sababu wanaondoka wakiwa na amani ya ndani na mtazamo tofauti wa maisha.”

NYAYO ZA MTAKATIFU RITA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

02 Juni 2026, 11:08