Guinea-Bissau:Maelfu ya vijana washerehekea Siku ya IX ya Vijana Wakatoliki kimajimbo!
Na Casimiro Jorge Cajucam – Bissau.
Kwa kuongozwa na kauli mbiu "Imani, Upendo na Matumaini,"jiji la Bafatá lilipitia siku tatu zilizojaa hali ya kiroho, furaha, na ushirika. Licha ya joto kali, ambalo lilikuwa kati ya nyuzi joto 42 na 43 kipimo cha Selsiasi, shauku na uchangamfu wa washiriki haikupungua. Shughuli zilianza Ijumaa alasiri, tarehe 24 Aprili ambapo vijana walikaribishwa na kusalimiwa na Askofu Vítor Quematcha wa Bafatá, na kufuatiwa na usiku ya kuabudu mbele ya Ekaristi Takatifu. Askofu Quematcha alitoa Katekesi yake kwa vijana na familia za waamini Wakatoliki waliohudhuria. Baadaye, Askofu José Lampra Cá wa Bissau aliadhimisha Ibada ya Misa Takatifu.
Maaskofu na Mwakilishi wa Vatican walitembelea gereza
Kabla ya kuadhimisha Misa Takatifu, wafungwa katika Kituo cha Gereza la Bafatá walitembelewa na viongozi kadhaa wa Kanisa, akiwemo Askofu José Lampra Cá, Askofu José Câmnate na Bissiga (Askofu Mstaafu wa Bissau), na Balozi wa Vatican nchini Guinea Bissau Askofu Mkuu Waldemar Stanislaw Sommertag, akiambatana na mapadre kadhaa. Wakati wa ziara hiyo, wafungwa walipokea zawadi ya mashati yenye mada ya Jubilei na vitu vya Siku ya Vijana, pamoja na vifaa vya usafi wa binafsi. Mpango huu ulikusudiwa kuonesha ukaribu na mshikamano wa Kanisa, na wafungwa.
Misa ya kufunga, iliyofanyika siku ya Dominika, tarehe 26 Aprili 2026 iliongozwa na Balozi wa Vatican nchini Guinea Bissau, Askofu Mkuu Sommertag, huku mahubiri yakitolewa na Askofu Vítor Luís Quematcha. Katika ujumbe wake, Askofu alisisitiza kwamba "kumfuata Kristo si hisia ya kidini tu bali ni uamuzi wa maisha." Aliongeza kuwa, "katika muktadha wa Guinea, hii ina maana ya kuchagua ukweli badala ya uongo, na haki badala ya ufisadi."
Nchi inahitaji vijana wake
Askofu Vítor Quematcha aliwakumbusha vijana kwamba "Kanisa linawaamini na kwamba nchi inahitaji kujitolea kwao," aliwomba wawe na ujasiri na matumaini. Pia aliwasalimia familia zilizokuwepo, na alisisitiza kwamba "jukumu lao la msingi kama nafasi ya kusambaza imani, upendo, na uwajibikaji." Askofu huyo pia alikabidhi Jimbo la Bafatá na Bissau zikijiandaa kusherehekea jubilei ya miaka 50 mwaka ujao kwa Mchungaji Mwema. Katika kuaga na baraka ya mwisho, Askofu Mstaafu wa Bissau, José Câmnate na Bissign, aliwasihi watoto wanaokwenda shuleni na vijana kuchukua jukumu kubwa katika kuhamaisha upatanisho na amani nchini Guinea-Bissau.
Imesasishwa na tarehe 30 Aprili 2026 saa 5.50. na Christine Masivo, CPS – Vatican.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.