Tafuta

2026.04.21 Kituo cha Magonjwa ya Akili na urejeshaji cha Jean-Pierre Olie,Guinea ya Ikweta. 2026.04.21 Kituo cha Magonjwa ya Akili na urejeshaji cha Jean-Pierre Olie,Guinea ya Ikweta.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV,Hospitali ya magonjwa ya akili:Ziara ya Papa itasaidia kujumuisha wote!

Kabla ya kuwasili kwa Papa Leo XIV katika Hospitali ya magonjwa ya Akili huko Malabo, wafanyakazi walizungumza na Vatican News kwamba ziara hiyo itatuma ujumbe mkubwa wa "fundisho kubwa"kuhusu umuhimu wa huduma ya afya ya akili.Mnamo Desemba 2025,Hospitali ilibadilishwa jina kwa heshima ya Daktari maarufu wa magonjwa ya akili wa Ufaransa Jean-Pierre Olié,mwanzilishi wa kituo.

Na Joseph Tulloch – Malabo.

Katika Hospitali ya Magonjwa ya Akili ya Jean-Pierre Olie huko Malabo, Guinea ya Ikweta, maandalizi yaliendeliwa vizuri kwa ajili ya kufika kwa  Papa Leo XIV. Nembo rasmi ya ziara ya Papa, yenye kauli mbiu: "Kristo, nuru ya Guinea ya Ikweta, kuelekea mustakabali wa matumaini", ilibandikwa nje ya majengo, na safu za viti zimechorwa katika banda la kati ambapo wagonjwa na wafanyakazi wangekusanyika  kusikiliza kutoka mawaidha kutoka kwa Papa. "Ni heshima kubwa", alisema Profesa Bechir Ben Hadj Ali, daktari wa Tunisia ambaye anahudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo. Ziara ya Papa ni "ishara muhimu sana", alisisitiza, ambayo alisema inaakisi umuhimu wa afya ya akili nchini Guinea ya Ikweta na duniani kote.

Papa akikaribishwa katika Kituo cha magonjwa ya akili
Papa akikaribishwa katika Kituo cha magonjwa ya akili   (@Vatican Media)
Papa alitembelea kituo cha magonjwa ya akili
Papa alitembelea kituo cha magonjwa ya akili   (@Vatican Media)

Wagonjwa 125 wanaume kwa wanawake wenye ugonjwa wa akili,mfadhika na uraibu

Kituo hicho, ambacho ni cha aina yake pekee nchini, kilianzishwa muongo mmoja uliopita, mwanzoni kikiwa na vitanda 25 pekee. Kwa sasa kina vitanda 146, vilivyogawanywa katika Wodi sita. Kwa sasa, kinawatunza wagonjwa wapatao 125 (wanaume 100 na wanawake 25) wanaoishi na ugonjwa wa akili, mfadhaiko, wasiwasi, na uraibu wa dawa za kulevya. Mnamo Desemba 2025, Hospitali hiyo ilibadilishwa jina kwa heshima ya Daktari maarufu wa magonjwa ya akili wa Ufaransa Jean-Pierre Olié, ambaye alikuwa mhusika mkuu katika kukianzisha.

Papa akiwatia moyo katika kituo cha magonjwa ya akili
Papa akiwatia moyo katika kituo cha magonjwa ya akili   (@Vatican Media)
Papa alitembelea kituo cha magonjwa ya akili
Papa alitembelea kituo cha magonjwa ya akili   (@Vatican Media)

Kutelekezwa wenye magonjwa ya akili

Msaada wa Mke wa Rais Constancia Mangue de Obiang pia ulikuwa muhimu, alisema Profesa Ben Hadj Ali. Daktari huyu wa Tunisia alisisitiza, kwamba  duniani kote, hasa barani Afrika, afya ya akili mara nyingi huchukuliwa kimakosa kuwa sio jambo la muhimu, na kwa hivyo alitumaini ya kwamba ziara ya Papa itatuma ujumbe ulio mzito kuhusu umuhimu wa kuwatunza wale wanaougua magonjwa ya akili. Daktari Engracia Asangono Nchuchuma, Naibu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, alielezea kwamba muundo huo hivi karibuni umebadilika kuelekea mfumo wa huduma inayotegemea jamii. Hospitali hiyo haitoi tu ushauri wa magonjwa ya akili na kisaikolojia kwa wagonjwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, bali pia ina timu inayoyoenda nje na kuwatembelea na kuwahudumia wagonjwa ambao, kwa sababu mbalimbali, hawawezi kuhudhuria uchunguzi  wao wa kimatibabu.

Umuhimu wa kujali wagonjwa wote bila kubagua
Umuhimu wa kujali wagonjwa wote bila kubagua   (@Vatican Media)

Ujio wa Papa Leo XIV utasaidia kuwatambua na kuwajali wagonjwa wote bila kuwatenga

Zaidi ya hayo, hivi karibuni imefungua kitengo cha magonjwa ya akili kwa watoto ili kushughulikia mahitaji yanayoongezeka miongoni mwa watoto wadogo. Juhudi zinafanywa pia ili kukidhi mahitaji ya kiroho ya wagonjwa, alisema Dk. Asangono Nchuchuma, ikiwa ni pamoja na sherehe za Misa na maandalizi ya ziara ya Papa. Ujio wa Papa Leo XIV, alisisitiza, "utasaidia kila mtu kuwaona watu wenye magonjwa ya akili si kama watu binafsi wa kutengwa, bali kujumuika katika jamii zetu."

Papa ni Baba wa wote
Papa ni Baba wa wote   (@Vatican Media)

Imesasishwa tarehe 24 Aprili 2026  saa  7:54 mchana na Sr Christina Masivo.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

24 Aprili 2026, 13:54