Tafuta

2026.05.01 CNEWA Yerusalemu kutoa msaada kwa Wapalestina huko Ukingoni mwa Gaza. 2026.05.01 CNEWA Yerusalemu kutoa msaada kwa Wapalestina huko Ukingoni mwa Gaza.  (© CNEWA Jerusalem)

Shirika la misaada Katoliki kuunga mkono juhudi za kutoa misaada kwa Wapalestina

Chama Katoliki cha Ustawi wa Mashariki ya kati(CNEWA)kimepeleka karibu dola milioni 1.2 kama msaada ili kusaidia juhudi za kutoa misaada unaofadhiliwa na Kanisa huko Gaza na Ukingoni mwa Magharibi tangu kusitishwa kwa mapigano kuanza Oktoba 2025.

Na Michael J. La Civita, CNEWA

Tangu kusitishwa kwa mapigano huko Gaza kulipoanza Oktoba 2025 Chama Katoliki cha Ustawi wa Mashariki ya kati(CNEWA kimepeleka karibu dola milioni 1.2 kwa ajili ya msaada ili kusaidia juhudi za kutoa misaada zinazofadhiliwa na Kanisa huko Gaza na Ukingo wa Magharibi. Alitangaza hayo rais wa shirika CNEWA, Askofu Peter I. Vaccari wa jimbo la Brooklyn na aliyekuwa mkuu wa Seminari ya Mtakatifu Yosefu huko Dunwoodie, New York, Marekani.

Timu ya CINEWA

Utume wa Kipapa ulioundwa kupitia timu ya CNEWA iliyoko Yerusalemu, ulitenga dola 457,635 kwa ajili ya familia zilizo katika mazingira magumu huko Gaza hasa Nyumba zinazoongozwa na wanawake zenye watoto wadogo, wazee, na watu wenye mahitaji maalum, ili kushughulikia ongezeko la ukosefu wa chakula, usaidizi wa usafi, na mavazi ya joto ili "kupunguza mateso ya kimwili ya haraka huku ikidumisha heshima ya familia zilizoathiriwa," ilibainisha ripoti ya mwisho ya timu hiyo  tarehe 29 Aprili. Ikiratibiwa kupitia Baraza la Makanisa ya Mashariki ya Kati na mshirika wa muda mrefu wa CNEWA-PMP huko Gaza, hufadhili vifurushi vya chakula vilivyopatikana na milo iliyofungashwa, vifaa vya usafi, na nguo za joto kwa familia zilizo hatarini zinazokaa kaskazini mwa Gaza na Jiji la Gaza.

Kuathiriwa kwa uchumi wa Palestina 

Ingawa kusitisha mapigano huko Gaza kunadorora, ubora wa maisha katika Ukingo wa Magharibi kwa familia nyingi za Wapalestina umeathiriwa vibaya kwa kutopata mahujaji na watalii kutokana na hali ya vita vya mara kwa mara vinavyoendeshwa na serikali ya Israeli. Hii imeathiri uchumi wa Palestina wa ndani, ambao unategemea utalii, na ongezeko la vurugu zinazoelekezwa kwa jamii za Wapalestina na walowezi wenye msimamo mkali, limeharibu zaidi utulivu wa jamii ya Wapalestina. Karibu nusu ya fedha zilizotolewa na Chama Katoliki vha Ustawi wa Mashariki ya kati(CNEWA) dola 507,550, zilielekezwa kwa ajili ya uundaji wa ajira na miundombinu ya jamii na miradi ya ustahimilivu katika Ukingo wa Magharibi. Timu ya CNEWA yenye makao yake makuu Yerusalemu ililenga jamii katika eneo la Bethlehem lenye watu wengi na lililoharibiwa kifedha na mji wa Taybeh, ambao licha ya kuwa mji pekee wa Kikristo uliobaki katika maeneo yaliyoko Ukingo wa Magharibi, umepitia mashambulizi mengi na walowezi wenye msimamo mkali, ikiwa ni pamoja na jaribio la kuchoma Kanisa lake la kale la Mtakatifu George.

Ikiwa imeratibiwa na Kanisa mahalia na mashirika yanayohusiana na Kanisa ambayo kwa pamoja hutoa wastani wa asilimia 40 ya huduma zote za kijamii kwa Wapalestina wanaoishi Mashariki mwa Yerusalemu, Gaza, na Ukingo wa Magharibi, jitihada hizi za uundaji wa ajira ziliimarisha miundombinu na huduma za jamii huku zikiwapa wakuu wa kaya wasio na ajira heshima, kazi, na kipato cha kusaidia familia zao.

Vifaa vya matibababu, dawa na huduma 

Salio la fedha, karibu $200,000, lilielekezwa kwa vifaa vya matibabu, dawa, na huduma kwa Hospitali ya Kianglikani  ya Al-Ahli, hasa kwa wale waliopata majeraha makubwa ya moto wakati wa vita pamoja na upasuaji wa dharura kwa watoto na vijana na kwa vifaa vya maabara katika kliniki ya mama na mtoto ya Baraza la Makanisa la Ukingo wa Mashariki  katika kitongoji cha Al-Rimal katika Jiji la Gaza. "CNEWA iliwashukuru wafadhili wake wengi," alisema Askofu Vaccari Rais  wa CNEWA, "ambao wameitikia kwa ukarimu wa  kilio cha maskini katika Nchi Takatifu." Fedha zilizotolewa na CNEWA tangu Oktoba 2025 zilikusanywa kwa sehemu za Parokia na Jimbo  la Marekani kujibu wito wa rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki la Marekani, Askofu Mkuu Timothy P. Broglio wa Shirika la Kijeshi la Marekani,  Columbus; Mashirika ya Kimataifa ya Kikristo ya Kiorthodox na watu binafsi Amerika ya Kaskazini na kwingineko.

MISAADA PALESTINA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

04 Mei 2026, 11:34