Mkuu wa Basilika ya Mtakatifu Agostino,Annaba:'Waalgeria wafurahi kwa ziara ya Papa Leo XIV
Olivier Bonnel -mwakilishi Annabana na Deborah Castellano Lubov- Vatican
"Watu wanafurahi sana kwamba Baba Mtakatifu, Papa Leo XIV, anatutembelea na sio sisi Wakristo tu, bali watu wa Algeria, na hasa hapa Annaba, ambapo Agostino alifanya kazi kama Askofu na akafariki." Katika mahojiano na Olivier Bonnel mwandishi wetu wa Vatican News huko Annaba, Padre Wekesa alishirikisha mawazo yake wakati Papa Leo XIV akifanya Ziara yake ya Kitume kwa taifa la Algeria kati ya ziara yake ya nchi nne barani Afrika.
Papa ametembelea wote si wakristo bali hata wasio wakristo
Ziara ya Papa Leo nchini Algeria iliashiria ziara ya kwanza kabisa ya Papa nchini humo. "Hali ya hewa hapa imejaa furaha," Padre Wekesa alibainisha. "Nina furaha sana, na pia ndugu zangu. Tunafurahi sana kwamba Baba Mtakatifu, ametutembelea na sio tu kututembelea sisi Wakristo, bali watu wa Algeria, na hasa hapa Annaba." Alikumbuka furaha ya Annaba wakati Papa wa kwanza Mmagostiniani Papa Leo XIV, alipochaguliwa mnamo Mei 8 , 2026: "Ilikuwa furaha kwa kila mtu hapa," Padre huyo alikumbuka.
“Kaka na dada wengi ambao ni Waislamu walitutumia ujumbe wa pongezi. Kwa nini? Kwa sababu, kama Baba Mtakatifu, yeye ni mwana wa Mtakatifu Agostino. Hilo lilisikika." Mtakatifu Agostino mkuu wa Kanisa hilo alisema, ndicho kinachoendelea kuwaunganisha Waalgeria na Baba Mtakatifu mara moja. "Ni Agostino," alielezea, "kwa sababu Agostino alizaliwa hapa, alikuwa Askofu hapa, na alikufa hapa. Kwa hivyo Agostino ni sehemu muhimu ya kinasaba cha Waalgeria. Hilo pekee lilikuwa furaha kwao, na kwa hivyo wanafurahi kukutana naye."
Akisisitiza ziara ya Papa kama tukio la kitaifa, Padre Wekesa alisisitiza, "Sio kwetu Wakristo tu, ambao ni wachache, bali ni tukio la kitaifa kwa Waalgeria wote." "Serikali ilimwalika kama Papa, lakini kwetu sisi, tunataka kumkaribisha kama mshirika. Tunatambua kwamba yeye ni Papa, lakini yeye ni Muagostiniani. Ukishakuwa wa Shirika la Kiagostino aliongeza, "wewe ni Muagostiniani milele." Hatimaye, mkuu wa Basilika ya Mtakatifu Agostino alieleza kwamba Papa Leo XIV ni Muagostiniani sana katika mtazamo wake, hasa kuelekea amani. "Ziara yake ni sehemu ya mazungumzo kati ya dini mbalimbali ili kuendeleza ujumbe wa amani. Kwa maneno na matendo yake, anatetea amani, akifuata nyayo za Mtakatifu Agostino."
Imesasishwa saa 4.41 asubuhi tarehe 15 Aprili 2026 na Angella Rwezaula
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here