Tafuta

Kituo cha Televisheni ya Tv2000 na InBlu radio Kituo cha Televisheni ya Tv2000 na InBlu radio 

Tv2000:Makala ya "Nguvu ya upole,"kuhusu Papa Leo XIV

Ni Safari kupitia nyakati kali na muhimu zaidi za mwaka wa kwanza wa upapa wake,ikiakisi pia kupitia ushuhuda mbalimbali,kujitolea kwake kwa amani na haki ya kijamii,mwendelezo wa ufunguzi wa kichungaji baada ya Wosia wa kitume wa Papa Francisko wa Evangelii Gaudium,chaguo na mtindo ambao Papa Prevost alijiwasilisha kwa ulimwengu na kuongoza Kanisa.

Vatican News

"Nguvu ya Upole," ni makala kuhusu miezi kumi na miwili ya kwanza ya upapa wa Papa Leo XIV, iliyotayarishwa na mtangazaji wa Baraza la Maaskofu wa Italia, ambayo itaoneshwa Ijumaa, tarehe 8 Mei 2026 saa 3:10 usiku  kwenye Tv2000. Ni safari kupitia nyakati kali na muhimu zaidi: Kujitolea kwake kwa ajili ya  amani na haki ya kijamii, mwendelezo wake wa uchungaji baada ya Wosia wa kitume wa Papa Francisko wa Evangelii Gaudium, na ziara zake, chaguo zake, na mtindo ambao Papa Prevost alijiwasilisha kwa ulimwengu na kuliongoza Kanisa. Mtindo uliooneshwa na upole, uliojikita sana katika Injili na Tasaufi ya Kiagostinian, hasa kwa sababu hiyo inauwezo wa kwenda kinyume na mantiki katika muktadha wa kimataifa uliooneshwa na migogoro ya vurugu na kiburi cha wenye nguvu.

Hati ya maandishi ya Gennaro Ferrara imeimarishwa na ushuhuda wa watu walio karibu na Papa na waangalizi wenye mamlaka: Kardinali Baldo Reina, Makamu Jimbo Kuu la Roma ; Vincenzo Buonomo, Mkuu wa  Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana na mwanaharakati wa kimataifa; Padre Pasquale Cormio, Msimamizi wa Basilika ya Mtakatifu Agostino Roma; Padre Sergio Massironi, Mtaalimungu katika Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu; Elise Ann Allen, mwandishi wa Crux na mwandishi wa wasifu wa Papa Leo XIV (Nyumba ya Uchapishaji  Mondadori,) ni matokeo ya simulizi ya ushirikiano ambayo, katika muda wa kama saa moja, inafupisha vyema mwaka wa kwanza wa upapa wake, ikiakisi sifa tofauti za Papa Leo XIV ambazo mara nyingi hubaki zimetengwa katika habari za kila siku za vyombo vya habari. Makala hii itapatikana kwa mahitaji kwenye: Play2000, programu ya Tv2000, na inBlu2000.

TV2000 NA PAPA LEO XIV

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

06 Mei 2026, 09:29