Peter Gates ateuliwa kuongoza Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu,Australia
Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.
Uteuzi wa Peter Gates unaashiria kilele cha kujitolea kwa muda mrefu kwa maisha ya umisionari na huduma ndani ya Kanisa Katoliki, na uongozi wake kwa miaka ijayo. Huyo ni Bwana Peter Gates aliyezaliwa Sydney mnamo 1959, wito wake haukuanza katika vyumba vya mikutano bali katika mandhari ya vijijini ya Zambia, ambapo alihudumu kwa kujitolea kama mwalimu kuanzia 1987 hadi 1989. Katika miaka hii ya malezi, alijikita katika maisha ya jamii akiwafundisha, na kuwashauri waelimishaji wa eneo hilo, na kusaidia programu za Katekisimu katika wilaya iliyotengwa. Kujitolea kwake katika miaka yake ya ujana, uliweka msingi dhabiti katika uelewa wake wa kazi ya huruma ya vitendo wa kina wa utume katika ngazi ya chini. Aliporudi Australia, Gates alijiunga na Utume wa Kikatoliki na majukumu mbalimbali kwa uwajibikaji, akipanda ngazi katika nyadhifaa kadhaa. Kazi yake imeonesha uhusiano wa kazi yake wa usikivu wa kichungaji na ujuzi wa shirika hili, na kumfanya kuwa mtu anayeheshimika katika wadhifaa huu wa utume.
Uongozi wa maono na ushirikiano
Kwa zaidi ya miongo mitatu, Gates amekuwa na jukumu muhimu katika kuunda uhamasishaji wa kimisionari nchini Australia. Kuanzia siku zake za mwanzo kama Afisa wa Elimu hadi muda mrefu aliohudumu kama Naibu Mkurugenzi wa Kitaifa, amekuwa muhimu katika kuunda programu za malezi na kuongoza mikakati ya kitaifa. Uongozi wake ulichangia pakubwa katika mpango mkakati wa 2022-2025, kwa msisitizo mkubwa juu ya sinodi, akihimiza kusikiliza, kushiriki, na uwajibikaji wa pamoja katika Kanisa lote. Ushawishi wake unaenea zaidi ya utawala. Gates amekuza kikamilifu ushiriki wa vijana kupitia programu za kimataifa za kujiweka katika nchi kama vile Timor-Leste, Mongolia, Kambodia, na Ufilipino. Mipango hii imesaidia kuunda kizazi kipya cha Wakatoliki wenye mtazamo wa kimisionari wa kimataifa, unaotegemea mshikamano na uelewa wa kitamaduni.
Kutumikia Kanisa, nyumbani na nje ya nchi
Mchango wa Gates kwa Kanisa pana nchini Australia pia unaonekana. Ushiriki wake katika Baraza la Tano la Wajumbe wa 2018 hadi 2022, ikiwa ni pamoja na jukumu lake kama Mratibu Kiongozi aliyekaimu, unaakisi kujitolea kwake kwa mazungumzo na ufufuko ndani ya Kanisa. Kupitia mawasilisho muhimu na juhudi za ushirikiano, amekuwa akitetea Kanisa linalozingatia utume na sinodi kila mara. Kimataifa, ushiriki wake katika vikundi vya kazi vya Mashirika ya Kipapa ya Misheni unaonyesha ushiriki wake na mienendo ya utume duniani, hasa katika mawasiliano, ufadhili wa fedha, na mabadiliko ya kidijitali.
Kazi yake imesaidia kuunda desturi zinazounga mkono juhudi za utume katika miktadha mbalimbali ya kitamaduni. Anapoingia katika nafasi yake mpya kama Mkurugenzi wa Kitaifa wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu wa Australia, Peter Gates haleti uzoefu tu, bali maono wazi yaliyojikita katika imani, huduma, na ushirikiano. Uongozi wake unaahidi kuimarisha mchango wa Australia kwa utume wa Kanisa kwa wote, ukihamasisha jamii kukumbatia wito wao wa kushiriki Injili kwa nguvu mpya na umoja.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.