Tafuta

2026.05.04 Kanisa la Mtakatifru  Luis Maria de Monfort, Jimbo la Pemba,huko Cabo Delgado lilichomwa Moto 2026.05.04 Kanisa la Mtakatifru Luis Maria de Monfort, Jimbo la Pemba,huko Cabo Delgado lilichomwa Moto 

Msumbiji:unahitajika mshikamano baada ya Kanisa kuchomwa moto na wanajihadi

Wanajihadi walishambulia Parokia nyingine nchini Msumbiji, katika jimbo la Cabo Delgado.Askofu Juliasse Ferreira Sandramo aliomba mshikamano wa kimataifa akisema kwamba "kwa miaka tisa makanisa yameharibiwa na kuchomwa moto."

Na Roberto Paglialonga – Vatican.

Kanisa limechomwa na makazi ya Mapadre wa Shirika la Shule za Wacha Mungu waitwao wa (Piarist ) shirika la Kitawa lililoanzishwa na Mtakatifu Yoseph Calasanz mnamo 1617 jijini Roma, lililojitolea kwa ajili ya elimu ya vijana, hasa maskini; na Shule yao ya  chekechea pia vilishambuliwa. Kumekuwa na wimbi jipya la vurugu za wanajihadi huko Cabo Delgado, nchini Msumbiji, ambapo vita vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya miaka minane, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 6,200 na kuwafanya watu zaidi ya milioni 1.3 kuhama makazi yao. Sr. Laura Malnati, mkuu wa Kanda ya  Masista Wamisionari wa Comboni nchini, humi alizungumza na Gazeti la Baraza la Maaskofu katoliki Italia ‘Avvenire’ kuhusu shambulio hilo la hivi karibuni.

Wanamgambo walichoma majengo ya kijiji pia

Kwa mujibu wa  maelezo yake, manmo  Alhamisi, Aprili 30, wanamgambo wa Ahlu al-Sunna wa al-Jama'a—kikundi cha wenyeji chenye uhusiano na kinachoitwa Serikali ya Kiislama( Islamic State (IS)) na kimekuwa kikifanya mashambulizi tangu 2017, walishambulia kijiji cha Meza, katika Wilaya ya Ancuabe, Kaskazini mwa jimbo Katoliki la Cabo Delgado. "Walichoma majengo ya kijiji. Kwa bahati nzuri, Mapadre walipewa onyo mapema na wakafanikiwa kuondoka huko Meza kabla ya magaidi kufika, Sr. alisimulia, akiwa bado anatetemeka. Wanamgambo hao pia waliharibu nyumba kadhaa, pamoja na kuchoma baadhi ya majengo ya Parokia. Parokia hiyo,inayosimamiwa na Matakatifu mlizi Louis de Montfort na lililojengwa mwaka 1946, linachukuliwa kuwa ishara ya uwepo wa Wakatoliki katika eneo hilo.

Mshtuko katika jumuiya ya kijamii

Katika ujumbe wa  Shirika la Kanisa Hiatji (Aid to the Church in Need,) Askofu António Juliasse Ferreira Sandramo wa Pemba, mji mkuu wa Cabo Delgado, alielezea kwamba wanamgambo hao walifika yapata saa kumi jioni na kuingia kanisani, na kuliteketeza kabisa. "Tukio hili lilikuwa la hofu sana. Kila kitu kiliharibiwa kabisa. Wakati wa shambulio hilo, raia walikamatwa na kutumiwa kama chambo cha  ujumbe wa chuki. Wamisionari wako salama, lakini jumuiya nzima  imeshtuka." Hata hivyo, aliongeza, "imani ya watu hawa haitaharibiwa kamwe."

Wito wa mshikamano wa kimataifa

Askofu kisha alizindua wito wa mshikamano wa kimataifa na waathiriwa wa vurugu katika eneo hilo. "Tunaomba umakini na mshikamano. Kwa karibu miaka tisa, makanisa katika jimbo yameshambuliwa, kuharibiwa, na kuchomwa moto." Cabo Delgado ni mojawapo ya  Mkoa maskini zaidi nchini Msumbiji, ambayo yenyewe ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani. Hata hivyo, kaskazini mwa nchi hiyo kuna utajiri wa migodi na akiba ya gesi asilia, na makampuni mengi ya Magharibi yanahusika katika uchimbaji wa rasilimali hizo. Kwa sababu ya vurugu hizo, kulingana na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi, zaidi ya watu 110,000 walilazimika kukimbia makwao mwaka 2025.

Imeasasishwa tarehe 4 Mei 2026 saa 5.00 asibuhi na Sr Christine  Masivo.

Kanisa kuchomwa moto Msumbiji

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

04 Mei 2026, 11:28