Tafuta

Watawa nchini Colombia  mara baada ya misa ya Jubilei mbalimbali za maisha ya wakfu. Watawa nchini Colombia mara baada ya misa ya Jubilei mbalimbali za maisha ya wakfu.  #SistersProject

Colombia:Kujitolea kupyaisha utume na jumuiya na miito

Kanisa nchini Colombia liliadhimisha Juma la Kitaifa ya kwa ajili ya Maombi ya Miito 2026 kama wakati wa neema,tafakari,na ari mpya ya kimisionari.Kwa kuongozwa na mada: "Yesu anaita, analeana anatuma katika jumuiya,"mpango huo uliakisi wito kama safari ya pamoja ya Kikanisa iliyohamaishwa kupitia sala na kutembea pamoja.Katikati ya kupungua kwa idadi ya mapadre, Kanisa linawaita waamini wote kuhamasisha miito na kuimarisha kujitolea kwao kwa uinjilishaji.

Na Sr. Christine Masivo CPS – Vatican.

Kuanzia Aprili 26 hadi Mei 3, 2026, Kanisa Katoliki nchini Colombia liliungana katika Juma la  Kitaifa la Maombi kwa Ajili ya Miito, mpango ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu wa Colombia. Sanjari na Siku ya 63 ya Maombi ya Miito Duniani, iliyoadhimishwa Dominika ya Nne ya Pasaka, na nia ya kichungaji kwa ajili ya hitaji la kudumu la miito ndani ya Kanisa.

Wito wa kitaifa kupitia maombi na utambuzi

Siku hiyo ya maombi ya kimataifa iliyoanzishwa mwaka 1964, na Papa Paulo VI, iliakisi mwaliko wa Injili wa kumwomba Bwana atume watenda kazi katika mavuno Yake. Nchini Colombia, maadhimisho haya yalipanuka na kuwa kwa Juma nzima lililojitolewa   kuimarisha ufahamu, kuhimiza utambuzi, na kuhuisha roho ya umisionari katika jumuiya za kikanisa.

Yesu anaita,analea na kutuma katika jumuiya

Mada ya mwaka huu ilisisitiza mwelekeo wa kijumuiya wa wito. Iliwasilisha wito si tu kama wito wa mtu binafsi bali kama zawadi inayokuzwa ndani ya maisha ya Kanisa. Mwongozo wa kichungaji ulioandaliwa kwa ajili ya Juma  hilo uliosisitiza kwamba kila wito, mlei, Padre, Mtawa au wa familia, uliibuka kutumikia jumuiya ya Kikristo. Mpango huu uliwaalika waamini kutambua upya wito kama njia ya kukua, ya huduma, na ya utakatifu. Uliakisi Kanisa kama mazingira hai ambapo watu binafsi wanakaribishwa, kuongozwa, na hatimaye kutumwa katika utume. Katika maono haya, wito unakuwa safari yenye nguvu inayoundwa na mahusiano, malezi ya imani, na ushiriki hai katika maisha ya kikanisa.

Safari ya wito katika hatua za maisha

Juma la  Maombi  kwa kawaida hujitokeza kupitia njia ya kichungaji iliyopangwa ambayo huunganisha liturujia, katekesi, sala, na uzoefu wa kijumuiya. Katika mkutano ulianza na Misa ya Dominika, iliyoelezwa kama "chanzo na kilele cha kila wito," na iliendelea na tafakari za mada zinazoshughulikia hatua tofauti za maisha. Utoto Mtakatifu kadhalika uliakisiwa kama wakati muhimu wa kusikiliza, ujana kama kipindi cha utambuzi, na familia kama mahali pa msingi ambapo miito hulelewa kwanza. Programu pia ilihusisha  umuhimu wa kuwa karibu na kutembea na watawa na mapadre.  Wakati muhimu sana katika Juma hilo ulikuwa "Masaa 24 na Bwana", ambapo ni wakati wa kuabudu Ekaristi Takatifu, kuimarisha umoja ndani ya Kanisa na kuamini muongozo wa Roho Mtakatifu, ukiimarisha sala kama msingi wa Utume wa kuhamasisha miito.

Changamoto ya kupungua  kwa miito

Mpango huu unasisitizwa na takwimu za Kimataifa na za ndani kinachoonesha kupungua kwa kasi kwa idadi ya mapadre duniani kote, mwenendo huo  unaoonekana hasa Marekani. Nchini Colombia, yenye takriban ya Wakatoliki milioni 48, na kuna mapadre wapatao 9,700 pekee wanaohudumia zaidi ya Parokia 4,600 katika eneo kubwa. Hii inasababisha uwiano wa Padre mmoja kuhudumia watu 5,000, na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya kichungaji kwa mapadre. Licha ya changamoto hizi, Kanisa linaendelea na utume wake kupitia mtandao imara unaojumuisha zaidi watawa 11,000, makatekista 51,000, na wamisionari walei wapatao 73,000. Kujitolea kwao kunaonesha Kanisa lililo hai linaloendelea katika uinjilishaji hata katikati ya uhaba wa utume wa kuhimiza miito.

Utume,ushirika na matumaini

Kanisa nchini Colombia linasisitiza mara kwa mara uhusiano wa ndani kati ya wito na utume. Mtazamo huu unahamasisha "Kanisa linaloendelea," ambapo kila mtu aliyebatizwa anashiriki jukumu la kuhamasisha wito na kueneza Injili. Kujitolea huko pia kunaonekana katika kuwatuma Mapadre kama Wamisionari nje ya mipaka ya Kitaifa, na kuimarisha ushirika miongoni mwa Makanisa mahalia duniani kote. Viongozi wa Kanisa walikisi ustahimilivu wa Mapadre wanaohudumu chini ya hali ngumu, ambazo mara nyingi huashiriwa na umaskini, vurugu, na kutengwa kijiografia. Kwa hivyo, Juma la Kitaifa kwa ajili ya  Maombi ya Miito ilikuwa zaidi ya tukio la kichungaji, ni wito wa matumaini. Kwa sala, Jumuiya na mpango wa kuhimiza miito, ilithibitisha wazi wito kama "mradi wa upendo na furaha," ukiwaalika waamini wote kusikiliza, kujibu, na kushiriki katika utume wa Mungu kwa ukarimu na imani.

Colombia miito

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

05 Mei 2026, 16:05